ARUSHA: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa kwa Amri ya Mkuu wa Mkoa

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alitoa amri Jana kwa jeshi la polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA ambaye ni mwenyekiti wa wilaya ya Arumeru na viongozi wengine wa mkoa wa Arusha CHADEMA kwa kudhaniwa kuhamasisha wananchi kuharibu mashine za kilimo cha umwagiliaji zenye gharama ya tsh.million 16, na kuwatuhumu viongozi hao kuitisha maandamano mpaka sasa hivi wapo mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea mpaka sasa ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Mkoa huyo wa mkoa wa Arusha Gambo amesema wasipewe dhamana wakae polisi mpaka kesi itakapoisha.

Chanzo:Waandishi wa habari Arusha
 
Kinacho fanywa saivi na viongozi wetu ni kubaka demokrasia.
Sheria ina semaje kuhusu utaratibu wa kumkamata mwalifu,aina ya kosa pamoja na utaratibu wa mdhamana
 
Ni aibu sana kukosa mbinu za kuwashawishi wananchi wa eneo lako na badala yake kutumia mabavu
 
Episode mpya ya Gambo amepiga Cleincy Camp amehamia Mang'ola.Anatafuta za kampeni yake ya ubunge 2020.
 
Mkuu wa mkoa wa arusha gambo alitoa amri Jana kwa jeshi la polisi kuwakamata viongozi wa chadema ambaye ni mwenyekiti wa wilaya ya arumeru na viongozi wengine wa mkoa wa arusha chadema kwa kudhaniwa kuhamasisha wananchi kuharibu mashine za kilimo cha umwagiliaji zenye gharama ya tsh.million 16, na kuwatuhumu viongozi hao kuitisha maandamano mpaka sasa hivi wapo mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea mpaka sasa ukikamilika watafikishwa mahakamani .

Mkoa huyo wa mkoa wa arusha gambo amesema wasipewe dhamana wakae polisi mpaka kesi itakapoisha .

Source.waandishi wa habari arusha
kwani wananchi hawaoni mpaka waambie, basi hata kura nazo tutakuwa tunaambiwa kampigie kura si unaona pa kumpigia kura, sasa wakiona hawajahusika na wakamfungulia kesi je atawalipa muda aliowapotezea, hivi Khalfani Liundi vipi ndo washamuweka jela,
 
Hiyo ni vita ya siasa.
nimesoma uzi 1 ukisema msajili wa mahakama anasema mahakama hazifanyi kazi kisiasa, sasa hapa ni nini,
Hiyo ni vita ya siasa.
nimesoma uzi 1 ukisema msajili wa mahakama anasema mahakama hazifanyi kazi kisiasa, sasa hapa ni nini, nahisi kuna sababu tu ya wananchi kufanya vile hawawezi from nowhere wakachoma tu, lama kuna kitu watawala walifanya kikawakera wananchi na kuhusu hizo machine, wananchi huwa hawakurupuki tu
 
Viongozi waaache kabisa mambo ya double Standard.
Tumekuwa tukishuhudia ukandamizaji mkubwa wa sheria,utawala wa mabavu eti waonekane ni watendaji wazuri.
Cheo ni dhamana,tena vyeo vyenyewe vya kuchaguliwa,mbaya zaidi vijana ndo wanafanya mambo ya ajabu.
HUWA NAJIULIZA SIKU WAKIPIGWA CHINI SIJUI WATAKUWA WAGENI WA NANI
 
Mh.Gambo huruma imemzidi mno, Hao walitakiwa siyo kukamatwa tu, wapigwe na viboko na kuteswa sana hadi waache hizo tabia za kichochezi.
 
nimesoma uzi 1 ukisema msajili wa mahakama anasema mahakama hazifanyi kazi kisiasa, sasa hapa ni nini,

nimesoma uzi 1 ukisema msajili wa mahakama anasema mahakama hazifanyi kazi kisiasa, sasa hapa ni nini, nahisi kuna sababu tu ya wananchi kufanya vile hawawezi from nowhere wakachoma tu, lama kuna kitu watawala walifanya kikawakera wananchi na kuhusu hizo machine, wananchi huwa hawakurupuki tu
Hapo inaleta picha kwamba saizi sheria haina nguvu tena.
 
Tatizo la upinzani wa hapa ni kupinga kila kitu, kama kweli wameharib u miundo mbinu na umwagiliaji na kuhamasisha maandamano wafungwe kabisa.
 
Ukweli hata sioni haja ya kuwepo mahakama na bunge. Hawa wote wamezidiwa, hela zetu tu za bure wanalipwa, maana kama haki haisimamiwi hamna haja ya wao kuwepo na kulipwa. Ukweli mchungu lakini acha tuseme.

Wangepumzishwa hadi 2020 warudishwe kazini. Bunge lisiwepo, mahakama zisifanye kazi, nchi iongozwe hivyo hivyo kwa utashi wa viongozi wenyewe, ikishanyooka wanavyotaka wao basi warudishe demokrasia kama ilivyokuwa.
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alitoa amri Jana kwa jeshi la polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA ambaye ni mwenyekiti wa wilaya ya Arumeru na viongozi wengine wa mkoa wa Arusha CHADEMA kwa kudhaniwa kuhamasisha wananchi kuharibu mashine za kilimo cha umwagiliaji zenye gharama ya tsh.million 16, na kuwatuhumu viongozi hao kuitisha maandamano mpaka sasa hivi wapo mikononi mwa polisi na upelelezi unaendelea mpaka sasa ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Mkoa huyo wa mkoa wa Arusha Gambo amesema wasipewe dhamana wakae polisi mpaka kesi itakapoisha.

Chanzo:Waandishi wa habari Arusha
Dhamana ni suala la kisheria, sio mpaka hisani ya Mkuu wa Mkoa.
 
Back
Top Bottom