[QUOTE][quote="VUTA-NKUVUTE, post: 6623987"][COLOR=#222222][FONT=Verdana]Niko hapa Arusha tangu juzi. Nimetembea viunga mbalimbalivya Arusha kuongea na kujionea hali ilivyo hapa. Nimesikia na kuona. Jana, name nilikoswa na mabomu ya machozi pamoja na risasi (za mpira na moto)pale Soweto.[/FONT][/COLOR]
[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Leo, nilikuwa Mahakamani kushuhudia kufikishwa na kusomewa mashtaka viongozi kadhaa waandamizi wa CHADEMA Taifa pamoja na watu wengineo waliokamatwa jana Soweto.Wamo Mbunge Said Arfi na Mawakili Wasomi Tundu A.M. Lissu na Mustafa Akoonay.Wamesomewa mashtaka tuliyoyazoea. YALE YALE. Kufanya kusanyiko lisilo halali. Nimeachamaombi ya dhamana yakiwasilishwa.[/FONT][/COLOR]
[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Wana-Arusha wanataka CHADEMA. Wanaishi na kuiamini CHADEMA. Mioyo yao inaongozwa na CHADEMA. CHADEMA inapendwa kwakuwa inahoji,inaahidi,inafanya pamoja na wananchi,inazungumza nao na kushiriki nao kijamii.Wako hivyo. Kwa hapa Arusha, 'chama tawala' ni CHADEMA. Hali hii inakera watawala-CCM. CCM wanajiona wanapuuzwa Arusha. Hawasikilizwi.Hawaheshimiwi. Hawashangiliwi. Hawasindikizwi. CCM inataka 'kutawala' Arusha.Ni jambo linalowezekana. [/FONT][/COLOR]
[COLOR=#222222][FONT=Verdana]CCM ifanye mema na kuishi na wanachi wao vile wapendavyo.CHADEMA wanaweza kuzidiwa kwa ukarimu na utekelezaji na usimamiwaji wa Ilani ya CCM tu. Si vinginevyo. Ni dhahiri kuwa wana-Arusha walishachagua Madiwani waohata kabla ya kuahirishwa uchaguzi kufuatia mlipuko wa bomu pale Kimandolu.Wanawajua na kujulikana. Ni wa CHADEMA. [/FONT][/COLOR]
[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Siasa safi inatoa nafasi ya kujipanga na kujiuliza kuelekea kujiboresha. CCM yaweza kujipanga,kujiuliza na kujiboresha hata kama hakitapatahata Kata moja ya Arusha. CCM bado ina wanachama wengi tu watiifu hapa Arusha.Iwatumie hao kuimarisha chama hapa. Siasa ina matunda yake. Matunda ya ushindi kwa CCM yaweza kupatikana. Penye nia,pana njia![/FONT][/COLOR]
[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Lakini kwa namna ilivyo sasa, CHADEMA waachwe 'watese'Arusha.[/FONT][/COLOR]
[B][COLOR=#222222][FONT=Verdana]Mzee Tupatupa (kwasasa Arusha) [/FONT][/COLOR][/B]
[B]Vuta Nikuvute [/B]CCm sikio la kufa