Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 478
- 1,025
Ukistaajabu ya Musa...Arusha Technical College ni kati ya vyuo Bora na vyenye sifa nzuri hasa kwenye swala la ufundi ndo maana serikali imeipa pia jukumu la kufundisha madereva na kutoa vyeti vinavyotambukilika na serikali.
Ili kuwezesha hili ATC inapaswa kusajiliwa katika mfumo unaounganisha chuo, TRA na police Ili kwa muhitimu anapomaliza chuo na kupata cheti chake inakuwa rahisi kufuatilia leseni yake kwakua taarifa za mwanafunzi pamoja na chuo tayari zinakuwa kwenye mfumo.
Matangazo yalikuwa wazi kuwa wanafunzi wa udereva wanapaswa kwenda VETA au NIT Ili kuhuisha leseni inayokidhi vigezo vya serikali.
Cha ajabu watu wameitikia wito, wameenda kujiunga na ATC wamesoma, wamepata vyeti ila unapoenda TRA au police unaambiwa chuo hakijasaliwa kwenye mfumo. Watu wamelipa pesa, wametumia muda lakini ghafla unaambiwa chuo hakitambuliki.
Je ni kweli kuwa Arusha Technical College (ATC) haitambuliki kama taasisi iliyopewa mamlaka ya kutoa mafunzo hayo?
Je kama ni kweli inahusika nani anapaswa kulaumiwa kwa kutokusajili chuo? Serikali au uongozi wa chuo wenyewe?
Kama ATC haihusiki katika utoaji wa mafunzo hayo, wanafunzi waliomaliza VETA (PSV pamoja na HGV) wafanyeje? Watarudishiwa pesa zao au ndo imekula upande wao?
Kama tatizo lipo upande wa chuo kutopeleka taarifa zinazosahili kwenye mamlaka husika je serikali inachukua hatua gani?
Serikali na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi wanafunzi au waathirika wa tatizo hili wanahitaji ufafanuzi na muongozo katika hili maana watu hawajui mwelekeo baada ya kuwa stranded kwenye kadhia hii.
Kwako mheshimiwa WAZIRI tunaomba majibu tafadhali.