Arusha: Taasisi ya Kiislamu ya Twarika yajitosa suala la Sensa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Mkoa wa Arusha imeandaa semina kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakazi wa jiji la Arusha juu ya kushiriki sensa ya makazi na watu inayotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa, Katibu mkuu wa Twarika Mkoa wa Arusha, Haruna Hussein ambaye pia ni msemaji mkuu wa Taasisi hiyo nchini, alisema semina hiyo inatarajia kufanyika kesho Januari 17, mwaka huu huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa naibu waziri wa madini, Dkt Steven Kiruswa ambaye tayari ameshatua Arusha kuongoza semina hiyo itakayofanyika katika ukumbi wa hotel ya Gorden Rose jijini hapa.

Sheikh Haruna alifafanua kuwa semina hiyo itawajumuisha pia viongozi wa Mila,(Laigwanani ), washiri na viongozi wa dini mbalimbali, lengo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kufanikisha zoezi zima la sensa ya makazi na watu.

Alisema Taasisi ya Twarika imekuwa mstari wa mbele kuona umuhimu wa Jambo hili ambalo linafaida kubwa katika uendeshaji wa serikali.

IMG_20220116_161211_501.jpg
IMG_20220116_161438_250.jpg


Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Mkoa wa Arusha imeandaa semina kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakazi wa jiji la Arusha juu ya kushiriki sensa ya makazi na watu inayotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu...
Nimekuja mbio mbio nikidhani wafuasi wa mood wanalianzisha kama kipindi kile cha sensa ya mwaka 2012:p
 
Back
Top Bottom