"Arusha sio Tanzania"

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,924
3,073
Salaam bandugu.
Naam kama mada inavyosema, hivi karibuni nilipata nafasi adhimu ya kwenda kutembelea makao makuu ya Jumuiya yetu tukufu na pendwa, Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ilikuwa ni ziara ya kikazi.

Mara tukawa tunaelezewa kuhusu kazi za sekretarieti ya Jumuiya, na hapo ndipo kauli tata ya "Arusha sio Tanzania" ilipotamkwa.

"Katika kazi zetu kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, hatuhesabu Arusha kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki au Federal Capital Territory.....kama Washington DC kule Marekani"

Hilo lilinifanya nitafakari ugumu wa kuanzishwa Jamhuri ya Shirikisho la Afrika Mashariki. Hivi ni watanzania wangapi watakubali Arusha imegwe na kuwa common territory ya EAC?
Below ni picha za jengo la EAC Arusha. Kuzuri hatari!

eac-building.jpg

Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki

DSC_0088.jpg

Mahakama ya Afrika Mashariki

Judges-of-the-Appellate-Division-during-session-with-court-clerks-in-front.jpg
 
Wewe huwa unahesabu A-city kama Tanzania, hujajiuliza mbona watu wa pale wapo kwenye level nyingine kwa kila kitu ikiwemo kujitambua kisiasa. Tanzania yote mngekua na hulka ya watu wa Arusha aisei tungekua tunasoma namba sisi majirani zenu.
Kawaida kama unaendesha gari na kuingia Arusha mtu huwa anahisi kama yupo Nairobi vile. Ukiangalia wanavyochangamka na kuchakarika.
 
Ni kweli kabisa Mkuu, sababu mojawapo ya maendeleo ya watu wa Arusha ni interaction na Kenyans pamoja na watu wa nje.

Watu wa Arusha hawana ulelemama na uswahili chovu.
 
Wewe huwa unahesabu A-city kama Tanzania, hujajiuliza mbona watu wa pale wapo kwenye level nyingine kwa kila kitu ikiwemo kujitambua kisiasa. Tanzania yote mngekua na hulka ya watu wa Arusha aisei tungekua tunasoma namba sisi majirani zenu.
Kawaida kama unaendesha gari na kuingia Arusha mtu huwa anahisi kama yupo Nairobi vile. Ukiangalia wanavyochangamka na kuchakarika.
nakubali hoja yako. nngekuwa na uwezo ningefanya mapinduz...arusha and moshi iko tofaut sana na wabongo wa huku pwani. nashaur mombasa ije tz na arusha na moshi tuipeleke kenya. cjui kwa nn kenyatta hakufight kipindi kileeee. afu pia wahaya hawajafanana na wazaramo kabisa..hivi obote na idd amini walizidiwaje ujanja na mwalimu? dah niutani tu modes usinipige ban. au ndugu unamawazo gan ww?
 
Back
Top Bottom