Arusha: Rais Magufuli azindua nyumba za Polisi, atanganza ajira 1,500 za Polisi, Polisi marufuku kufyeka bangi..

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,830


Rais John Magufuli akiwa jijini Arusha amezindua nyumba za Jeshi la Polisi na ametaka watu ambao waliounguliwa nyumba zao kesho wahamie wasije kuhamia maofisa na wao kuachwa.

Pia amesema maisha ya Polisi anayajua kwani ndiyo yaliyomtunzia mke kwani alikuwa mtoto wa askari Polisi.

Kwa sasa Rais Magufuli yuko uwanja wa Sheikh Amri Abeid akishuhudia umahiri na mazoezi ya Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu na opereshani zao mbalimbali. Fuatana nami kujua kinachijiri Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kwa upande wao polisi wameahidi unyang'anyi kwa kutumia pikipiki unaenda kuwa historia kwani wamejipanga na maonyesho yanafata ni ya kutuliza ghasia.



======​


wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha.

Sirro amesema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza.

Amefafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi.

Amesema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14.

“Hatuna muhali kuwachukulia hatua askari wanaokiuka utaratibu na nidhamu ya utendaji katika Jeshi la Polisi,” amesema IGP Sirro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli akiwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ameahidi kutoa BILIONI 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Maaskari wa vyeo vya chini.

“Mimi nimeoa kambini, mke wangu ni mtoto wa Askari Polisi, kwahiyo maisha ya askari wa chini nayatambua, leo nitatoa bilioni 10 ili zikasaidie kujenga nyumba za maaskari na hizi nyumba ziwe za maaskari wa chini”

Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho (Aprili 8, 2018) awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa hii leo.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo leo (Aprili 7, 2018) wakati alipokuwa anazungumza muda mchache alipomaliza kuzindua nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha na kusema anawapa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto, huku akiwapongeza wadau mbali mbali waliojitolea kwa mioyo yao katika ujenzi wa nyumba hizo.

“Nimepata mawazo ni kitu gani tunaweza kufanya kuhusina na matatizo ya nyumba za Polisi, sasa ninachoomba Mhe. IGP wale walionguliwa nyumba, kesho waingie katika nyumba zao hizi mpya ambazo zimemalizwa kujengwa. Kwasababu najua muda mwingine wanaweza wakachomekwa Polisi wengine halafu waliokuwemo wakaambiwa hapana”, amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Magufulia ameendelea kwa kusema “sasa nataka wale wale walionguliwa ndio waingie humo kwenye nyumba kwasababu Mungu aliwasaidia, moto ukaungua ungua kwa faida ya wao lakini hii inadhihirisha ni kwa namnagani makazi ya nyumba za polisi yalivyo kuwa mabovu”..

Rais John Magufuli ameagiza askari kuwakamata wazee, wanawake, vijana na watoto wa maeneo yanapobainika mashamba ya bangi akieleza kuwa wakikamatwa watasema ukweli na watazifyeka wenyewe.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati akizungumza na wakazi wa Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kuzindua kituo cha polisi na nyumba 31 za polisi.

“Sitaki Jeshi la Polisi litumike kufyeka bangi, kwa nini mkafyeke bangi? Tumieni intelijensia yenu mkakae pale kijijini na mtajua nani anakwenda kukagua mashamba hayo. Nyie shikeni wote katika hicho kijiji, kamateni wote, wazee, wanawake hata watoto shika, ndipo watasema ukweli,” amesema.

Rais amesema wanaolima bangi wakikamatwa ndio wanaotakiwa kuzifyeka.

RAIS Dk.John Magufuli ametangaza nafasi 1500 za ajira mpya kwa Jeshi la Polisi nchini huku akitoa maelekezo, anataka vijana wa JKT ndio wapewe nafasi hizo na si kutafuta ndugu,jamaa na marafiki wa makamanda wa wilaya na mikoa.
Amesema kuna tabia imejengeka pale inapotokea nafasi za ajira kwa ajili ya jeshi la polisi,baadhi ya makamanda wanatafuta watu wao na hivyo hata wakienda kwenye mafunzo wanapewa mafunzo kwa kuangalia waliowapeleka.

Rais Magufuli ametoa tangazo hilo wakati anazungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kuzindua nyumba npya za Polisi zilozojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wadau wa maendeleo wa mkoa huo.Ambapo ameagiza nyumba hizo wapewe askari wa vyeo vya chini.

Amesema kutokana na kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama hivyo ameamua kutoa ajira mpya 1500 na kufafanua anataka kuona wanaopata ajira hiyo ni watoto wa masikini na si vinginevyo.

"Nataka hizi nafasi ambazo nimezitangaza hapa leo hii zielekezwe kwa JKT ambazo waliamua kujitolea kupata mafunzo na kwa sehemu ni vijana ambazo hawana ndugu, kamanda wa Polisi,mkoa au kiongozi wa serikali." Bali ni vijana ambao wanatoka familia masikini.Hivyo niombe kipaumbele cha ajira hiyo kielekezwe kwa vijana waliopita JKT.Tabia ya kusikia wanaopewa nafasi ni ndugu wa wakubwa hapana,"amesema Rais Kikwete.

Pia amezungumzia namna ambavyo Jeshi la Polisi linafanya kazi vizuri ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akielezea wakati ameingia madarakani kuliibuka mauaji katika wilaya ya Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani.Amefafanua katika mauaji hayo watu 59 wamepoteza maisha na kati yao wamo askari 17 ambao wamepoteza maisha wakati wakilinda usalama wa wananchi wa maeneo hayo.

Dk.Magufuli amesema askari waliopoteza maisha Kibiti walikuwa na nia ya kuhakikisha nchi inakuwa salama na kimsingi ni Polisi ambao ni watoto wa watanzania masikini.Hivyo amesema hata hivyo polisi wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha mauaji hayo yanakoma na leo kuko salama na hata kama waliokuwa wanatekeleza mauaji hayo bado wapo Polisi wamejipanga na wanaendelea kuimairisha ulinzi.

=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 07 Aprili, 2018 ameungana na Watanzania wote kuadhimisha siku ya mmoja wa waasisi wa Taifa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi kwa kuzindua kituo cha polisi, kufungua nyumba 31 za askari polisi na kushuhudia maonesho ya Polisi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini la Arusha.

Kituo cha polisi cha watalii na wanadiplomasia kilichopo Naura, kituo cha polisi cha Muriet, na nyumba za 18 kati ya 31 za makazi ya polisi vimejengwa kwa mchango wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha na Benki ya CRDB kwa gharama ya Shilingi Milioni 753, wakati nyumba za polisi 13 zimejengwa na Serikali kwa gharama ya Shilingi Milioni 250.

Mhe. Rais Magufuli aliagiza kujengwa kwa nyumba hizo baada ya kutokea ajali ya moto iliyosababisha nyumba 13 za makazi ya askari polisi na mali zao kuungua moto tarehe 27 Septemba, 2017.

Katika kutekeleza agiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akaamua kuwashirikisha wafanyabiashara na benki ya CRDB kuchangia ujenzi huo na kufanikiwa kujenga nyumba nyingine 18 na vituo hivyo viwili vya polisi.

Pamoja na kuzindua miradi hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia maonesho ya Jeshi la Polisi ya kuzuia na kupambana na uhalifu yakiwemo kukabiliana na waandamanaji haramu, wezi, waporaji watumiao silaha na magaidi, yaliyofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid.

Akizungumza baada ya maonesho hayo Mhe. Rais Magufuli amesema Taifa litaendelea kumkumbuka Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa juhudi zake za kujenga nchi ikiwemo kuwajengea makazi wananchi masikini kule Zanzibar na ametoa wito kwa Watanzania kumuenzi kwa kudumisha amani na kuchapa kazi.

Pamoja na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo kwa jitihada zake za kuwaunganisha wadau na kisha kufanikiwa kujenga nyumba za askari na vituo vya polisi Mhe. Rais Magufuli ametoa Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi wa vyeo vya chini nchini, na amewaagiza viongozi wa mikoa yote kuwashirikisha wadau katika ujenzi huo kama ilivyofanyika mkoani Arusha ili kukabiliana na tatizo la askari kukosa nyumba za makazi.

“Askari polisi mnafanya kazi kubwa sana ya kulinda raia na mali zao, natambua juhudi kubwa mnazofanya na napenda kuwashukuru sana, naomba Watanzania wote tuendelee kuliunga mkono Jeshi la Polisi.

“Wakati naingia madarakani kulikuwa na mauaji kila wakati, kule Kibiti pekee yake waliuawa watu 59 wakiwemo askari polisi 17 na raia 42, Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa na sasa mauaji yale yamedhibitiwa, ni lazima tulipongeze jeshi letu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amekubali maombi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro la kuongezewa idadi ya askari na kupandishwa vyeo kwa maafisa wa polisi ambapo ameruhusu Jeshi la Polisi kuajiri askari wapya 1,500 kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kumpelekea mapendekezo ya maafisa wanaostahili kupandishwa vyeo.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza IGP Sirro kwa hatua ya kuwafukuza kazi askari polisi 458 waliokutwa na makosa ya kinidhamu na uadilifu kuanzia mwaka 2015 hadi sasa, na ametaka hatua hizo ziendelee kuchukuliwa dhidi ya askari wengine wanaokiuka maadili na taratibu za kazi ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi yakiwemo upokeaji rushwa na unyanyasaji raia kwa kuwabambikiza kesi.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amepiga marufuku askari, maafisa wa polisi na viongozi wengine wa Serikali kushiriki ufyekaji wa mashamba ya bangi na badala yake ametaka mashamba hayo yanapobainika yafyekwe na wanavijiji wenyewe waliohusika kuyalima.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wabunge na wananchi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Arusha

07 Aprili, 2018
 
Rais Magufuli ameshaingia uwanjani Sheikh Amri Abeid tayari kuwahutubia wananchi, karibu! Up date; Gwaride la jeshi la polisi limepita mbele ya Amiri Jeshi mkuu na kutoa heshima. Tukio linalofuata ni maonyesho ya kikosi cha kuzuia ujambazi kwa askari wanaotumia pikipiki. Vijana shupavu wa ffu wanaonyesha jinsi wanavyodhibiti uhalifu mitaani!
 
Back
Top Bottom