ARUSHA: Polisi wakamata tani 45 za sukari inayodaiwa kufichwa

Attachments

  • downloadfile-14.jpeg
    downloadfile-14.jpeg
    55.7 KB · Views: 65
Hahaha...huyo jamaa ni mmoja kati ya wafanyabiashara ambao huwa wanaitetea na kuisupport sana Chama Cha Majipu.

Nahisi sasa hichi chama kimegeuka "Mkia wa kondoo" unaojikaanga na mafuta yake yenyewe mpaka yanaishia jikoni.

Yeeeetu Macho na Masikio.
 
Hahaha...huyo jamaa ni mmoja kati ya wafanyabiashara ambao huwa wanaitetea na kuisupport sana Chama Cha Majipu.

Nahisi sasa hichi chama kimegeuka "Mkia wa kondoo" unaojikaanga na mafuta yake yenyewe mpaka yanaishia jikoni.

Yeeeetu Macho na Masikio.
Ashughulikiwe bila kujali hayo tunao umia ni sisi wananchi wa chini,tunachokitaka sisi wananchi ni sukari kupatikana madukani hayo sijui maccm macheda ma act na nengine mengi hayana msaada kwetu.
 
Polisi mkoani Arusha wamekamata tani 45 za sukari zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala la mfanyabiashara Karim Dakik.

Kamanda Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Mkuu naomba kufahamu tofauti ya kuficha na kuhifadhi , na naomba pia ijulikane ili kitu kifichwe kinapaswa kuhamishwa kutoka sehemu A kwenda sehemu B , sasa je hiyo sukari imetoka wapi hadi kukutwa kwenye hiyo godown ?
 
Wenye vichwa vya panzi wanatamani wanaokamatwa wawe makada wa UKAWA ili waseme rais anawaonea wapinzani!
Mwaka huu hamtapata hoja ya kujitetea!!
Nashangaa kila mwenye sukari akidakwa watu mnashadadia ni kada wa CCM, mnataka hao CCM wakihujumu uchumi wa nchi waachwe kwasababu ya u-CCM wao??
Ni akili gani hizi jamani??
 
KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA HUYO KARIM NI KADA MTIFU SANA WA CCM

Hapa ndipo ambapo huwa sielewi hoja za aina hii...suala hili halihusu vyama sasa inakuwaje mlete masuala ya CCM hapa? Lakini jambo jngine ni kuwa 'kada mtiifu' ina maana gani wakati kuna tani hizo za sukari zimepatikana kwa le go ambalo siyo zuri?
 
Ina maana walikuwa hawaju?Je,huko nyuma wafanyabiashara hawa walikuwa hawahifadhi sukari kwa kiwango hiki?Je,haiwezekani kuwa hili ni jambo la kawaida tu na ndio maana polis na watu wa usalama walikuwa hawawafuatulii?
Mkuu mimi leo nimemwambia mke wangu awagawie ndugu zake ule mfuko mmoja wa kilo 50 uliokuwa kwenye kijistoo changu , abakishe kilo 5 tu , kuna kila dalili wataanza kukamata hata mwenye kilo 10 tu , enzi za mwl nyerere kuna watu walikamatwa kwa kumiliki mche mmoja tu wa sabuni kisura au mbuni .
 
Nadhani sheria ya uhujumu uchumi imeweka vigezo kadhaa kwa mtu kushukiwa mhujumu uchumi. Kiwango cha chini cha mali inayokuwa imefichwa imetajwa ni yenye thamani inayozidi Sh. milion moja. Cha mhimu mfanyabiashara huyo awe ameificha, yaani hataki kuiuza wakati inahitajika sokoni au anaiuza kidogokidogo ili ipande bei au anaiuza kwa bei ya juu ya ile iliyoelekezwa na serikali.
 
Mkuu naomba kufahamu tofauti ya kuficha na kuhifadhi , na naomba pia ijulikane ili kitu kifichwe kinapaswa kuhamishwa kutoka sehemu A kwenda sehemu B , sasa je hiyo sukari imetoka wapi hadi kukutwa kwenye hiyo godown ?
Hapo ndipo kizungumkuti kipo. Kuhifadhi na kuficha. Ni lini unakuwa umeficha na ni lini unakuwa umehifadhi? Halafu tani 45 ni kiasi kidogo sana kwa mfanyabiashara mkubwa kuwa nacho.
 
Back
Top Bottom