Arusha ni Mfano Mzuri wa Uwezo wa Watanzania Kiuchumi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha ni Mfano Mzuri wa Uwezo wa Watanzania Kiuchumi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamundu, Oct 28, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi nimebahatika kuishi Arusha, Mwanza na Dar-es-salaam . Lakini nimekulia Arusha na naomba niweke hilo wazi.

  Arusha ni sehemu tofauti sana Tanzania kwa mawazo yangu na kuna mengi mazuri Arusha kwa nchi kuliko tunavyojua. Dar imeendelea zaidi lakini kuna serikali, Bandari, bahari n.k ambazo ni muhimu sana kwa nchi lakini naomba nieleze mazuri ya Arusha.

  1. Kutokuwa na Serikali: Kwasababu hakuna wafanyakazi wengi wa serikali kama Dar rushwa sio nyingi sana. Dar wafanyakazi wengi wa serikali wamakuwa wakitafuta pesa za rushwa kama biashara vile hivyo kila unachofanya kuanzia kupima viwanja mpaka kuweka maji inakuwa kama ni vigumu lakini ni kwasababu ya serikali kuwa kwenye kila kitu (Too much regulations). Hii imesaidia kupunguza gharama za biashara
  2. Jasirimali: Nenda Arusha leo uangalie Majengo ya Mjini ni nani anayamiliki si serikali wala NSSF bali ni Watanzania wa kawaida wafanya biashara. Hii inatokana na ukweli kwamba kwasababu hakuna serikali watu wengi wakikua hata mimi binafsi nilikuwa sitegemei kufanya kazi serikalini kwasababu hizo kazi hazipo na kama zipo mwajiri yupo Dar na siyo Arusha. Vilevile kuna mwamko kwamba huhitaji kutegemea mtu unaweza kufanya mwenyewe ukiwa Arusha. Vijana wengi wameanzisha vi kampuni vya kuetembeza wageni, kukata ticket, kuuza vitu vya sanaa, kuuza madini na kukata madini. Kwa ujumla serikali kutokuwepo Arusha ni kitu kizuri na sio kitu kibaya kwa wafanyabiashara kwani Dar ukisha pandisha ghorofa TRA wanaona deal.
  3. Serikali: Serikali ni tatizo mfano serikali ilichukua viwanja vya madini ya Tanzanite na kuwapa wawekezaji hivyo serikali inachopata hatukioni ni bora ingewaachia wananchi tungeona maghorofa zaidi mijini, shule za binafsi, na biashara nyingi za wazawa badala ya sasa wameua soko la Tanzanite, hakuna ushindani kama zamani na gharama za biashara zimeenda juu. Kwa ujumla serikali yetu ni tatizo kwa nchi ni bora wangewaachia wananchi wajenge nchi yao.
  4. Mashamba: Wakati tumeanza kuona sehemu chache nchini zimeanza kilimo cha kisasa Arusha wameanza kilimo cha kisasa sikunyingi sana kuanzia mashamba ya kahawa, maua, miwa, karanga na ngano. Wakina Mzee Mtei wa chadema na Mzee wa Prec Air wamepata utajiri kwenye kilimo. Sasa tuangalie sehemu nyingine za nchi serikali ndiyo inataka isaini mikataba ya Kilimo kuanzia Kigoma, Morogoro, na Kagera wakati hayo mashamba Watanzania wenyewe wangeweza kuingia mikataba moja kwa moja na wawekezaji au hata wakafanya wenyewe. Kama unataka kujua kuna watanzania wanaweza kulima kisasa bila mikataba ya serikali basi nenda Arusha. Tatizo kubwa la serikali na hawa wawekezaji ni kwamba si wenyeji na hawata wekeza pale. Serikali ina viongozi wanaotafuta 10% na wawekezaji wanatafuta materials wapeleke nje. Na hii ni tatizo kubwa kwenye madini pia.
  Mwanza ineweka ikawa zaidi ya Arusha lakini bahati mbaya ndugu zetu kule walisahaulika kwenye miundo minu kwa muda na serikali imeingia kwa kasi sana kwenye maisha yao hasa madini na samaki.

  Mimi kwa mawazo yangu Arusha ilikuwa inaenda vizuri na ni mfano mzuri wa serikali kuwa ndogo na kuwaachia wananchi walete maendeleo yao wenyewe. Watanzania wanajipenda na wanapenda maendeleo na kitu kikubwa ni kwamba serikali iko sana kwenye maisha yao. Serikali ya Tanzania inatakiwa kutoa huduma muhimu na biashara iachie wananchi wenyewe wafanye. Huwezi kuzuia watu wa Mwanza kufanya biashara ya uvuvi halafu ukategemea kuendeleza Mwanza, huwezi kunyanganya watu wa Arusha Tanzanite na tukategemea maendeleo, hatuwezi kunyanganya watu washamba na tukategemea maendeleo. Kuna vitu kama Kuchimba mafuta na gas ambavyo vinahitaji kampuni kubwa lakini vitu ambavyo wananchi wanaweza kufanya serikali inabidi iondoke na kuwaachia wananchi. Kwani serikali ijiingize kwenye mikataba ya mashamba!
   
 2. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Halafu Arusha kila mtu mtemi na mbabe, kuomba msamaha ni kama kumtusi mtu! Napenda kutembelea Arusha lakini sio kuishi.
   
 3. m

  massai JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  arachuga hakun wa kudanganywa kwa kanga 'tshirt au pilau.hivyo vitu huko arachuga watu walisha jitosheleza.labda waende pwani na kwa waswahili wa darisalama kwanza wengi wao ni brainwashed ndio maana unakuta dar imejaa watu wasio wenyeji wakimiliki uchumi wakati wanaojiita wenyeji wao ni kupiga domo na kupumzika kwingi.mbezi imejaa wachaga ,maduka kariakoo yote yawachaga majumba yote mazuri wachaga na wengine wasio waswahili.waswahili ni mtaji wa magamba kwani bado wapo usingizini hawajui dunia imebadilika wao wamebaki kuishi kwa hofu na kudanganywa na magamba.mtabaki kulalama chadema tunasonga mbele.
   
 4. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Huwa tunabadilishana mitaji tu huku kwetu maisha ya huku tunayajua wenyewe japo wageni wakija wanayaona magumu
   
 5. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Maisha ya Dar magumu kwako tu,huku Dar kunaitwa MTAKUJA.
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Maneno mengi yasiyo na sababu. Ungefupisha habari yako ingeeleweka vizuri maana mengi ya yale yaliyomo humu ni porojo.
   
 7. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  tumekusoma. lakini kwa rushwa mbona hapa ndo penyewe?
   
 8. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  mbona na ww ndio umeongeza utumbo wako shenzi
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Kuna ukweli fulani,ingawa pia deal za watu wa kipande ile nazo ni ndefu ndefu. Wale wezi na majambazi wengi wa magari na hela za wenzao je?
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha
  Wengi hawafahamu kuwa hapa bongo tunaishi kwa miundo mbinu tu, kulala njaa ni kupenda kwako.
   
 11. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kwa ujumla nachotaka kusema hapa ni kwamba

  1. Serikali isijiingize kwenye kila biashara na maisha ya watu kama ubinafishaji wa mashamba
  2. Serikali ni tatizo hasa kwenye rushwa. Watanzania wangekuwa bora kama serikali ingefanya vitu muhimu na kuacha biashara zifanye biashara.
   
 12. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kumbe wenye chama chenu SUBCONCIOUSLY muna admit kuwa ni chama cha Wachagga. Sasa mbona mnamshambulia NAPE wa watu akiyarudia maneno yaleyale ambayo wenyewe mnayaamini vichwani mwenu.

  Kwa mwendo huu huko mbele sijui itakua ni Tanzania ya aina gani? Kila la heri kwa kujiona CHADEMA ni cha WACHAGGA, wengine wanavamia.
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  halafu haujapangika kimji kabisa asilimia 90 ni makazi.duni
   
 14. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  asante kwa kutufumbua macho kuhusu chadema
   
 15. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni hoja nzuri KAMUNDU,
  Ili jambo pia lipo Mbeya kama umewahi kufika au kuishi,
  Wananchi wanapambana wenyewe kuwekeza na kilimo,
  Tatizo ni pale Serikali inapotia mkono, ni balaaa
  Nakuunga mkono
   
 16. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nafikiri kabla ya kufanya uchambuzi wa hii hoja inabidi kwanza uji-update na nini au Arusha kiuchumi inasimama wapi ukitilia maanani sehemu muhimu za north circuit tourist attraction Kilimanjaro, Serengeti, etc. je mapato yanayotokana na hizo attraction nani anafaidi kwa njia gani nk. then unaweza kuja na good conclusion .... ..... ..... I was here.
   
 17. h

  hubby Member

  #17
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona ume quote porojo zote hizo? nawew hujioni......
   
 18. d

  davestro Senior Member

  #18
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kila shilingi 100 ya pato la taifa,Dar ina 97,Mwanza kwa ajili ya migodi na samaki ina sh.2 na Arusha kwa ajili ya utalii na ile bloodtanzanite ina sh.1.,source BOT
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu Davestro
  Kama waamini hizo takwimu za kutoka BOT me sikuhungi mkono kabusa hizo takwimu jnazitilia shaka kabisa 100%

  Ina maana nchi hii mikoa mingine haichangii pato au serikali ina kula mapato ya mikoa hiyo mingine kama mwanza ni migodi (Shinyanga,Tabora,Mara,Kagera, mikoa tajwa ina migodi ya dhahabu na mmoja una Almasi) inamaana wao pato lao la kimkoa lina enda wapi halipo katika shiling 100? au hiyo shilingi 100 ya pato la taifa lina pigiwa vipi hiyo hesabu? ina husika na idadi ya wakazi wa mkoa husika au?

  Katika hili me sikubaliani na hizo takwimu fake zinazo wapotosha watanzania na ndio maana viongozi walipo madarakani wana dumaaa kia fikra badala ya kuwa proactive kifikra katika kukuza maendeleo ya mikoa mingine na kufanya Dar kuwa vamizi la vijani wengi kutoka mikoani yet Dar ina infrastructure duni kukidhi idadi ya wahamiaji.

  My Take;

  Takwimu nyingi za serikali yetu zinanipa shaka kubwa sana kuwa watanzania hatupewi ukweli jinsi uchumi wetu unakuwa vipi na unapoleomoka vipi kwa sababu zipi halii hiii ya kukua na kushuka inatokeaje.

  Bali viongozi wetu wenye nyadhifa za kitendaji katika sector hizo muhimu husika kama BOT, Hazina wanatupa fake takwimu kabisa leo hii ukiwauliza kwanini Shilling inashuka zidi ya USA Dollar Hawana jibu na natural resource tulizo nazo zote hizo na elimu ya wachumi tulio nao hakuna jibu lielewekalo kwanini shilling inazidi kudidimia kila leo?

  Uchumi wa nchi kukua sio tu kuangalia takwimu za Hazina na BOT bali pia kujua je pato la mtania lina kidhi haja ya kila myu hata mwenye kipato cha chini then hapo tutajua uchumi una kuwa lakini kwa hali hii kila bidhaa iko juuu matumizi ya kila aina yako juu mtu anakuja anasema ati uchumi unakuwa its outrageous
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mikoa mingine vipi?
   
Loading...