ARUSHA: Mwenyekiti wa mtaa FFU ajiuzulu na kuhamia CCM

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa FFU kata ya Muriet jijini ndugu Anacletus Edward Arusha ameamua kuachia uwenyekiti na kujivua uanachama wa CHADEMA na kuhamia CCM.

Huu ni muendelezo wa viongozi wa CHADEMA kuachana na Chama hicho na kuamua kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, kusimamia maendeleo na Rasilimali za nchi huku CHADEMA ikionekana kukinzana na kila jambo jema kwa maslahi ya nchi.

Tetesi kutoka Arusha zinaeleza kuwa bado kunatarajiwa wimbi kubwa la viongozi wa CHADEMA kuachia ngazi.
Mimi kwakweli nashindwa kuelewa inamaana kiongozi kama umekubali utendaji mzuri wa serikali ni mpaka ujiuzulu wadhifa uuliopewa na wananchi kwa kukupigia kura? Kama umefurahishwa na utendaji mazuri wa raisi muda huu siindiyo mazuri wa kuwa begakwa bega na raisi ili umuunge mkono utekeleze Yale mazuri ya raisi anayofanya ukiwa na wadhifa huo,je ukijiuzulu utamoneshaje raisi unamuunga mkono?je wengine mmbona wao wanawatumikia wananchi bila kujiuzuluu?sijajuwa madhumuni ya huo mtindo wa kiongozi kujiuzulu kwa kigezo cha kumuunga mkono raisi wangejiuzulu kwa utendaji mbovu hapo ningeelewa
 
Nasubiri kwa hamu kubwa sana uchaguzi wa marudio ili ccm wapate aibu ya miaka mingine mitano.angaikeni na matatizo ya wananchi,kununua viongozi sio suluhisho la nyie kukataliwa arusha.sisi waafrika tumelogwa na nani,unanunua kura moja badala ya kuangaika na matatizo ya walio wengi.ccm mtapata aibu sana Kama mtafanya uchaguzi mwingine.

Sent from my itel it1505 using JamiiForums mobile app
Kilio chako kiwasilishe kwa mwenyekiti wako wa chadema mkoa..
 
Ili kumsaidia JPM.hautakiwi kujiuzulu bali kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Hawa wote wanaojiuzulu wamefika bei yao

Hilo neno! Pia nadhani hakuna ubishi kuwa graph ya dau la malipo kati ya watoaji na wapokeaji inashuka gradually! watoaji nao wanaisoma namba kimtindo.
 
Hii ni anaesthesia kwa CCM ili waone kuwa CHADEMA inakufa Arusha. Nawashauri CCM mwaka 2020 walale wasipige kampeni wakihisi CHADEMA imekufa
 
INAELEKEA WEWE UNA MAHUSIANO YA KINASABA NA NDUGAI . . , UNATUMIA "RUNGU" KUFIKIRI NA KUPOTOSHA WATU . . !

Huwezi kuendelea kuwa kwenye chama kinachopinga hata bajeti za maendeleo kwa wananchi.

1. Siku bajeti inapitishwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni hakuwepo bila kuwa na sababu ya msingi.

JIBU: SABABU ZA MSINGI ZILIKUWEPO NA NDIO MAANA HAKUWEPO . .

2. Wakati wa utekelezaji wa bajeti ataanza kuja na maswali yasiyo na tija.
JIBU: WAJIBU WA BUNGE NI KUISIMAMIA SERIKALI, KUIHOJI SERIKALI INAPOTENDA KINYUME NA SERA, BAJETI AU KATIBA . . WABUNGE WA CHAMA PINZANI TUU NDIO WANAOTEKELEZA WAJIBU HUU SAWASAWA KULIKO WABUNGE WA CCM . .


3. Watanzania walilalamikia sana ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma...Rais anachukua hatua Viongozi wa Chadema wanapinga.

JIBU: CHADEMA WANALALAMIKA NAMNA JPM ANAVYOSHUGHULIKIA MAFISADI KWA KUTOFUATA SHERIA NA KWA UPENDELEO . . TAZAMA SAKATA LA ESCROW, WEZI HALISI AMBAO NDIO WALIOPANGA NA KURUHUSU PESA ZILIPWE KWA RUGE NI RAISI MSTAAFU NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI, LAKINI WAO WAKO HURU, NA MTU MFANYABIASHARA HALALI KATUPWA NDANI . . HUU NI UONEVU . . !

Watanzania walililalamikia sana umungu mtu wa wafanyakazi serikalini na akaahidi kuwashughulikia na akaanza kuwashughulikia Chadema wakapinga.

Watanzania walilalamikia sana madini kutoroshwa na kutuachia mashimo...Rais anachukua hatua viongozi wa chadema wanapinga.

Watanzania walilalamikia hali mbaya ya barabara,usafiri wa reli na uzima wa shirika la ndege...Rais amechukua hatua chadema wanapinga.ndege zinanunuliwa watu hawataki.
JIBU: SUBIRI RELI IJENGWE KWANZA, NA TRENI ZIFANYE KAZI NDIO UTOE SIFA . . NDEGE ZIMENUNULIWA BILA KUFUATA TARATIBU HALALI ZA SERIKALI ZA MANUNUZI . .

Watanzania walililalamikia kuhusu ada ya elimu ya msingi kuwa kikwazo ...Rais amechukua hatua chadema wanabeza.

Watanzania walilalamikia tatizo la ukosefu wa mahindi na njaa ...Serikali ikisimamisha uuzaji wa mahindi nje Chadema inapinga.

Watanzania walihitaji ajira kupitia viwanda...Viwanda vinaanza kufufuliwa chadema wanabeza.

JIBU: VIWANDA VILIKUWEPO VINGI TUU, NYERERE ALIFANYA KAZI NZURI SANA. WALIOUZA, WALIOVIUA VIWANDA VYETU KWA BEI YA BURE NI MARAISI WALIOPITA WA CCM NA MAKADA WA CCM, WENGI BADO WAPO HAI . .
KWA SASA CCM WANAIKABIDHI NCHI HII KWA WAGENI (WACHINA) TENA, KWA KISINGIZIO CHA UWEKEZAJI NA VIWANDA . .

Wananchi walilalamikia sana kuhusu baadhi ya watu kuhodhi ardhi bila kuziendeleza...Rais anachukua hatua chadema inasema matajiri wanahujumiwa.

Wananchi waliongelea sana kuhusu ukwepaji kodi kwa wafanyabiashara wakubwa ...hatua zimechukuliwa chadema inasema wafanyabiashara wananyanyaswa.

Wananchi walihitaji maji kwa muda mrefu..utashangaa maji yakisambazwa viongozi wa chadema wanaebeza propaganda eti yana chumvi.

MAJI BADO NI TATIZO KUBWA KILA KONA YA NCHI HII INAYOTAWALIWA KWA MKONO WA CHUMA NA CCM ZAIDI YA MIAKA 40 . .


Mbaya zaidi mwenyekiti wa chadema ni mwenyekiti wa kudumu hivyo hatoi fursa ya mawazo mapya na mbadala kwa anaowaongoza.

Kwa muktadha huu utaelewa kwa nini viongozi hawa wa chadema wanaamua kuachia ngazi.
Wanaamua kuwa wazalendo na kuweka maslahi ya Taifa mbele.



Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Njaa na siyo uzalendo na kampeni za chini chini za mkuu wa Mkoa za kuwapa chochote weak solders ili ku surrender ndio mbinu inayotumika. Wote wanaoondoka ni wale weak ili wabaki wale strong for the next Battle kwani principle ya vita ni kutumia strong solders kama ilivyo katika kitabu cha Joshua.
 
Nawaza kwa sauti, kama Chadema wanasema madiwani wao wananunulika. Je? kumbe wanachama wa chadema wana bei? kama wana bei ingekuwaje wangepewa nchi? sio ndio wangetuuza kwa wazungu? Najiuliza sipati jibu, unanunuliwaje sasa kwanini isiwe kipindi cha uchaguzi.? Utetezi mwingine wa hovyo kabisa, na Chadema wasipobadilika mpaka 2020 chama kitabaki historia kama NCCR mageuzi. Tuliwaeleza wakati wa kubadili gia angani mkatuita buku saba n.k.
 
" if there is no movement, no progress , no growth..."
mara chache sana mtu kupanda treni au bus ambayo haiendi, na hata ikienda haijulikani itaelekea wapi na wakati gani.

chadema mjitafakari. siasa sio maandamano,kupinga kila kitu,mawazo mapya kuyaita usaliti, opreations na matamko.
Watanzania wamehamia kwenye mode ya maendeleo kwa vitendo.Mbadilike ili muwe bora zaidi vinginevyo mtapotea milele.
Mbona ccm wanapongeza kila kitu? Acha upinzani pia ukatae kila kitu.

Sent from my SM-G530H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom