ARUSHA: Mwenyekiti wa mtaa FFU ajiuzulu na kuhamia CCM

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa FFU kata ya Muriet jijini ndugu Anacletus Edward Arusha ameamua kuachia uwenyekiti na kujivua uanachama wa CHADEMA na kuhamia CCM.

Huu ni muendelezo wa viongozi wa CHADEMA kuachana na Chama hicho na kuamua kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, kusimamia maendeleo na Rasilimali za nchi huku CHADEMA ikionekana kukinzana na kila jambo jema kwa maslahi ya nchi.

Tetesi kutoka Arusha zinaeleza kuwa bado kunatarajiwa wimbi kubwa la viongozi wa CHADEMA kuachia ngazi.
 
Chezea kufika bei weee.. na hali ilivyo tight tena, hata kwa buku tano mtu anahama tu wakiongozwa na baba lao Propesa pumba.
Baada ya kuwatosa ndio mnasema wamefika bei...kwa hiyo na lowassa mlimpa sh ngapi?
 
" if there is no movement, no progress , no growth..."
mara chache sana mtu kupanda treni au bus ambayo haiendi, na hata ikienda haijulikani itaelekea wapi na wakati gani.

chadema mjitafakari. siasa sio maandamano,kupinga kila kitu,mawazo mapya kuyaita usaliti, opreations na matamko.
Watanzania wamehamia kwenye mode ya maendeleo kwa vitendo.Mbadilike ili muwe bora zaidi vinginevyo mtapotea milele.
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa FFU kata ya Muriet jijini ndugu Anacletus Edward Arusha ameamua kuachia uwenyekiti na kujivua uanachama wa CHADEMA na kuhamia CCM.

Huu ni muendelezo wa viongozi wa CHADEMA kuachana na Chama hicho na kuamua kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, kusimamia maendeleo na Rasilimali za nchi huku CHADEMA ikionekana kukinzana na kila jambo jema kwa maslahi ya nchi.

Tetesi kutoka Arusha zinaeleza kuwa bado kunatarajiwa wimbi kubwa la viongozi wa CHADEMA kuachia ngazi.

Ili kumsaidia JPM.hautakiwi kujiuzulu bali kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Hawa wote wanaojiuzulu wamefika bei yao
 
Maendeleo yapi?Yakurudisha pesa za Escrow au za kurudisha pesa za Kivuko kibovu?
Barabara
Maji
Elimu n.k

Kurudishwa kwa fedha ni matokeo ya Serikali ya Magufuli ya kupambana na mafisadi.
 
Back
Top Bottom