Arusha, Muleba waikimbia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha, Muleba waikimbia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, May 18, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  KIMBUNGA cha ‘Operesheni Vua Gamba, Vaa Gwanda’ ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezidi kutikisa kote nchini, baada ya kumzoa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha Mjini, Emmanuel Temba.

  Temba ambaye pia amewahi kuwa diwani wa Kata ya Kimandolu, alikuwa miongoni mwa Wana CCM 400 wa Kijiji cha Enduleni, akiwamo Mwenyekiti wao, Pettey Kitaika, waliohamia CHADEMA na kukabidhiwa kadi jana na Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Amani Golugwa.

  Wakati mwenyekiti huyo wa kijiji, Kitaika, akisema ataeleza sababu za yeye kujitoa ndani ya chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kwenye mkutano mkubwa utakaofanyika kijijini hapo, utakaowashirikisha viongozi wa CHADEMA mkoa, Temba yeye alisema viongozi wa CCM hawashauriki na wameacha misingi ya kuanzishwa kwa chama hicho, kwa sasa wanajilimbikizia mali na familia zao.

  Alisema kuwa kuna wanachama wengi wa CCM kutoka vijiji vya jirani ambao nao wanatarajia kujiunga na CHADEMA siku hiyo ya mkutano ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa kutoka CHADEMA.

  Temba alisema kuwa amevutiwa na operesheni hiyo ya ‘Vua Gamba, Vaa Gwanda’ ambayo imekuwa ikiwahamasisha wananchi kujua haki zao na kuikataa CCM.

  Alisema kuwa viongozi wa CCM wamesahau kuwatumikia wananchi ambao kila kukicha maisha yao yanazidi kuwa magumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kunakosababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa.

  “CCM hawashauriki, mimi nilikuwa nikiongea kwenye vikao lakini hakuna anayesikiliza, nimeamua kuja huku (CHADEMA) ili niweze kuongea kwa sauti, sina nia ya kugombea uongozi wowote, nitashirikiana na wanachama wenzangu kuendeleza ‘Operesheni Vua Gamba, Vaa Gwanda’” alisema Temba.

  Naye Mwana CCM mwingine, Lucas Eliahu, ambaye alitangaza rasmi kukihama chama hicho alisema kuwa amechoka kudanganywa kila siku maisha bora kwa kila Mtanzania huku maisha yanazidi kuwa magumu.

  “Nimechoka hata nikifa acha nifie CHADEMA, ni bora kufia kwenye haki niweze kupumzika kwa amani kuliko kuendelea kukaa CCM ambayo haiwajali na inawakandamiza wananchi walio maskini kwa kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao,” alisema Eliahu.

  Kwa Prof. Tibaijuka hoi

  Huko Bukoba, CHADEMA kimeendeleza wimbi hilo baada ya kuvuna wanachama wapya 112 katika Jimbo la Muleba Kusini ambalo mbunge wake ni Prof. Anna Tibaijuka.

  Wanachama hao walipokewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Msalaba Mwekundu mjini Muleba juzi jioni, ambapo pia ulifanyika ufunguzi wa ofisi ya chama ya jimbo, na kufuatiwa na mkutano wa hadhara ulioongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Kagera, Wilfred Lwakatare.

  Wengine waliohudhuria mkutano huo uliofurika mamia na wananchi ni Mbunge wa Viti Maalumu, Conchesta Rwamulaza (CHADEMA), Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake mkoa (Bawacha), Anna Mukono na madiwani mbalimbali kutoka vyama vingine vya upinzani wilayani humo.

  Katika idadi hiyo ya wanachama waliojiunga na chama hicho, 45 walirudisha kadi kutoka vyama vingine vya siasa na 67 ni wapya. Hao ni 21 kutoka CCM, 11 wa TLP, 7 wa CUF na 6 kutoka NCCR - Mageuzi.

  Source Tanzania Daima la Jana
   
 2. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  M4C, haina huruma!
   
Loading...