Arusha: Monaban Kuvunja Chungu kwa waliokula unga

Arusha: Monaban Kuvunja Chungu kwa waliokula unga

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Mgombea wa Ubunge aliyeshindwa vibaya Arusha OlaIs Mollel (Monobangi) ametoa vioja na kusema magari ya polisi yamewafanya wananchi wasijitokeze kwenye uchaguzi wa mbunge uliofanyika jumapili iliyopita, akuishia hapo ameendelea kusema kwa wale wote aliyowapo unga wa kupikia ugali na ambao hawajampa kura anategemea kuvunja chungu siku za karibuni.
 
Sasa kuhusu magari ya polisi anamlaumu nani, amlaumu mzee wa ndovu aliemkimbia usiku kwa usiku
 
Duu!
Naona sasa mnanza kumfanya dingi wa watu aonekane kawa comedian.
Mshampiga chini kwa aibu, mwacheni auguze maumivu.
 
Kweli nimeamini, La kuvunda halina ubani. CCM kwa Arusha mmechacha ile mbaya. Monabangi angelisikia ushauri angejikalia na vijisenti vyake. Ila naamini hiyo ya unga, alilipwa na mzee wa ndovu na kipara. Hawakukesha bure Arusha. Anayasema hayo ili kuwafanya Taakukuu wasiwafuatilie. Tunajua haswa mzee wa Kipara haendagi bure mahali. Tangu atuite Malofa haachi pochi. Huzimwaga kwa kumwaga.
Kuhusu magari ya Polisi, yalitolewa kwa nia njema tu. Lema angempita kwa kura laki tatu 300.000 na hii ingempa BP bure. Akubali hata hiyo 60.000. Nalo ni pigo
 
Kweli huyo ndie aliyekuwa anautaka Ubunge wa Arusha mjini!!!!!!!!!! bado yuko kwenye zama za kuvunja chungu!!!!!!! kweli ccm mbele kwa mbele............
 
bora avunje drum, huemda ikawa na afadhali
 
Kula CCM Kura CDM.
Btw unga wa magunzi wamekula sana watu wa ungaltd, sombetini, murieti, kwa mromboo n.k

Avunje tu hiyo chungu ili magunzi yarudi kwake coz tumechoka
 
Kula CCM Kura CDM.
Btw unga wa magunzi wamekula sana watu wa ungaltd, sombetini, murieti, kwa mromboo n.k

Avunje tu hiyo chungu ili magunzi yarudi kwake coz tumechoka

Sombetin sio wote ni kamtaaa kamoja tu akivunja chungu watapuputika wote mtaaa utabaki haina watu
 
Mwambie Jamani Asivunje Chungu.Uchaguzi unaofuata hakutakuwa na watu huku.Aache Khasira jamani.Baada ya uchaguzi kuna Maisha jamani.Aah.
 
mwambien avunje safuria kabisa chungu chepesi.wana arusha hatudanganywi na unga kama ameweza kutoa unga na kumwaga hela hizo fedha angeenda kuzirudishaje?huko bungeni angefanya nini?arusha ccm nevery
 
Chungu hakitafanya kazi kwa sababu unga wenyewe ulikuwa wa magunzi sio mahindi! Mwenyewe Kakiuka miiko ya kuvunja chungu, hatutishiwi nyau!

Mgombea wa Ubunge aliyeshindwa vibaya Arusha OlaIs Mollel (Monobangi) ametoa vioja na kusema magari ya polisi yamewafanya wananchi wasijitokeze kwenye uchaguzi wa mbunge uliofanyika jumapili iliyopita, akuishia hapo ameendelea kusema kwa wale wote aliyowapo unga wa kupikia ugali na ambao hawajampa kura anategemea kuvunja chungu siku za karibuni.
 
Nani amchague kama alikuwa anatoa unga wa magunzi tena bila mboga!
 
Back
Top Bottom