Arusha ,mji ulionifanya kukosa amani.

nina miaka mingi sana hapa arusha sijawahi kukutana wala kuona tukio la namna hiyo ni jambo geni kabisa na bado najiuliza kwa nini itokee kwako?!!...watu wa arusha wana utu sana na ni tofauti mno na maelezo yako labda kama ingekuwa maeneo ya ngaleloo,majengo au matejoo labda kidogo huko kuna matukio lakini si kama hilo
 
Niseme uongo ili iweje? Na wote kati ya waliojibu siwajui sasa niwadanganye ili nipate faida ipi hasa ?
....sasa hujanijibu maswali yangu,unaniuliza ya kwako tena?
..basi nijibu hili:ulipoulizwa unapokaa ukazidi kusema uongo mana huwa hupendi KUJIVUA NGUO kwa mtu usiemjua,si ndio?
..chukua soda take away wakati ukinijibu!
 
nina miaka mingi sana hapa arusha sijawahi kukutana wala kuona tukio la namna hiyo ni jambo geni kabisa na bado najiuliza kwa nini itokee kwako?!!...watu wa arusha wana utu sana na ni tofauti mno na maelezo yako labda kama ingekuwa maeneo ya ngaleloo,majengo au matejoo labda kidogo huko kuna matukio lakini si kama hilo
Kiukweli limeniacha na maswali mengi sana hadi sasa na sielewi nini dhima ya yule mtu.
 
....sasa hujanijibu maswali yangu,unaniuliza ya kwako tena?
..basi nijibu hili:ulipoulizwa unapokaa ukazidi kusema uongo mana huwa hupendi KUJIVUA NGUO kwa mtu usiemjua,si ndio?
..chukua soda take away wakati ukinijibu!
Poa usjali,asante kwa kushiriki
 
nina miaka mingi sana hapa arusha sijawahi kukutana wala kuona tukio la namna hiyo ni jambo geni kabisa na bado najiuliza kwa nini itokee kwako?!!...watu wa arusha wana utu sana na ni tofauti mno na maelezo yako labda kama ingekuwa maeneo ya ngaleloo,majengo au matejoo labda kidogo huko kuna matukio lakini si kama hilo
Kwa maelezo ya hapo juu, tayari huyu mtu inaonekana Ni Giant, Ni mtu wa kazi Ana mvuto wa aina yake kila idara kwa mana hiyo Ni kwamba anaweza tumika kufanya lolote
 
Uzi huu ungekamilika kama walau nawe muhanga ungetoa picha ya unadhani nini kilitaka kukutokea baadae iwapo ungefuata matakwa yao,naandika hivi sababu we umeeleza tu aliekuhoji kuwa ni wazi waonekana unatokea kaskazini ila we hujatueleza yule uliyekuwa unastorika nae yukoje mrembo au anatisha na Ile kampani yake uliiona maana mpaka wakakupiga picha wakoje,wako kama wabana pua au wamekaa kishari shari maana kama we mtoto WA mjini ukimuona mtu tu unaanza mtolea mitazamo tofauti kama amekaa kiteja utaweka simu yako mbali,mbabe ka Scorpion utajua hapa soon hapatatosha kana anabana pua kama hawa wanaotuburudisha kwenye luninga utahisi hapa Kuna kitu wanataka nipewe ambacho ni kigumu kumuomba mwanaume mwenzio na wangekuwa na sura ya kondoo ungejua wanataka kukushauri ujiunge labda na fellowship yao.
Sasa tatizo mdau hujatupa walau kidogo taswira ya hao watu unatupa wakati mgumu kutaka kukutolea ufafanuzi ukifikiria kwamba we ndio uliowaona,ongea nao na ukawatoroka, hebu rudi tena ujazie Nyama maana Kuna vitu hujaviweka sawa.......

....,
 
Mambo ya kawaida tu hayo Mombasa kuhudumiwa.

Ulishindwa kutuma sense ya 6 mbali na 5 ulizopewa na Mungu
 
Kiukweli hakuna jiji ambalo naliogopa Tz .siwezagi kukaa zaidi ya siku2!kama kuna shughuli ya zaidi ya siku2 basi nibora nikalale Moshi. Ule mji unatembea roho mkononi presha juu mda wote. Kila kona si salama
 
Nimekumbuka sana mji wa Arusha ambao kiukweli ulikuwa mji mzuri na wenye hali nzuri ya hewa ila gharama za maisha zilikuwa juu sana (nadhani sababu kuu ni utalii)

Nikiuzungumzia mji huu sitoacha kukumbuka tukio hili ambalo liliniacha na maswali mengi,Mnamo mwezi june mwaka 2015 wakati nikiwa chuoni katika mji wa Arusha nilikuwa naenda kwenye bar moja "kilimanjaro bar" ipo mkabala na city link.

Siku hiyo nilifika hapo kuangalia mechi na katika bar ile ulikuwa ukinunua kinywaji na kuangalia mtanange wako bila wasiwasi.

Wakati naingia kwenye hiyo bar mimi na mwenzangu moja kwa moja hadi kaunta nikatoa wallet nikanunua take away Mbili (soda),Ila wakati nipo kaunta pembeni yangu alikuwepo ndugu mmoja anaweza kuwa na umri kati ya miaka 35-45 alinisalimia "vipi kaka" nikamjibu nikachukua soda zangu mbili,moja yangu na nyingine ya mwenzangu ile nataka kuondoka akaniita akamwambia mhudumu mmoja kuwa "huyo kaka mpe pombe nitalipia mimi" nikamwambia "situmii kilevi chochote"

Akaonekana kutahamaki ila akasema nile chochote nachotaka maana pale bar kulikuwa na nyama choma na vitu mbalimbali ila nilimwambia "Nashukuru",kiukweli mimi ni ngumu sana kumzoea mtu kwa muda mfupi ,yote hii ilinifanya nione kama naboreka kuendelea na maongezi yale.

Baada ya kukataa offer zile akampa mhudumu Tsh 1000/= akamwambia nikimaliza soda niongeze,basi wakati naangalia mpira alirudi ndani , yeye alikuwa amekaa nje ya bar akanichek akaniuliza "upo" nikamjibu na akaniambia "ukimaliza kinywaji chukua tena nimekwisha lipia",bado nilikuwa sijajua yule mtu ni nani na kwanini amenichangamkia kiasi kile.

Ilipofika mapumziko nikiwa nimeboreka kwa ukaribu ule nikaamua kumuaga mwenzangu na kurudi kulala ,ile natoka tu nje nikakutana nae akiwa mezani na wenzake kama wanne (wanaume 3 na Binti 1) walikuwa wanakula nakunywa pombe.

Alinishika mkono na kunisogeza mbele ya wale wenzake na kuanza kunihoji maswali " wewe ni mwenyeji wa arusha? Nilijibu natokea mkoa mmoja kanda ya ziwa akasema "kweli kwa mwili huo sishangai kutokea huko" nilizidi kujiuliza yeye ni nani na anataka nini baada ya muda nikamwomba tuzungumze moja ya lugha iliyopo mkoani mara ila akasema yeye si wa huko ni mtu wa Kigoma (ila awali aliniambia yeye ni mzaliwa wa mkoani mara )

Nikiendelea na mazungumzo mmoja kati ya wale wenzake akasimama na tablet na akaanza kutupiga picha nikiwa na yule mtu,alipiga picha kama Tano (akili ilianza kwenda kasi ikizidi kutaka kujua wale ni wakina nani na wana nia gani na mimi hadi kufikia kunipiga picha).

Baada ya cameraman kufanya yake jamaa aliomba namba za simu na akaomba nimtafute kesho yake (saa nne asubuhi,huku akisisitiza) nilichukua zile namba ila mimi sikumpa namba zangu.

Aliniuliza napoishi nikazidi kusema uongo kwani huwa sipendi kujivua nguo kwa mtu nisiyemjua ,basi nikaagana nae kisha nikaondoka ma kwenda kulala baada ya kuona mwili wangu umekataa kukaa sehemu ile.

Kesho yake na mimi sikumtafuta nilichana karatasi yenye namba zake nakumbuka zilikuwa za Airtel.

Sikumwambia mwanachuo yeyote juu ya tukio lile hadi leo na huwa nikilikumbuka huwa nakosa sana amani kwanza zile picha zilikuwa na maana gani !!! Hali hii ilinifanya kukosa amani kwa muda mrefu nikiwa jijini Arusha.

Kama kuna mdau JF ashakutana na watu wa aina hii basi unaweza funguka ili niangalie nia na lengo lao kwangu lilikuwa ni lipi.

Natanguliza shukrani.
Usiwe unaongea ongea na watu usiowajua,mpaka upigwe picha ni wewe mwenyewe ndo uliluhusu hali hyo,mtu unampa jibu moja tu akikutazama na usoni anajua anaemuuliza ni Rambo,atapotea mwenyewe.sasa wewe unanuliwa soda unaikubali,why mtu akununulie soda.unapigwa picha unakubali pia.dah!
 
Usiwe unaongea ongea na watu usiowajua,mpaka upigwe picha ni wewe mwenyewe ndo uliluhusu hali hyo,mtu unampa jibu moja tu akikutazama na usoni anajua anaemuuliza ni Rambo,atapotea mwenyewe.sasa wewe unanuliwa soda unaikubali,why mtu akununulie soda.unapigwa picha unakubali pia.dah!
Ndio maana nikamwambia maswali ni mengi kuliko majibu....
 
Na wewe ulikosea kumpa ushiriano kwa muda ule mchache mpaka picha ukapiga siku nyingine uwe makini hao sio watu wazuri inaonekana kabisaaaa.
 
Kwanza mshukuru Mungu uliondoka salama na kukupa ujasiri wa kuchana namba zao. Pia jiepushe sana kukubali kupiga picha hovyo na usiowajua na hata unaowajua wakati mwingine. Angalia sehemu za kujichanganya na uwe mshapu kwa kutafuta njia za kukatisha mazungumzo yasiyoendana na wewe
 
Nimewahi kukutana na hili tukio, arusha ni mji wa kitalii wazungu wakifuka huku huwa wanatafuta watu wa kuwapa strong sex, hivyo huwatumia wenyeji wao kutafuta watu wenye miili ya kuwaridhisha kingono.

Wenzao huwa wakirudi kwao huwasimulia jinsi waafrika wanavyoweza mambo ya kitandani.
Hivyo huwatuma wenyeji kuwatafuta watu hao Kwa makubalia ya kulipwa dola nyingi sana.

Walikupiga picha ili waende kuwaomyesha hao wazungu kama unafaa.
Kama ungeonekana unafaa basi wangekupeleka Kwa hao wazungu na ungeongea nao habari za malipo.

Nimeishi na hao wazungu nchi nyingi hapa Afrika na ndo tabia zao. Hao watu walitumwa kutafuta mtu Mwenye mwili kama wa kwako.
Jinsia inategemiana na mwitaji, wakatimwingine wanatafutwa wa kiume, wakati mwingine wa kike.
 
Back
Top Bottom