Arusha ,mji ulionifanya kukosa amani.

Arusha ,mji ulionifanya kukosa amani.

Kutokana na uandishi na maudhui, yaonyesha mwandishi ni mwanamke.
ni mara chache wanawake kuongozana kwenda kuangalia mpira, halafu hata approach ya huyo jamaa ilikuwa ni ya kiume, ingekuwa ni mwanamke asingeleta hapa kwa sababu kuitwa itwa ni sehemu ya maisha yao na ni kawaida.
 
Siku hizi maisha yamebadilika sana mkuu hapo, kila kitu kinawezekana inawezekana hao jamaa sio watu wazuri walikuwa na lengo baya au ilikuwa ni ishu ya kufahamiana tu ila hata hivyo uliwavumilia sana wamekuita paka na wamekupiga picha bila idhini yako unawaangalia tu ningekuwa mimi hapo bar pasingetosha pamoja na sifa mbaya za watu wa Arusha nisingewaogopa hata kidogo
 
Usiwe unaongea ongea na watu usiowajua,mpaka upigwe picha ni wewe mwenyewe ndo uliluhusu hali hyo,mtu unampa jibu moja tu akikutazama na usoni anajua anaemuuliza ni Rambo,atapotea mwenyewe.sasa wewe unanuliwa soda unaikubali,why mtu akununulie soda.unapigwa picha unakubali pia.dah!
Wala soda niliyonunua ilipoisha sikuongeza tena kinywaji na kuhusu picha ilikuwa ghafla katikati ya maongezi,ndipo mmoja kati yao alipiga picha nikiwa na yule jamaa.
 
Kwanza mshukuru Mungu uliondoka salama na kukupa ujasiri wa kuchana namba zao. Pia jiepushe sana kukubali kupiga picha hovyo na usiowajua na hata unaowajua wakati mwingine. Angalia sehemu za kujichanganya na uwe mshapu kwa kutafuta njia za kukatisha mazungumzo yasiyoendana na wewe
Naam hadi leo huwa nafikiria kile kisa nashindwa kujua kulikuwa an lengo lipi kwangu ila mwisho nimshukuru mungu kwa ulinzi wake juu yangu.
 
Nimewahi kukutana na hili tukio, arusha ni mji wa kitalii wazungu wakifuka huku huwa wanatafuta watu wa kuwapa strong sex, hivyo huwatumia wenyeji wao kutafuta watu wenye miili ya kuwaridhisha kingono.

Wenzao huwa wakirudi kwao huwasimulia jinsi waafrika wanavyoweza mambo ya kitandani.
Hivyo huwatuma wenyeji kuwatafuta watu hao Kwa makubalia ya kulipwa dola nyingi sana.

Walikupiga picha ili waende kuwaomyesha hao wazungu kama unafaa.
Kama ungeonekana unafaa basi wangekupeleka Kwa hao wazungu na ungeongea nao habari za malipo.

Nimeishi na hao wazungu nchi nyingi hapa Afrika na ndo tabia zao. Hao watu walitumwa kutafuta mtu Mwenye mwili kama wa kwako.
Jinsia inategemiana na mwitaji, wakatimwingine wanatafutwa wa kiume, wakati mwingine wa kike.
Kumbe kuna biashara za kutafuta watu kwa ajili ya ngono!!! Asante sana kwa ku-share nasi tukio hili ,nadhani kwa wengine watakakumbwa na adha hii watajua wapi pa kuanzia.
 
Siku hizi maisha yamebadilika sana mkuu hapo, kila kitu kinawezekana inawezekana hao jamaa sio watu wazuri walikuwa na lengo baya au ilikuwa ni ishu ya kufahamiana tu ila hata hivyo uliwavumilia sana wamekuita paka na wamekupiga picha bila idhini yako unawaangalia tu ningekuwa mimi hapo bar pasingetosha pamoja na sifa mbaya za watu wa Arusha nisingewaogopa hata kidogo
Hizi picha hata mimi baada ya kurudi kulala zilinifanya nizidi kuchanganyikiwa sana ,nini lengo la kupiga picha !!!
 
Raphael wa Ureno nadhani bar unayozungumzia kwenye hki kisa ni Kili time na sio kilimanjaro bar. Hii ipo next to City link hotel maeneo ya kurugenzi Arusha
 
Uzi huu ungekamilika kama walau nawe muhanga ungetoa picha ya unadhani nini kilitaka kukutokea baadae iwapo ungefuata matakwa yao,naandika hivi sababu we umeeleza tu aliekuhoji kuwa ni wazi waonekana unatokea kaskazini ila we hujatueleza yule uliyekuwa unastorika nae yukoje mrembo au anatisha na Ile kampani yake uliiona maana mpaka wakakupiga picha wakoje,wako kama wabana pua au wamekaa kishari shari maana kama we mtoto WA mjini ukimuona mtu tu unaanza mtolea mitazamo tofauti kama amekaa kiteja utaweka simu yako mbali,mbabe ka Scorpion utajua hapa soon hapatatosha kana anabana pua kama hawa wanaotuburudisha kwenye luninga utahisi hapa Kuna kitu wanataka nipewe ambacho ni kigumu kumuomba mwanaume mwenzio na wangekuwa na sura ya kondoo ungejua wanataka kukushauri ujiunge labda na fellowship yao.
Sasa tatizo mdau hujatupa walau kidogo taswira ya hao watu unatupa wakati mgumu kutaka kukutolea ufafanuzi ukifikiria kwamba we ndio uliowaona,ongea nao na ukawatoroka, hebu rudi tena ujazie Nyama maana Kuna vitu hujaviweka sawa.......

....,
Mwonekano wa wale watu hasa huyu aliyekuwa kaunta alionesha licha ya kunywa pombe hakuwa kwenye kiwango cha juu cha ulevi alikuwa kawaida na yule binti alikuwa na miaka kati ya 19-23 ila yule kaka mpiga picha yeye alionekana kama mtu wa mazoezi sana kwani alikuwa mpana sana juu (kifua) ila wengine mwanaume mwingine yule alikaa kimya sana wakati wa mazungmzo na yeye alikuwa na miaka kati ya 30-35.
 
ni mara chache wanawake kuongozana kwenda kuangalia mpira, halafu hata approach ya huyo jamaa ilikuwa ni ya kiume, ingekuwa ni mwanamke asingeleta hapa kwa sababu kuitwa itwa ni sehemu ya maisha yao na ni kawaida.
Nimesema hivyo kutokana na utata wa sentensi na tukio.

Sasa mwanaume unafika bar tu upewe ofa ya fasta afu unakua mpole?

Anataka kuondoka anasimamishwa anasifiwa umbo? Siriaz?

Mara akapigwa picha (angalia jinsi alivyolalamikia picha)

Na wanaume hatukai nayo, ukifika maskani au popote unalielezea tunacheka yanaisha.

Uandishi una walakini sana.
 
Hapo ndio karibu na mtaa wangu kuna wajamaa wanafanya tabia mbaya sii kidogo bora ulikacha yaani kuna wehu wanataka marinda tu
 
Nimesema hivyo kutokana na utata wa sentensi na tukio.

Sasa mwanaume unafika bar tu upewe ofa ya fasta afu unakua mpole?

Anataka kuondoka anasimamishwa anasifiwa umbo? Siriaz?

Mara akapigwa picha (angalia jinsi alivyolalamikia picha)

Na wanaume hatukai nayo, ukifika maskani au popote unalielezea tunacheka yanaisha.

Uandishi una walakini sana.
haha, design kama mchalii flani hv siyo wa kujichanganya, machalii wengi siku hizi wananishi kishua shua, angekuwa ni mchalii wa kitaa, lazma angewaka
 
Tulivamiwa na majambazi tukiwa hostel kule njiro sitasahau maisha yangu yote, machalii ni noma
 
Nimekumbuka sana mji wa Arusha ambao kiukweli ulikuwa mji mzuri na wenye hali nzuri ya hewa ila gharama za maisha zilikuwa juu sana (nadhani sababu kuu ni utalii)

Nikiuzungumzia mji huu sitoacha kukumbuka tukio hili ambalo liliniacha na maswali mengi,Mnamo mwezi june mwaka 2015 wakati nikiwa chuoni katika mji wa Arusha nilikuwa naenda kwenye bar moja "kilimanjaro bar" ipo mkabala na city link.

Siku hiyo nilifika hapo kuangalia mechi na katika bar ile ulikuwa ukinunua kinywaji na kuangalia mtanange wako bila wasiwasi.

Wakati naingia kwenye hiyo bar mimi na mwenzangu moja kwa moja hadi kaunta nikatoa wallet nikanunua take away Mbili (soda),Ila wakati nipo kaunta pembeni yangu alikuwepo ndugu mmoja anaweza kuwa na umri kati ya miaka 35-45 alinisalimia "vipi kaka" nikamjibu nikachukua soda zangu mbili,moja yangu na nyingine ya mwenzangu ile nataka kuondoka akaniita akamwambia mhudumu mmoja kuwa "huyo kaka mpe pombe nitalipia mimi" nikamwambia "situmii kilevi chochote"

Akaonekana kutahamaki ila akasema nile chochote nachotaka maana pale bar kulikuwa na nyama choma na vitu mbalimbali ila nilimwambia "Nashukuru",kiukweli mimi ni ngumu sana kumzoea mtu kwa muda mfupi ,yote hii ilinifanya nione kama naboreka kuendelea na maongezi yale.

Baada ya kukataa offer zile akampa mhudumu Tsh 1000/= akamwambia nikimaliza soda niongeze,basi wakati naangalia mpira alirudi ndani , yeye alikuwa amekaa nje ya bar akanichek akaniuliza "upo" nikamjibu na akaniambia "ukimaliza kinywaji chukua tena nimekwisha lipia",bado nilikuwa sijajua yule mtu ni nani na kwanini amenichangamkia kiasi kile.

Ilipofika mapumziko nikiwa nimeboreka kwa ukaribu ule nikaamua kumuaga mwenzangu na kurudi kulala ,ile natoka tu nje nikakutana nae akiwa mezani na wenzake kama wanne (wanaume 3 na Binti 1) walikuwa wanakula nakunywa pombe.

Alinishika mkono na kunisogeza mbele ya wale wenzake na kuanza kunihoji maswali " wewe ni mwenyeji wa arusha? Nilijibu natokea mkoa mmoja kanda ya ziwa akasema "kweli kwa mwili huo sishangai kutokea huko" nilizidi kujiuliza yeye ni nani na anataka nini baada ya muda nikamwomba tuzungumze moja ya lugha iliyopo mkoani mara ila akasema yeye si wa huko ni mtu wa Kigoma (ila awali aliniambia yeye ni mzaliwa wa mkoani mara )

Nikiendelea na mazungumzo mmoja kati ya wale wenzake akasimama na tablet na akaanza kutupiga picha nikiwa na yule mtu,alipiga picha kama Tano (akili ilianza kwenda kasi ikizidi kutaka kujua wale ni wakina nani na wana nia gani na mimi hadi kufikia kunipiga picha).

Baada ya cameraman kufanya yake jamaa aliomba namba za simu na akaomba nimtafute kesho yake (saa nne asubuhi,huku akisisitiza) nilichukua zile namba ila mimi sikumpa namba zangu.

Aliniuliza napoishi nikazidi kusema uongo kwani huwa sipendi kujivua nguo kwa mtu nisiyemjua ,basi nikaagana nae kisha nikaondoka ma kwenda kulala baada ya kuona mwili wangu umekataa kukaa sehemu ile.

Kesho yake na mimi sikumtafuta nilichana karatasi yenye namba zake nakumbuka zilikuwa za Airtel.

Sikumwambia mwanachuo yeyote juu ya tukio lile hadi leo na huwa nikilikumbuka huwa nakosa sana amani kwanza zile picha zilikuwa na maana gani !!! Hali hii ilinifanya kukosa amani kwa muda mrefu nikiwa jijini Arusha.

Kama kuna mdau JF ashakutana na watu wa aina hii basi unaweza funguka ili niangalie nia na lengo lao kwangu lilikuwa ni lipi.

Natanguliza shukrani.
Mi bado nashangaa kwamba jamaa wanakung'ang'ani kiasi hicho bila kukwachia. Hii ni kwa sababu waligundu moja ya weakness yako ni kukataa kwa woga na kumpatia mtu usiye mjua muda wa ku-burgain mambo ambayo hauko tayari kufanya.
Aidha walikwona una kauoga au ushamba fulani kwa mwonekano labda pamoja na kutokuwa na comfidance wewe mwenyewe.
Ni dharau kubwa mtu humjui kuendelea kukuandama mara kadhaa mpaka kukuita mbele ya rafiki zake na wewe ukakubali kwenda japo hukutaka tena ukalazimishwa kupigwa picha bila kuonyesha upinzani. Huo ni udhaifu mkubwa sana.
Kuna mazingira unajiweka mpaka mtu anakuchukulia poa na kukudharau.

Binafsi huwa sitoagi fursa ya mtu nisiye mjua kunishobokea bila sababu ya msingi!
 
Hapo arusha kipindi hicho 2010 niko form five pale Ilboru, nilikutana na fala mmoja (mtu mzima ana kitambi hivi very smart) anabonga kingereza akaanza kunichangamkia. Salam za hapa na pale mara kaanza kunisogelea huku akinisifia nilivojengeka na nilivo na mvuto. Mara sijakaa sawa anaanza kunitolea macho namna suruali yangu ilivotuna kwa mbele huku akitaka kunipapasa hayo maeneo. Akili ikanijia kuwa huyu mtu atakuwa punga ama tapeli tu. Nilipompa kisogo sikugeuka tena nyuma. Kweli Arusha sio sehemu salama kiviiile. Umakini unahitajika
 
Back
Top Bottom