Arusha: Maisha Bora Kwa kila Mtanzania ndio haya??!!!!!!!

Faulisa

Member
Nov 11, 2009
45
25
attachment.php
attachment.php
attachment.php

Katika hekaheka za safisha jiji leo arusha bado Manispal ya mjini hapa wakiendelea kuwaondoa wale wote wanaofanya biashara maeneo ya barabarani, leo nilikutana nao wakiwa wanaviondoa vibanda hivyo kwa wale waliokaidi agizo hilo.

Ni kweli jiji linakuwa safi lakini je hawa watu wanakwenda wapi? je kuondoa uwanja wa NMC waliouteuwa kuwa soko kuna eneo lingine lililoteuliwa kwa ajili yao? NMC hauna huwezo wa kuwaweka wafanyabiasha hawa je serikali wanaliona hii kama tatizo la Taifa?au hadi pochi zetu ziishe kwa kuchukuliwa na vibaka ndio wajue chazo?

Pamoja na yote tunahitaji jiji liwe safi.Basi tunawataka manispal wawe wabunifu wawatafutie mahali ambapo wataweza kujibatia riziki angalae waweze kuendesha familia zao.Je serikali inajua kuwa watoto hawaindi shule, hawapati milo mitatu kwa siku hata matibabu ndio kabisa bado kodi ya nyumba, Je Maisha bora kwa kila Mtanzania Itawezakana??????

Chanzo: Tanzania AsiliaLive
 

Attachments

  • DSCN2275.jpg
    DSCN2275.jpg
    333.4 KB · Views: 283
  • DSCN2280.jpg
    DSCN2280.jpg
    523.9 KB · Views: 304
  • DSCN2283.jpg
    DSCN2283.jpg
    316.5 KB · Views: 284
Ngoja wamalizie msimu wao, watabaki historia kama kulikuwa na chama kinaitwa CCMabwepande...wapuuzi sana wameshindwa kubuni sehemu za kuwa peleka machinga wamebaki kutumia guvu tu...
 
Ngoja wamalizie msimu wao, watabaki historia kama kulikuwa na chama kinaitwa CCMabwepande...wapuuzi sana wameshindwa kubuni sehemu za kuwa peleka machinga wamebaki kutumia guvu tu...
Jaani natamani masaa yawe matatu mchana na usiku matatu tuwaondoe kwa vigelegele tu na sio kura maana hata kura wataona aibu kuhesabu.
 
Je hukuona rais alivyokuwa anajivinjari huko Canada jana? Farasi wa kizungu walivyomsonga ana nafasi ya kufikiria maisha bora kwa kila mtanzania? Yale aliyoahidi yameishia kuwa maisha bora kwake, mkewe, na wanae. Watanzania wameambulia kulipuliwa tu na vitu vizito na mabomu ya kivita huku Joyce Banda akiondoka na kipande cha Ziwa Nyasa kama zawadi ya yale waliyopeana kule Msumbiji. Ama kweli DHAIFU habandikwi jina ila maisha bora kwa kila mtanzania huku tanzanite, dhahabu, gasi, na mengine yakigawanywa bure kwa wazungu!
 
Serikali ya ccm ina amani na furaha isiyo ya kifani pale wanapoona mtu anatembea barabarani anaongea mwenyewe
 
wametuharibia utaratibu sana........kuna watu wangu nilikuwa nanunua viatu kwao....nimewatafuta siku ya nne sasa siwaoni.....kwa nini wasiwaweke hawa watu sehemu moja ili tunapowatafuta tuwapate.....?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom