Arusha: Lema amewapa kilema Wanaarusha

Wakimfunga.... Lowassa achukue jimbo bila hata ya kampeni
 
Achana na mambo ambayo yako mahakamani. Huwezi kutabiri kitakachotokea. Anaweza kulambwa kifungo cha miezi 6 au zaidi na hivyo kumuondolea sifa ya kuwa mbunge kwa miaka 10. Tuache sheria ichukue mkondo wake. Tuache viherehere.
 

Mkuu Rejea tu tukio la Geita kulikuwa na sababu ipi ya kuwapiga raia waliokuwa wanamsalimia Lowassa. Nchi imekuwa ni ya vitisho. Viongozi ni wavivu wa kufikiri ni aibu tupu wanachofanya.
 
Angalia utaolewa huko kwa ujinga wako wakuwafuata mabwana za watu Arusha
 
Mkuu Rejea tu tukio la Geita kulikuwa na sababu ipi ya kuwapiga raia waliokuwa wanamsalimia Lowassa. Nchi imekuwa ni ya vitisho. Viongozi ni wavivu wa kufikiri ni aibu tupu wanachofanya.

Vitisho vyao vina mwisho kwani kila lenye mwanzo halikosi mwisho. Kwa tukio la Geita na tukio la kumkamata Lema wanasababisha hata watoto wadogo wajiulize " Huyu Lema na Lowasa ni akina nani"

Nakumbuka wakati wa kampeni mwaka 2015 watoto wadogo mtaani kwangu ambao baba yao ni Mjumbe wetu wa nyumba kumi, kila mara wakicheza lazima walikuwa wanasema "MABADILIKO LOWASA, LOWASA MABADILIKO" na ndivyo ilivyo pia watajiuliza ni kwanini hawa watu wapo midomoni mwa watu wanatajwa. Leo hii hata watoto wadogo wakipewa nafasi ya kupiga kura wataandika jina la Lowasa na Lema na hakuna mwingine.

Hivyo viongozi wetu wanashindwa kufikiria kuleta maendeleo kwa wananchi kutwa wanawaza namna ya kupambana na wapinzani.

Si ajabu miaka hii mitano ya mwanzo tutaishia kupambana na wapinzani na hakuna maendeleo hata ahadi zao hazifanyiki kipindi hiki.

​
 
Hii kesi wana frame wamfunge masikini Lema! Ila kwa hasira nadhani hata wakimfunga akapoteza ubunge wake......hawatapata lile jimbo!!!
 
Kila mtu afe kivyake.kuzoeazoea watu mwishowe utazoea majini.Mwana F.A 2:5
 
Huwezi kumtenganisha Lema na Arusha, kuitaja Arusha bila Lema haiwezekani, kuanguka kwa Lema ni kuanguka kwa Arusha, Lema amefanya wana Arusha kujisimamia kwa hali na mali bila kujali kama kuna serikali kuu, hata mapato ya jiji yameongezeka tangu Lema awe mbunge yameongezeka mara mia baada ya halmashauri ya jiji kuwa chini ya chadema, so Arusha inaweza kujiendesha kwa mapato yake.. viva Lema haki itasimama juu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…