Arusha: Lema 'aendelea kuongoza' akiwa mahabusu

Arusha: Lema 'aendelea kuongoza' akiwa mahabusu

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) ambaye yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo anaendelea kutenda na kumudu kazi zake akiwa mahabusu. Taarifa za kuaminika zinaonesha kuwa Lema huombwa mawazo, maelekezo na ushauri kabla ya kufanyika jambo lolote Arusha.

Mambo yote yafanyikayo kwa kujadiliwa au kuamriwa na Baraza la Madiwani la Arusha ambalo linadhibitiwa na CHADEMA yanahusisha mawazo na melekezo ya Mbunge Lema. Taarifa zinaonesha kuwa Lema yu katika afya njema na mwenye ari kubwa ya kutenda kazi.

Lema, Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Arusha Mjini aliyeweza kutetea kiti chake cha Ubunge, anahusishwa na kuhusika na kila jambo jimboni Arusha katika kulipanga, kulijadili na kuliamua. Lema anatajwa kuwa ni mmoja wa Wabunge machachari wa upinzani nchini.

Yuko mahabusu baada ya kukosa dhamana katika mahakama huko Arusha katika kesi zake mbili za jinai. Bado Lema anapambania kupata dhamana huku akiendelea na kesi zake za jinai.

Mwafaaaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Hahahah Uncle,waangalie tu isije ikawa wanamtandikia mtu jamvi,bora waambie Ma-Ficiem,wanataamani tupoktee kwenye map,hahahahah Darasa kamaliza
 
Hahahah Uncle,waangalie tu isije ikawa wanamtandikia mtu jamvi,bora waambie Ma-Ficiem,wanataamani tupoktee kwenye map,hahahahah Darasa kamaliza
Mwanangu Tetty, punguza uchochezi

Mzee Tupatupa
 
Tz tuna mambo INA maana waliopo nje hawezi kufikiri vizuri mpaka aliyopo mahabusu atoe maamuzi nini kifanyike nje.

Tuna kazi kubwa kufika Maendeleo ya kweli kama kama viongozi Huru wanategemea mawazo ya kiongozi under custody.

Tungekuwa Tuko uwanja ws vita sawa lakini watu wako Hutu mmmmh its ridiculous
jpm kwa kupwaya anawaandama wenye mawazo mbadala licha yake kutoeleweka kabisa
 
Ulaghali huu..
Unajua hili jukwaa linazo data kibao za hiyo barabara na hata uzinduzi wake uko humu?
Afu unadanganya watu kuwa barabara imejengwa kwa kodi za wana Arusha...??
Kuweni na aibu hata kidogo.
Ziweke hizo data maana sasa wewe ndiye unapoga blabla
 
Hizo fund mbona hazikufanyika kipindi cha felix mrema au kinana? Acheni wivu kila jambo hunda na nyota baba, na Arusha now watu wanaishi kwa kufaidi nyota ya muwakilishi wao.
......
......mwambie H uyo kapuku LEMA mtumishi wa Mungu
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) ambaye yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo anaendelea kutenda na kumudu kazi zake akiwa mahabusu. Taarifa za kuaminika zinaonesha kuwa Lema huombwa mawazo, maelekezo na ushauri kabla ya kufanyika jambo lolote Arusha.

Mambo yote yafanyikayo kwa kujadiliwa au kuamriwa na Baraza la Madiwani la Arusha ambalo linadhibitiwa na CHADEMA yanahusisha mawazo na melekezo ya Mbunge Lema. Taarifa zinaonesha kuwa Lema yu katika afya njema na mwenye ari kubwa ya kutenda kazi.

Lema, Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Arusha Mjini aliyeweza kutetea kiti chake cha Ubunge, anahusishwa na kuhusika na kila jambo jimboni Arusha katika kulipanga, kulijadili na kuliamua. Lema anatajwa kuwa ni mmoja wa Wabunge machachari wa upinzani nchini.

Yuko mahabusu baada ya kukosa dhamana katika mahakama huko Arusha katika kesi zake mbili za jinai. Bado Lema anapambania kupata dhamana huku akiendelea na kesi zake za jinai.

Mwafaaaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Nonsense! mtu analala saa kumi jioni anaongoza vipi ikiwa kumuona ni mpaka wikiendi tena kwa dak 10.
Acheni kujifariji Lema yupo kwenye wakati mgumu tokea azaliwe
 
jpm kwa kupwaya anawaandama wenye mawazo mbadala licha yake kutoeleweka kabisa
Lema hana mawazo mbadala bali Anafanya Fujo tu kule Arusha.Kwani Wabunge wa upinzani nchi hii ni Lema tu wengine hakuna.

Nchi haitaki wafanya fujo nchi inataka wafanyakazi ili kuleta Maendeleo ya MTU mmoja mmoja na hatimaye nchi nzima kwa ujumla.
 
C unafiki ni ukweli uliowazi kuwa wabunge wa upinzani wanajitahidi kuwasilisha hoja zenye mrengo wa kitaifa hawa wa Lumumba chama kwanza

Hata hawa wa upinzani siku wakifanikiwa kuwa watawala, na kuamua kuendelea na katiba hii ya 1977 basi asilimia kubwa watageuka kuwa watetezi wa serikali badala ya wananchi. Katiba ya sasa imewafunga wabunge na misukule ya vyama vyao. Hivyo basi, ukionekana mkorofi na hauendeani na matakwa ya chama dola, basi siku zako zitahesabika chamani, na ukipoteza uanachama, umepoteza ubunge, wangapi wapo tayari kwa hilo? Katiba ya sasa ina maslahi makubwa sana kwa watawala au watawala wajao, na itachukua uzalendo wa hali ya juu kukubali kuibadili, ili iangalie maslahi ya walio wengi zaidi (wananchi wa kawaida). Mpaka sasa ukiangalia chama tawala ni dhahiri kinapenda madaraka na kipo tayari kubaki madarakani kwa nguvu na hila yeyote. Lakini, ukiangalia pia vyama vyetu vya upinzani, vina dalili kubwa ya uchu wa madaraka haswa ukiangalia viongozi wake wa juu. Vyama vingi vya upinzani vikiongozwa na CHADEMA, wenyeviti wamengangania uenyekiti wao na hawataki kupisha wengine. Hii sio dalili njema kwa muskbali wa demokrasia. Upande wa CCM wanabadilishana kila miaka 10 kwasababu wanayo serikali, na wao siku wakikosa serikali, basi hili tatizo litaonekana pia. Hiki ni kitendawili kinachoikabili nchi yetu...maslahi binafsi mbele, nchi nyuma.
 
Lema hana mawazo mbadala bali Anafanya Fujo tu kule Arusha.Kwani Wabunge wa upinzani nchi hii ni Lema tu wengine hakuna.

Nchi haitaki wafanya fujo nchi inataka wafanyakazi ili kuleta Maendeleo ya MTU mmoja mmoja na hatimaye nchi nzima kwa ujumla.
Nijuavyo nchi hii inatawaliwa na wapigaji. Fujo ya Lema sijui ni ipi lakini mlimtaka Lema kwa mabilioni ili mpite bwelele Arusha akawatolea nje. Anachopitia alikijua na tulikijua hatushangai.
 
Nijuavyo nchi hii inatawaliwa na wapigaji. Fujo ya Lema sijui ni ipi lakini mlimtaka Lema kwa mabilioni ili mpite bwelele Arusha akawatolea nje. Anachopitia alikijua na tulikijua hatushangai.
.....
......Arusha Chadema daima
 
Back
Top Bottom