Arusha: Kiwanda ‘bubu’ kinachozalisha pombe kali chakamatwa

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
664
1,272
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa Sakina ambaye ni msimamizi wa kiwanda bubu kinachozalisha pombe kali na kumkuta akiwa na vitu mbalimbali ikiwemo stika 340 za TRA, chupa 483 za pombe kali, mtambo wa kutengenezea pombe hiyo pamoja na pipa lililojaa pombe kali lita 250.
 
Huyu nilimwambia aondoke tu ahesabu hasara akakaza shingo

20210525_171140.jpg
IMG_20210525_171236.jpg
IMG_20210525_171314.jpg
 
Huyo lazima atakuwa mkemia aliyekuwa anapika hizo Konyagi kiwandani kwao wakampunguza!!! Akasema isiwe taabu kama formulae ninayo nitatengeneza nyumbani!!! Konyagi si inatengenezwa kutokana na gongo!!!!!

Inanikumbusha hadithi ya High Court judge mmoja mstaafu aliyetoa ushuhuda kuwa akiwa kwenye bench hakuwahi kumtia hatiani hata siku moja mwana mama yeyote aliyeletwa mbele yake kwakushtakiwa kwa kuuza gongo!! Sababu yake ikiwa, yeye alisomeshwa shule kwa fedha ambazo mama yake alizipata kwa kuuza gongo; hence it would have been disingenuous to punish such women!!!
 
#HABARI Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa Sakina ambaye ni msimamizi wa kiwanda bubu kinachozalisha pombe kali na kumkuta akiwa na vitu mbalimbali ikiwemo stika 340 za TRA, chupa 483 za pombe kali, mtambo wa kutengenezea pombe hiyo pamoja na pipa lililojaa pombe kali lita 250.
Pombe kali isiyokuwa na jina ni pombe gani isijekuwa chang'aa
 
Sheria na taratibu zetu mbovu zinaua vipaji na ubunifu, Huyu angepewa zile 10 mil kama za wale wabunifu wa mitambo ya umeme . SSH naye afanye kama JPM halafu mwanamke mwenzie huyo
 
Alipokuwepo Jiwe hamkutoa maoni ya kijinga kama haya
Ukiona hivyo ujuwe kuna baadhi ya watu wamemsusia Mama Nchi,hadi police hawana tena morali ya kazi zao ndiyo maana unaona na ujambazi nao umerudi kwa kasi sana! Tosomeni alama za nyakati,Mambo yamebadilika ghafla Tanzania na Majambazi yanajaribu kutupa ujumbe flani hivi!!
 
Ujasiriamali at the core.... Kakosa mtaji tu big up kwake that's balls..... Ngoja nitafte mkemia tutengeneze kitoko tu
 
Hizo pombe zipo muda mrefu sana. Na sio Arusha tu, karibu nchi nzima.
Dar ndio usiseme. Tumezinywa sana kule Temeketemeke. Na hii ilikuwa miaka ya 1990s.
 
Back
Top Bottom