Arusha & Kilimanjaro: Utajiri, Mapenzi na vifo vya kutisha. Kwanini matajiri hawadumu?

Kwanza kabisa hakuna Moshi na Kilimanjaro, ukishasema Kilimanjaro tayari Moshi ipo ndani yake

Pili Mengi kafa na miaka 75, Mrema kafa na miaka 68, huyo msuya sijui kafa na miaka mingapi ila anaonyesha naye alikuwa ni zaidi ya 65, kuna Ndesamburo amekufa na miaka mingi tu na yeye, na bado wengine wengi tu wanadunda

Sasa umelinganisha na umri upi hadi kusema wanakufa haraka? Wastani wa kuishi kwa mtanzania ni umri gani?

Na je Kilimanjaro au Arusha zina matajiri wangapi hadi uhitimishe kwa kusema kuwa wanakufa vifo vya mapema kwa kuangalia hao watatu uliowataja? kama kuna matajiri labda 100, kisha ukataja watatu ambao walikufa na umri zaidi ya miaka 65 una hitimisha kuwa matajiri wa mikoa fulani wanakufa vifo vya haraka? Elimu yako ni kiasi gani ndugu?

Uzi wako unataka uvutie comments kuwa wanauana na comments kama hizo utazipata sababu ndivyo Watanzania walivyo, mawazo ya kimaskini kuwajadili maisha ya watu
labda yeye hatakufa.
 
Back
Top Bottom