Arusha: Kichanga chakutwa kwenye majani ya malisho

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kichanga chenye umri wa siku moja kimekutwa kimekufa kwenye shamba la majani ya Ng'ombe baada ya kutupwa na mtu asiyejulikana katika mtaa wa Lolovono kata ya Sokoni 1, jijini Arusha

Tukio hilo la kusikitisha limetokea mapema leo kwenye mtaa huo baada ya mwili wa kichanga hicho chenye jinsia ya kike kugunduliwa na wapita njia likiwa kimelazwa kwenye majani ya Malisho ya mifugo, ambao walitoa taarifa kwa majirani.

Mwenyekiti wa mtaa huo,Orgeness Lema amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa tukio hilo ni tukio la pili katika mtaa huo kwa kipindi Cha wiki mbili mfururizo ambapo wiki iliyopita mwili wa kichanga kingine chenye umri wa miezi mitatu uliokotwa kwenye shamba la migomba ukiwa umenyofolewa viungo.

Aidha Mwenyekiti huyo ameapa kuwasaka nyumba kwa nyumba wahusika wote wanaojihusisha kufanya umalaya na kubeba ujauzito na Kisha kuvitupa vichanga baada ya kujifungua.

*Nilipigiwa simu majira ya saa mbili asubuhi na kufika eneo la tukio ambapo nilishuhudia mwili wa kichanga ukiwa kwenye shamba la majani na ndipo nilipowapigia simu polisi ambao walifika na kuuchukua mwili wa kichanga hicho"Alisema Mwenyekiti.

Aidha amesema kuwa serikali ya mtaa kwa kushirikiana na wananchi imeanza msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini kina nani wanaohusika kujifungua na kutupa watoto wao.

"Hili tukio ni la pili katika kipindi Cha wiki mbili mfururizo Sasa nimeagiza kufanyike msako was nyumba kwa nyumba kubaini Nani alikutwa na ujauzito hivi karibuni na Hana Mtoto"amesema.

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo ambao walishuhudia tukio hilo,Happyness,Hamida waziri na Maximilian Olotu wamesikitishwa na kitendo Cha kinyama. kilichofanywa na mtu asiyejulikana na kuwataka wananchi kusaidia kufichua wahusika wa matukio Hilo.

"Inasikitisha kuona mwanamke akijifungua na kutupa Mtoto kwa kisingizio Cha kushindwa kulea tukio hili linapaswa kulaniwa kwa nguvu zote na muhusika asakwe kwa nguvu zote na kufikishw kwenye vyombo vya Sheria ili hatua zaidi ziwwze kuchukuliwa"Alisema Happyness.

1.jpg
Ends
 
Back
Top Bottom