Arusha halisi ilivyo na watu wake

Soma vizur mkuu serengeti ipo karibu na Arusha
 
Hizi mada za kuisifia arusha sijui zina lengo gani.
Ninyi vijana wa arusha hao wakenya wamewalemaza mawazo huko kijijini kwenu arusha mnaanza kuwaiga tabia zao za kibaguzi.
Hivi nikuulize mleta uzi hiyo mada itawasaidia nini watanzania wa mikoa mingine.
Mkumbuke kwamba mnavyozidi kujitekenya humu JF na kisha mnacheka wenyewe mjue watanzania wenye uelewa wanazidi kuwadharau.
Kuna msemo unaosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza huko kujitembeza kwenu mitandaoni kuisifia arusha ni kama mnautafutia bwana mkoa wa arusha.
Tulieni watu watakuja huko arusha na watawasifia hapa JF.
Nitarudi badae
 

Kwani katiba inakataza mtu kujivunia kwake??
 
Hatutaki ligi soma uelewe...amesema zipo ndani ama karibu na mji wa arusha sasa Serengeti inaangukia upande wa karibu na mji wa arusha
Serengeti haipo Arusha,na mleta mada hoja yake kuu anauzungumzia mkoa wa Arusha,sasa suala la kuzungumzia vitu vilivyo karibu mkoa wako na kuvifanya ndio advantage ya mkoa wako hiyo ni irrelevant na hoja yenyewe na yeye mwenyewe mwanzo kabisa amesema hana lengo la kuulinganisha mkoa wa Arusha na mkoa mwingine,so alichopaswa kuzungumzia yeye ni mkoa wa Arusha tu,kama kuwa karibu na Serengeti basi mwanza wako karibu zaidi kuliko Arusha,yeye alipaswa kuzungumzia ni vile vilivyomo Arusha na uzuri wa Arusha tu na maeneo yake kama vile karatu,kwa mrombo,oljoro ,ikidinga, maji ya chai,usa river,ngulelo,ngaramtoni.kisongo,monduli,muriet,majengo,mbauda ,njiro,moshono,kijenge,tengeru,na kwingineko
 
Kitu cha kweli nachojua mimi swala la kipato kingi taifa linavuna ni Dar na Mwanza ikifuatiwa na Mbeya,hiyo ni tosha kuonyesha Arusha imekalia wapi na siyo misifa tu bila la maana,all in all hii ni Tanzania yetu sote,ila mkileta ubaguzi nakuapieni Arusha hamuifati Mwanza,maana hilo ndo hua linawaumiza,sema hamuwezi kuamini kwa sababu jamii ya Mwanza ni ya kistaarabu haina majivuno,kuleta maneno ya kusifia majengo,mala keepleft ndani ya mji kama napoona hapo juu ndugu mmoja kapiga picha na kupost hapa ni utoto tu au kutokuelewa maana maeneo yenu hayo tunayajua na muonekano wa picha siku zote utaona kama kitu kinatisha kumbe ni bla bla.fanyeni mkoa uwe na kipato kizuri kitaifa ndo mjisifie
 

Wewe umeona Serengeti pekee?? Kwani Kilimanjaro upo Arusha?? Alichosema ni zipo au zipo karibu.. Serengeti watalii wote wanaoenda huko wanapitia Arusha.. Kampuni zote za kitalii zinazopeleka watalii Serengeti ni za Arusha.. Ebu niambie wewe ni watalii wangapi wanapitia Mwanza?? Ni kampuni gani ya tours inapeleka watalii Serengeti ambayo HQ zake ni Mwanza au huko Mara?? Purposefully anayefaidika na Serengeti zaidi ni Arusha kuliko hata huyo Mara na Mwanza..
 
Soma vizur mkuu serengeti ipo karibu na Arusha
Mleta mada kajichanganya ,hakupaswa kuhusisha vitu vilivyo karibu na Mkoa wa Arusha kwa msingi wa hoja yake anauzungumzia mkoa wa Arusha sasa kuzungumzia eti Mkoa waArusha upo karibu na mkoa mwingine hapo si sawa,angalia sifa nyingi alizoziorodhesha ni za mkoa wa Arusha tu sasa kama alikua anataka kuuzungumzia mkoa wa Arusha hakupaswa kukodi majeshi na kufanya kama ndio sifa ya mkoa wa Arusha
 

Kipato kipi mkuu?? Kodi inayokusanywa na TRA Arusha ni zaidi ya kodi yote inayokusanywa Mwanza, Kagera na Shinyanga.. GDP per capita ya Arusha ni 2.1 M wakati ya Mwanza ni 1.7 M.. Hizi ni takwimu za kitaalamu si blah blah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…