ARUSHA: Basi Abood lapata ajali

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
752
1,810
Abiria zaidi ya 50 waliokuwa wakitokea jijini Arusha kuelekea Morogoro wamenusurika kufa na baadhi yao kujeruhiwa akiwemo Dereva, baada ya basi la Abood waliokuwa wakisafiria kuligonga gari jingine kwa nyuma katika eneo la Sang'isi , Tengeru mapema asubuhi leo, Polisi wapo eneo la tukio.

Angalia Picha za basi hilo
f234746cbd2badd8155b40a80d7dfeaf.jpg
0f067cea7f7e7d1079466c5dd977f009.jpg
b812cf15a259c94622d4460e08248396.jpg
 
Baada ya barabara kujengwa eneo la tengeru na kuwa double road bado kuna ajali? Madereva wetu hawatakaa wajifunze .
 
Madereva inatakiwa wawe wanakwenda shule kuanzia mwaka mmoja na kuendelea, hawa hawa wamesababisha speed barabarani imekuwa mwendo wa kombe sababu ya uzembe wao lakini bado hawajielewi.
 
Jamani asanteni sana, nami nilikuwa abiria mmojawapo humo. Na nimeahirisha na safari nipo hapa Arusha, tunamshukuru sana Mungu kwa kutulinda sote japo dereva wetu na wengine watatu walipelekwa hospitali Tengeru. Aisee nimejifunza mengi sana kupitia tukio hili, jamani nyie wenye simu kubwa msipende kupiga picha kabla ya kuokoa watu. Wakati tumemaliza kuruka madirishani wengine pale Mbele.
.dereva alikuwa amebanwa hakuweza kutoka hivyo alibakia palepale lakini cha ajabu watu wengi walikuwa busy kupiga picha na vijana wengine walikuwa wanatafuta mali za kuiba...jamani nafsi za watu tuzipe uzito na tusaidie wengine na sio kukimbilia kupiga picha.

Traffic wa barabarani jamani wasaidieni abiria kwa kudhibiti magari asubuhi...wanachokifanya madereva wanawahi kutoka stendi alafu wanakimbilia kupakia abiria njiani hivyo hukimbizana kupakia wote yaani awe anaenda moshi au moro wao husomba tu. Hiki ndicho kilichotuponza wenzenu nusura tuage dunia....ilikuwa mida ya saa kumi na mbili hivyo abiria wengi tulikuwa tukijiweka vizuri Kwenye siti zetu...kwakweli spidi ilikuwa si mchezo...brake zilimgomea jamaa hivyo akaamua kupiga nyuma lakini isingepiga track ya mchanga nadhani ingekuwa stori zingine hapa maana alikuwa akilielekeza kule upande wa chini ambako nahisi tungepoteza nafsi zetu.

Gari inatakiwa itoke stendi saa kumi na mbili kamili lakini gari imetoka saa kumi na mbili kasoro dakika tano. Jamani traffic wasaidie yaani yaachiane mda hawa watu wanakimbilia abiria huko njiani ni hatari....
 
Back
Top Bottom