ARUSHA: Azalisha umeme kwa maji ya mfereji, agundua trekta yenye injini ya pikipiki

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Kutana na Jackson Mungule mkazi wa Arusha ambaye amefanikiwa kuzalisha umeme kwa maji ya mfereji na kuusambaza kwa watu zaidi ya 100.

Pia anazalisha umeme kwa kutumia kinyesi cha mifugo.

Katika hatua nyingine bwana Mungule amefanikiwa kutengeneza trekta kwa kutumia injini ya pikipiki ambayo inatumia mafuta kidogo hivyo kuweza kuwa mkombozi kwa wakulima.

Mgunduzi huyu anaomba serikali imsaidie ili aweze kuongeza ujuzi wake zaidi na kuleta tija kwa taifa.

 
Yaani huyu hasipo pongezwa na kuwezeshwa na kufungua kiwanda cha anachokifanya basi kuna haja ya kuiangalia Tanzania upya kwa maana ya kuitaifiti society yetu kwa kina sana.
 
Huyu watamuuliza kasomea wapi!? Afu kibali kampa nani!? Mwishowe watamwambia afunge tu,maana tanzania watu kama hawa hawatakiwi aseee

Wakati kwenye Western world ndio wanatakiwa sana; halafu sisi tunao halafu tunawazima; halafu tunaenda kuomba trekta nje, na umeme wa kwenye mpira wa miguu kule ambako watu wa namna hii wanathaminiwa sana na kuangaliwa kwa hali ya juu na kupata sifa ya nchi. Lazima kuna kitu sio sawa sehemu fulani.
 
Tanzania inahitaji watu wa aina hii maana kama mafundi mchundo na mainjinia wa ki-Tanzania wangelikuwa wabunifu na wathubutu basi maendeleo ktk sekta ya kilimo, viwanda na miundo-mbinu ya usafiri nchini yangekuwa kama nchi za uchumi wa kati za Asia na Marekani ya Kusini.
 
Back
Top Bottom