Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa majini na nchi kavu, SUMATRA imeonja joto ya jiwe katika ukumbi wa polisi Mesi Arusha, pale ilipoachwa soremba na wamiliki wa magari ya usafirishaji baada ya kutoka nje ya ukumbi huo wakisusia rasimi ya sheria mpya ya makosa ya usafirishaji iliyosheheni utitiri wa faini zinazoanzia sh, 100,000 hadi 250,000.
Rasimu hiyo mpya ilipingwa vikali na chama cha wamiliki wa magari ya abiria AKIBOA na kuamua kutoka nje kususia ambapo ilionekana tayari ilishapitishwa na mamlaka hiyo ila ilikuja kwa lengo la kuwasomea tu.
Hali ilichafuka pale wamiliki wa magari walipokuwa wakitoa maoni yao kwa lengo la kufanyia marekebisho katika SHERIA hiyo mpya lakini vigogo hao wa Sumatra waligoma ndipo wamiliki hapo wa magari walipoamua kwa umoja wao kutoka nje na kususia kikao hicho na kujikuta SUMATRA wakibaki wenyewe na askari Trafiki wachache.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo kuna makosa zaidi ya 100 yameainishwa kwa wamiliki na madereva wa Magari ya abiria yakianzia tozo ya sh,100,000 hadi 250,000 jambo ambalo AKIBOA walidai kuwa SUMTRA imekuja kutafuta mtaji kwa wamiliki wa Magari na si kudhibiti makosa ya usafirishaji.