Arusha: Afisa elimu msingi azua taharuki michango mashuleni, wazazi wamjia juu

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Wazazi katika shule za msingi 48 jiji la Arusha, zinazonufaika na msaada wa chakula unaotolewa na kampuni ya Mount Meru Millers ,wamelalamikia hatua ya kuchangishwa fedha kwa ajili ya kununua kuni kupitia LIPA NAMBA wakidai mpango huo ni kinyume cha maelekezo na miongozo ya serikali.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wamemtupia lawama afisa elimu jiji la Arusha,Hussein Bakari ambaye alitoa maelekezo kwa walimu wakuu wa shule hizo kwa kuwataka wasajili LIPA NAMBA bila kushirikisha wenyeviti wa kamati ya shule jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa serikali.

Jambo hilo limezua taharuki kwa wazazi baada ya kubaini kwamba shule moja ya msingi Osunyai tayari imesajili LIPA NAMBA kwa ajili ya kuchukua michango ya wazazi ili kuchangia kulipia kuni.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha ,Hargeney Chitukuro alipata taarifa hiyo ambayo haikuwa na baraka zake na kuamua kuitisha kikao cha ghafla kati ya kamati za shule na walimu wakuu akiwemo afisa elimu.

Inadaiwa kuwa Chitukuro alimwashia moto afisa elimu huyo kwa kuendesha mpango huo bila kufuata taratibu za serikali ikiwemo ofisi yake.

Chitukuro alitoa maagizo kuwa mdau aendelee kutoa chakula kwenye shule husika na kamati za shule ziendelee na utaratibu wao wa awali kuhusu upatikanaji wa kuni kwa kupata kibali maalumu .

Wazazi wa shule hizo wameshtukia mpango huo wa LIPA NAMBA wakidai ni ulaji wa aina yake wenye lengo la kuwanufaisha wachache kwa sababu hawatajua idadi kamili ya fedha zilizowekwa, makato pamoja na utoaji wa fedha hizo huku wakimlalamikia mwenyekiti wa kamati ya elimu Isaya Doita ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwashawishi baadhi ya wenyeviti wa kamati za shule kuunga mkono wazazi kuchangia fedha hizo kupitia LIPA NAMBA.

Taarifa zinadai kwamba kampuni ya Mt. Meru Millers imesitisha kupeleka chakula katika shule hizo kutokana na mkanganyiko wa maelekezo ya afisa elimu ulioibua taharuki kwa wazazi wakigomea utaratibu huo huku walimu wakitaka maelekezo hayo wapatiwe kwa maandishi wakiitaka TAMISEMI iingilie kati suala hili .

IMG-20221116-WA0028.jpg
IMG-20221116-WA0027.jpg
 
Back
Top Bottom