Arumeru Mashariki ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arumeru Mashariki ya CHADEMA

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mbulumundu, Mar 5, 2012.

 1. M

  Mbulumundu Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  For sure kama kinachoendelea Arumeru Mashariki hakitabadilika, Chadema wana jimbo.Nahofia tu fununu za ununuzi wa kadi za wapiga kura ambao wadau wanaozungumzia pia hawajanipa ushirikiano wa kutosha niweze kupata ushahidi. Kwa aliyeko karibu na eneo hili na mdadisi mzuri afanyie kazi hili!
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mkuu, unamaanisha ccm wamenza tena kununua shahada za kupigia kura Arumeru!!!!
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  sishangai,hamna habari nyingine labda????
   
 4. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Acha kuweweseka kijana . Igunga na uzini mlisema hivo hivo . Mpira dk 90.
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Jamaa wamejipanga vilivyo mkuu,kila kona na mkabaji,hoja za haja kuanzia katiba mpya,mgomo wa madaktari na ufumbuzi wake,mipango na mikakati yao naona huruma kwa CCM
   
 6. e

  evoddy JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sina wasiwais lazima magamba wang'oke
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa Chadema ndiyo wana historia nzuri ya kununua kadi. Ujanja huo waliutumia kule Tarime na Igunga.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni kauli za kawaida tu hizo wala haziwatishi CCM, ilikuwa hivyo hivyo Busanda, Igunga na kwingine. Hata hivyo CDM watashinda kwa sera ipi? ufisadi? Naona kama hawana jipya.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wananchi hawadanganyiki kirahisi hinyo. Wanajua kuwa Mgomo wa Madaktari ulichochewa na CHADEMA na hilo linakwenda kuwamaliza CHADEMA kwa vile watu wana vielelezo na vinakwenda kuwekwa hadharani. Arumeru CHADEMA hakiwezi kupata hata asilimia 30 ya kura zote.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Big Up Mkuu ulijuaje?
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kwani hiyo hapo juu ni hadithi hadi uulizie habari nyingine.
   
 12. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Najua Chadema mngependa Kushinda Arumeru Mashariki lakini kwa Uhakika kabisa CCM lazima ishinde! Ushindi Arumeru Mashariki ni Lazima! CCM oyeeeeeeee!
   
 13. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mtashinda wizi na siyo kura
   
 14. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ningekua Chadema ningeli fanya juhudi kushawishi timu ya kampeni iendelee na kampeni kwa bidii kuliko kuanza kutamani ushindi mda huu!chaguzi ndogo Chadema wamekua na hamu ya kushinda bila kusoma hali halisi na mikakati ya Ushindi inakuaje,mwisho huangukia kulalamika kuwa kura zili ibiwa na CCM! Halafu sera ya Ufisadi inayo tumiwa na Chadema ni ya kitaifa wanashindwa kuelewa matatizo ya eneo husika! Halafu Mgombea huyu huyu wa Chadema alishindwa na Mgongwa Mzee Sumari ambae hakupiga hata kampeni akapata kura 34000 na Nassari 19000,sasa leo hii Nassari anapambana na mtu mzima! Kutabiri ushindi leo Arumeru Mashariki ni Sawa na Kuendesha Mtumbwi kwenye Nchi kavu!
   
 15. B

  BigMan JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  [FONT=&amp]CHADEMA KUTUMIA RED BRIGADE ARUMERU???[/FONT] [FONT=&amp]Na Charles Charles[/FONT] [FONT=&amp]Kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha, zinaanza Machi 9, mwaka huu, lakini uchaguzi wake umepangwa kufanyika Aprili Mosi.

  Tayari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kwamba kinaweza kutumia kikundi kinachoitwa Red Brigade katika jimbo hilo ili kutembeza kipigo, jambo ambalo limeelezwa kwa kisingizio cha kumjibu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.

  Akiandika makala yake kwenye gazeti moja litolewalo kila siku nchini Jumatano, wiki jana, Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alimuonya Nape kuwa Arumeru Mashariki siyo Igunga, kisha akafichua hatari inayoweza kutokea huko.

  Nataka pia kuutolea majibu utapeli uliokusanya hadithi nyingi zilizosheneza uzushi, uongo, uchochezi na ulimbukeni wa madaraka ya kisiasa unaotengenezwa maalum ili Chadema ikishindwa huko Arumeru Mashariki watu wawe wamejengewa mazingira ya kutokubali kupokea matokeo hayo!

  Inaletwa hadithi kuwa Nape anataka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa akagombee ubunge katika jimbo hilo, uongo ambao asiyekuwa mwathirika wa siasa za vurugu hawezi kuuandika mpaka gazetini.

  Mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo hilo mwaka 2010, Joshua Nasari alitangaza kwamba kuna watu wanataka Dk. Slaa agombee nafasi hiyo mwaka huu, jambo ambalo pia lilibarikiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Freeman Mbowe akisema hawana pingamizi lolote kama yeye mwenyewe angeridhia.

  Kauli hizo ndizo zikazungumziwa na Nape kuwa CCM iko tayari kupambana naye huko, na kwamba huo utakuwa mwisho wa ndoto zake kuwania tena urais mwaka 2015.

  Hata hivyo, Nape kamwe hakuzungumzia suala hilo kwa kuita waandishi wa habari ila kwa kuulizwa, tena ilikuwa na gazeti linalomilikiwa na familia ya Mbowe ambaye ndiye bosi wa juu kuliko wote kwa Chadema. Hivyo, inashangaza kwa Mwigamba kutaka kueneza uongo wa makusudi kwa watu.

  Kama kuna tatizo kuhusu Dk. Slaa kutaka akagombee ubunge katika jimbo hilo hapo wanasiasa wambeya ni Nasari na bosi wake Mbowe. Hao ndio watu ambao Mwigamba anapaswa kuwashushua na siyo kudandia mgongo wa Nape kama mlevi wa gongo.

  Anadai eti CCM mwaka huu “itagaragazwa” huko Arumeru Mashariki, ndoto iliyoota usugu kwa viongozi kama yeye na siyo ngeni miongoni mwa Watanzania.

  Ilihubiriwa kila mahali ulipotokea uchaguzi mdogo wa Igunga, Tabora. Mmoja wa viongozi wa Chadema aliyekuwa akitangaza hadi anataka kulazimisha watu waamini hivyo alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Taifa wa Chama hicho, Mwita Mwikwabe Waitara.

  Mwingine alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi (wakati huo), Erasto Tumbo, wale ambao pia walianza kampeni hata kabla ya tarehe rasmi iliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa wakisingizia eti wanafungua mashina ya chama chao.

  Mwigamba na kalamu yake hakuandika chochote kuhusu ukiukaji huo wa sheria na kanuni, hivyo Watanzania hawashangai kumuona leo naye akitangaza utabiri wa mizimu kama vile mganga wa mitishamba kwa kusema CCM itashindwa vibaya huko Arumeru Mashariki.

  Anafikiri kila Mtanzania ni mjinga kiasi kiasi kwamba anaweza kudanganywa kwa urahisi kama mtoto wa chekechea. Anadhani kuwa kura zinapigwa kwa makala za uzushi na uongo magazetini!

  Anadai kuwa Dk. Slaa alipoteuliwa kugombea urais mwaka 2010 ilibidi apelekwe kwanza Karatu ili wananchi wa jimbo hilo wakaulizwe endapo walikuwa radhi au hawataki, kisha akapelekwa kwenye Viwanja vya NMC mjini Arusha, pale ambako watu kutoka wilaya zote za mkoa huo walikusanyika na wao wakaulizwa kama wanaridhia na wao pia wakaruhusu.

  Anadhani hatuelewi ilivyokuwa kazi ngumu kumshawishi agombee nafasi hiyo akisema asingeweza kumshinda mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete hata kama angekesha anachezeshwa maruhani ya kwao.

  Ili aweze kukubali baada ya mvutano mkali ofisini, Chadema ililazimika kumlipa mshahara mkubwa kupindukia na usiokatwa kodi, posho za kufuru na pensheni inayokaribia shilingi milioni 100 mwaka 2015.

  Lakini akihofia kupewa ahadi hewa na chama hicho chenye misingi ya ukabila, ukanda, ukoo na ufamilia, kasisi huyo wa zamani aliyeshindwa kuumudu utakatifu kanisani naye alishinikiza waandikishiane mkataba wa kisheria ili baadaye asije “akarukwa”.

  Huo ndio uongo wa Mwigamba kutaka kuwadanganya Watanzania eti kuwa wana Arusha wamemtoa Dk. Slaa kwa ngazi ya kitaifa, lakini hata alipokuwa Mbunge wa Karatu alikuwa pia ni Katibu Mkuu wa Chadema.

  Inawezekana Mwigamba hajui kama Katibu wa Wilaya ni wa ngazi ya wilaya yote, halafu yule wa mkoa naye eneo lake ni mkoa na Katibu Mkuu anakuwa wa nchi nzima na siyo wa wa mkoa wala jimbo moja. Ndiyo maana Dk. Slaa kamwe hajaanza miaka miwili iliyopita kuwa wa kitaifa ila tangu mwaka 2004.

  Kuhusu “mtiti” wa Chadema uliokuwepo Igunga hapo mwaka jana kama ilivyobainishwa na Mwigamba hata miye nakubali.

  Ulikuwa “mtiti” wa kumwagia tindikali watu na kuwatia vilema vya maisha kutokana na siasa tu za kishamba, na pia ulikuwa “mtiti” wa kujaribu kuwateka wabunge wa CCM baada ya kuona hali inazidi kuwa ngumu kupindukia.

  Ulikuwa “mtiti” wa kuhubiri uzushi, uongo na uchochezi wenye kila aina ya majungu, wivu, chuki na hasira za kuhofia kushindwa licha ya kwenda katika jimbo hilo kwa mbwembwe na vitisho kama “chinjachinja”.

  Kama anavyosema tena Mwigamba kuwa “mtiti” wa Igunga ulikuwa kama “trela” ila wa Arumeru Mashariki utakuwa ni “kiboko”, hapa pia nakubali kwa asilimia 100.

  Nazingatia hulka za viongozi wa Chadema ambao siku zote kazi yao ni kuchonganisha watu ili wafarakane, wanuniane, wavurugane, wapigane, waumizane, wachomeane mali zao kama ilivyokuwa Arusha Januari 5, mwaka jana na ikiwezekana, wengine wapoteze mpaka maisha yao kwa kutolewa “sadaka” au kafara kwa ibada za kishetani.

  Ametumia nafasi yake kama Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha kutangaza kuwa “mtiti” wa Arumeru Mashariki utakuwa mkubwa kuliko wa Igunga, lakini hizo ni juhudi

  za kuwatisha watu ili wasifuatilie kampeni za uchaguzi huo mdogo pindi zikianza na hivyo washindwe kutenganisha mchele na pumba.

  Anataka Nape aulize “mtiti” wa Chadema katika mkoa wa Arusha kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Arusha Mjini mwaka 2010, Dk. Batlida Burian au Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck ole Medeye kusudi wamwambie ukoje.

  Viongozi wa CCM kama Nape kamwe hawafanyi siasa za “mititi” anazohubiri Mwigamba, hivyo hata kumjibu kamwe hawezi kupoteza muda wake maana yupo “bize” anashughulikia itikadi na kueneza chama chake kistaarabu na siyo kwa “mtiti”.

  Anataka pia Nape amuulize Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Luteni Yussuf Makamba kuhusu “mtiti” wa Chadema ulivyokuwa katika uchaguzi mdogo wa Tarime mwaka 2009, kisha atakachoelezwa akizidishe mara moja na nusu ili kujua “mtiti” gani utakuwepo huko Arumeru Mashariki.

  Kama Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Mwigamba ameonyesha kuwa chama chake hakiendi Arumeru Mashariki kushindanisha sera, ilani za uchaguzi wala vinginevyo, badala yake kinakwenda kwa “mtiti” wa vurugu au vita vya silaha na umwagaji wa damu.

  Anafahamu kuwa chama chake hakiwezi kushinda kama ilivyokuwa pia mwaka 2010 wakati mgombea wake wa kiti cha ubunge katika jimbo hilo, Joshua Nasari alipotupiliwa mbali na Jeremiah Sumari wa CCM, yule ambaye sasa ni marehemu na Mungu amrehemu!

  Anatangaza vita mapema kwamba wana “jeshi” linalokwenda Arumeru Mashariki kufanya “mtiti” mkubwa zaidi kuliko wa Tarime na Igunga.

  Anasema watatumia “kikosi” cha Red Brigade ambacho “askari” wake watano watakuwa “wanamshughulikia” mwana CCM mmoja, kazi ambayo ni kumpa mkong’oto ili kutafuta ushindi kwa kuwatisha watu.

  Hayo ndiyo maandalizi ya kigaidi yanayofanywa na viongozi wa Chadema, yale ambayo yanaweza kusababisha kuzuka kwa mauaji ya kikatili kwa kisingizio cha kuwadhibiti vijana wa CCM wasinyanyase wananchi wa Arumeru Mashariki!

  Yanaweza kuwa ni mauaji mabaya zaidi baada ya mwaka jana kule Igunga, mwana CCM mmoja kumwagiwa tindikali usoni na kupelekwa hadi India ili kufanyiwa upasuaji.

  Akitengeneza mazingira mengine ya siasa za kitapeli na kijinga, Mwigamba anadai kwamba anajua CCM itakwenda Arumeru Mashariki kumtumia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Lyatonga Mrema ili kuisaidia ishinde.

  Anasema katika uchaguzi mdogo wa Igunga, mwaka jana, na Uzini uliofanyika wiki mbili zilizopita, CCM ilimtumia Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Civic United Front (Tanzania Bara), Julius Mtatiro na mwenzake wa Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu.[/FONT] [FONT=&amp]
  Kama Tanzania imewahi kuwa na Wenyeviti wa Mikoa wa vyama vya siasa wazushi kupita kiwango basi Chadema inaongoza katika sifa hiyo ya ovyo kupindukia.

  Sifahamu kama Mwigamba alitaka CUF isishiriki chaguzi hizo ndogo ila Chadema peke yake, na pia sijui endapo anadhani kuwa vyama vingine vya upinzani nchini havipaswi kugombea nafasi yoyote ile ya uwakilishi wa umma katika vyombo vya dola kama Bunge, Baraza la Wawakilishi Zanzibar au nafasi za udiwani.

  Ni ujinga kwa mtu kusema kuwa Mtatiro na Jussa walikwenda kuisaidia CCM ili ishinde huko Igunga na Uzini wakati CUF ilikuwa na wagombea wake yenyewe.

  Kama viongozi wa CUF hawakupaswa kwenda kuwanadi wagombea wa chama chao katika jambo hayo yote, ukuwadi huo pia ulifanywa na viongozi wa Chadema akiwemo Mbowe na Dk. Slaa maana pia walikuwa Igunga na Uzini wakifanya kampeni.

  Mbona hasemi kwamba nao walikwenda huko kuisaidia CCM ili ishinde dhidi ya wagombea waliosimamishwa na CUF kama siyo wendawazimu wa kufikiri?

  Inawezekana Mwigamba amevamia siasa ukubwani huku akidhani kuwa ni ugomvi, na pia huenda akawa limbukeni wa madaraka aliyonayo akiwa Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa.

  Ni ujinga kusema viongozi wa CUF wanapokwenda kuwanadi wagombea ubunge, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar au nafasi za udiwani wanatumiwa na CCM, lakini wanachofanya ni kilekile kinachofanywa na viongozi wa Chadema wakati uleule na sehemu ileile!

  Akihutubia taifa kwa njia ya redio Januari, 1979 kuhusu Vita vya Kagera, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wakati huo), Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alimshangaa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar al Qadaffi.

  Mwalimu alisema wakati vikosi vya Tanzania vinapambana na majeshi ya serikali ya aliyekuwa Kiongozi wa Kijeshi wa Uganda, Field Marshal Idi Amina katika ardhi ya nchi hii, Qadaffi alikuwa akifahamu kila jambo, lakini hakusema lolote wala kufanya chochote.

  Lakini pale majeshi ya Amin yalipopigwa na vita hivyo kuingia katika ardhi ya Uganda, Qadaffi alimtuma balozi wake hapa nchini, kumuomba Mwalimu aviondoe vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ndani ya nchi hiyo ambayo sasa inaongozwa na Luteni Jenerali Yoweri Kaguta Museveni.

  Pamoja na kuwasilisha ombi hilo, Qadaffi alikwenda mbali zaidi akimtishia Mwalimu kuwa kama angekataa kuviondoa vikosi vyake katika ardhi ya Uganda, nchi yake nayo ingeingiza jeshi lake kwenda kuyasaidia majeshi ya Amin.

  “Nilimwambia balozi yule akamwambie Qadaffi kwamba vita vinavyopiganwa sasa katika ardhi ya Uganda ndiyo vilevile vilivyokuwa vinapiganwa katika ardhi ya Tanzania”, alisema Mwalimu na kuongeza:

  “Kama vita vile vilikuwa halali wakati vinapiganwa katika ardhi ya Tanzania haviwezi kugeuka na kuwa haramu wakati vinapiganwa katika ardhi ya Uganda. Ni vita vilevile”.

  Nimetumia mfano huo kuonyesha ujinga wa kufikiri walionao baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema, wale wanaodhani kuwa ni halali chama chao kushiriki chaguzi za uwakilishi wa wananchi katika vyombo vya dola, lakini ni haramu kwa CUF na TLP kufanya hivyo wakati pia vimesajiliwa kwa sheria ileile ya vyama vya siasa nchini, katiba ileile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kanuni zilezile zilizopo.

  Kuhusu madai kwamba Nape na wajumbe wenzake wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyoteuliwa Aprili 11, mwaka jana, walipita katika mikoa yote ya Tanzania isipokuwa Arusha pekee pia ni uzushi, uongo na uzandiki uliopitiliza mpaka miguuni.

  Ni ujinga wa aina yake kiongozi wa kisiasa kutaka kudanganya hata kwa jambo linalohitaji kuliona kwa macho, lakini anataka kuwafanya watu wote ni vipofu “tititi” isipokuwa yeye peke yake.

  Nape na wajumbe wenzake wa Sekretarieti ya Taifa ya CCM hawakwenda mikoa yote 26 ya Tanzania kama anavyodai Mwigamba ila walifanya hivyo kwa mikoa mitatu tu.

  Walianzia Dodoma kwa kutambulishwa kwenye Uwanja wa Nyerere Square uliopo mjini humo, kisha wakaenda Dar es Salaam walikotambulishwa kwenye Viwanja vya Bakhresa, Manzese wilayani Kinondoni.

  Hata hivyo, safari ya kuelekea Dar es Salaam iliwapitisha pia Morogoro na kisha Chalinze katika mkoa wa Pwani, kule ambako walikuta maelfu ya wananchi wakiwasubiri ili angalau wawasalimie peke yake, ukweli ambao Mwigamba angependa aupotoshe kwa nguvu zake zote.
  [/FONT] [FONT=&amp]Mbali na Dodoma na Dar es Salaam, ziara hiyo ya kutambulishwa pia ilifanyika katika mkoa wa Mjini Magharibi huko Zanzibar na huo ndio ukawa mwisho wa zoezi hilo.

  Walitambulishwa katika mikoa hiyo mitatu kwa sababu tatu peke yake. Kwanza walianzia Dodoma kwa vile ndipo yalipo Makao Makuu ya CCM, pili wakaenda jijini Dar es Salaam ambako kuna Ofisi Ndogo ya Makao Makuu pale Lumumba na tatu, ziara yao iliishia mkoa wa Mjini Magharibi kwa sababu hapo ndipo ilipo Afisa Kuu ya Chama hicho kwa Zanzibar.

  Ilikuwa ni lazima wakaonyeshwe ofisi zao kila baada ya kupewa mapokezi ya halaiki kutoka kwa wananchi na kuwahutubia angalau kwa dakika chache tu.

  Katika hali hiyo, hakuna ziara hata moja ya pamoja waliyofanya katika mikoa ya Arusha, Manyara, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Mtwara, Morogoro, Iringa, Lindi, Pwani, Tanga, Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja au Kilimanjaro.

  Viongozi wa CCM hawarundikani kwenye ziara moja kiasi cha kufunga hadi ofisi kama wa Chadema, jambo ambalo Mwigamba akiwa Mwenyekiti wa Mkoa analifahamu.

  Anajua kuwa ziara za Chadema huwakusanya pamoja Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Wenyeviti wake wote, Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu wote, Wakurugenzi wa Taifa wa Idara zote za Makao Makuu, wabunge wote wa kuchaguliwa kwenye majimbo, wabunge wote wa Viti Maalum na watendaji wote waandamizi wa taifa na kila mkoa wanaokwenda.

  Wanalazimika kufanya hivyo kwa sababu akienda mmoja peke yake hawezi kupata watu mkutanoni na maandamano yake yanaweza kuwa ya vibaka tu.

  Inabidi wafuatane kwa sababu kuna watu hujitokeza kuandamana au kwenda mkutanoni ili pengine kuiona sura ya “Ze Komedi” kama Dk. Slaa, Mwenyekiti wa Taifa “aliyemezwa”

  na Katibu Mkuu wake, Freeman Mbowe au Tundu Lissu, mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuwachonganisha wananchi na serikali yao.

  Kila mmoja husubiri mtu wake asimame na kusalimia au kuzungumza hata kama msema ovyo na akimaliza tu unaona wengine wanaondoka, jambo lililowahi kumtokea Mbowe kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mlandege iliyopo Iringa mjini, mwaka jana.

  Nasema tena ni ujinga kutumia jina la Nape kutengenezea uongo, tatizo linalokuwa kubwa maradufu linapofanywa kwa makusudi hasa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama chochote kile cha siasa!

  Upeo mwingine finyu wa masuala ya kisiasa aliouonyesha Mwigamba ni kudai Chadema “haikamatiki” kwa mkoa wa Arusha, neno ambalo kwa tafsiri ya kawaida maana yake ni “kutowezekana”.

  Mkoa wa Arusha una majimbo saba ya uchaguzi ambayo ni Arumeru Magharibi, Arumeru Mashariki, Arusha Mjini, Karatu, Longido, Monduli na Ngorongoro.

  Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, CCM ilinyakua majimbo matano ya Arumeru Magharibi, Arumeru Mashariki, Longido, Monduli na Ngorongoro huku Chadema ikishinda mawili ambayo ni Arusha Mjini na Karatu.

  Kama Chadema ingekuwa “haikamatiki” katika mkoa huo ingeshinda yote na siyo mawili peke yake, vinginevyo ingepata angalau sita na kushindwa moja tena kwa taabu, hivyo kutamba kwa Mwigamba inaonyesha jinsi gani alivyokosa hata aibu ya kufikiri kichwani.

  Anajishaua akidhani watu hawaelewi au akili zao haziko timamu, hivyo kwa muda wote na mahali popote zinasubiri kuhubiriwa uongo na viongozi wa Chadema kama yeye.
  [/FONT] [FONT=&amp]Pamoja na uzushi wote alionao, lakini inawezekana akisema chama hicho “hakikamatiki” katika mkoa wa Arusha anamaanisha kuwa hakiwezekani kwa uchochezi, vitisho, vurugu, ghasia, majungu, uongo, uzandiki, inda, chuki, uzabina, umbeya na sema kingine chochote unachojua kuhusu uharamia na ugaidi mkubwa kabisa wa kisiasa duniani. [/FONT] [FONT=&amp]Mungu Ibariki Tanzania! [/FONT]
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hawana hoja na sera kilichobaki ni kutumia matatizo ya watanzania kujinufaisha kisiasa.arumeru kama igunga na uzini
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ww kaa apo kwenye komputa subiri uletewe matokeo.wanaume wapo kazini.
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mpira ni dk90 na uwanja wenyewe ndiyo huu. wewe ndiyo unaweweseka
   
 19. A

  Awo JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Charles Charles ndio magamba gani tena? Ya nyoka au kobe? Maana daaa!
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Halafu huyo Nape Nnauye anathubutu kudai kuwa JF ni ya Chadema!
   
Loading...