Kufa kufaana,mkuu!Habari Wanajamii
Nimetokea Kikatiti Leo Asubuhi Mida Ya Saa Tatu Hivi Kuelekea Tengeru, Katika Kila Kituo Cha Daladala Na Penye Maduka Au Soko Kumepandishwa Bendera Za CCM Tena Mpya Kabisa, Kufika Usa River Nawakuta Watu Wanazidi Kuzipandisha.
Swali. Je Ndio Kampeni Zimeanza? Na Kama Sio, Je Ni Kwanini Zipandishwe Leo? Mwenye Kujua Anijuze.
Rest In Peace J. Sumari Mbunge
Na pia kuwaaminisha kuwa CCM inapendwa na wananchi wa Arusha wakati si kweli.kesho kuna ugeni wa chama na serikali kwa ajili ya mazishi.hapo lazima kuna shinikizo la R.C ili aonekane mchapa kazi.
We ndg yangu acha tu zingepandishwa za CHADEMA pasingetosha wapandishe hd kwenye migomba jimbo liko CHADEMA Tena nawashauri wasijusumbue ku2mia bilion 3 kama Igunga, Arumeru watu niwasomi hawadanganyiki NAWASILISHA
Cha Ajabu hazipepei nusu mlingoti
kesho kuna ugeni wa chama na serikali kwa ajili ya mazishi.hapo lazima kuna shinikizo la R.C ili aonekane mchapa kazi.
sasa mtu kabadndika dirishani kwake hapo ita kaaje nusu mlingoti.embu jaribu kuwauliza kwanini wameweka hizo bendera.Je wameweka kwa utashi wao au kuna watu walipita na kuweka wao wakanywa pebusi.
Una uhakika na uyasemayo? Ulikuwepo RC aliposhinikiza? Wewe utakuwa ni mmoja wa wale wanaokufa na kufikia kuzikwa midomo ikiwa wazi. Uzushi haupendezi na wala Mola hapendi. Chinga sana!