Mtade_Halisi
Member
- Feb 23, 2008
- 28
- 0
Hello wadau wa soka, The gunners mpaka sasa dakika ya 78 wanaongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya Birmigham city. Hadi Kipindi cha kwanza Arsenal walikuwa wamelala kwa bao moja lililopachikwa kimiani na mshambuliaji J. McFadden dk. ya 28 pia katika kipindi hicho cha kwanza mshambuliaji machachari wa Arsenal alifanyiwa rafu mbaya iliyopelekea kuvunjika mguu na kutolea kadi nyekundu kwa beki Martin Tylor. Mabao yote mawili ya Arsenal yamepachikwa na mchambuliaji mwenye mbio na chenga za maudhi bwamdogo Theo Walcott mwanzoni mwa kipindi cha pili. Kuna kila dalili Arsenal wakaibuka na ushindi kama kumbukumbu ya shujaa aliyeumia Eduardo ambaye jumatatu ijayo ni siku yake ya kuzaliwa. Go GUNNERS....Kazi kwenu ManU, maana Newcastle wamepania kweli...