Baada ya kipigo kutoka kwa Man City cha goli 3-0, Wengere awataka Arsenal kuwa na umoja

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Klabu ya Manchester City imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3 – 0 dhidi ya Arsenal mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliyopigwa katika dimba la Emirates.

City inafanikiwa kuchomoza na ushindi huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya wiki iliyopita kushuhudiwa timu hiyo ikinyakuwa kombe la Karabao Cup kwa ushindi kama huo mbele ya the Gunners.

Baada ya matokeo hayo meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa wachezaji wake walikosa kujiamini na ndiypo sababu ya kupoteza mchezo huo na kuwataka kuwa na umoja na kufikiria mchezo ujao.

Wenger alisema;

"Wakati imani yako inapokuwa ndogo cha kwanza kinachotokea kukosa kujiamini na nguvu kupungua na hicho ndicho kilichotokea katika mchezo."

"Nadhani umeweza kuona usiku wa leo, sidharau ubora waliyokuwa nao City lahasha lakini tunapitia katika kipindi kigumu ndani ya uwanja."

"Hii ni sehemu ya mchezo nilazima tuunganishe nguvu zetu na tuwe kitu kimoja ndani ya timu na tufikirie mchezo ujao na tuweke juhudi zetu huko."

ar.jpg

ars.jpg

arsn.jpg
 
Kuna shabiki mmoja wa Arsenal simuoni.... sijui kama hajajinyonga lakini.

Maneno mingiiii... Timu za london zote miwa.... EPL imekuwa ya kaskazini sasa.
 
Huyu muzee anasikitisha mno. By the way ang'atuke tu...au anataka yamkute ya Mugabe!
 
Huyu mzee atang'atuka tu. Kwa sababu malengo ya mmiliki yanaanza kupotea, nayo ni nafasi ya champions leagued kupata kushiriki. Arsenal hajawahi kushindania kombe, kwenye priorities anazopewa wenger anaambiwa top 4 finish inatosha. Utaona mzee anatolewa kwenye team kwa sababu ya kutokuwepo top 4. Lakini kama angekuwa anaingia top 4 huyu mzee asingeng'atuka hadi astaafu mwenyewe.
 
Hahahahaa it's true kamanda
 
Acha uongo.
main aim ya arsenal ni kwenda UCL!! hata leicester wanatarget EPL, sasa iweje sio kwa arsenal?
 
Mkuu unakuwa unasoma vizuri kabla ya kureply post lakini? hebu isome vizuri hio post yangu uloquote halafu tizama utumbo uloandika. Aliekwambia Leceister ana target ya EPL title nani? :D :D :D basi hata middlesborough ana target ya EPL.

Lazima ujue kila timu inaweka priority nini, hizi priorities ndio zinafukuzisha makocha.

Mfano, timu kama Man utd baada ya kuondoka Fergie, board members walijua kwa asilimia 100% hawawezi kuchukua EPL title na hasa kwa manager kama moyes, kwaio kwao haikuwa priority.
 
Usidanganye, Team kubwa kama arsenal haiwezi kukosa priority ya kutwaa epl.sema mambo hayaendi upande wao
 
Hawana priority ya kuchukua EPL Arsene wenger ndio maana miaka kumi na kuendelea hajatwaa huo ubingwa na bado yupo. Priorirty yao ni kuwa top 4 na kuingia UEFA kitu ambacho ndio kilikuwa kina mpa uhakika wa kuendelea na Arsenal. EPL ni kama Bonus tu kwao. Hujui ata nini kinaendelea kwenye board, sasa ivi washabiki wanataka Wenger na Kroenke wasepe, kwa sababu Club goals imekuwa sio kushinda titles as it used to be.

Utakuja kunambia mwenyewe hapa Arsene Wenger atakpoachishwa kiti chake. Halafu utajiuliza, Miaka 10 hatoki top 4, ila miaka miwili au mitatu hayumo top 4 halafu kafukuzwa?

Wewe unaiona timu kubwa, imebakia jina tu. Wanabodi wanajua kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.

Huwezi kumwambia fundi akujengee nyumba ya vyumba sita kwa mifuko miwili ya saruji! hichi ndicho kilichotokea Arsenal, Kroenke anajua kwa asilimia 100 kuwa Arsenal haina uwezo wa kuchukua kombe la EPL na UCL, tena iweje ampe hizo priority? Hapa tunaongea uhalisia hatuongei eti timu kubwa, tena ukubwa wenyewe umebaki jina tu. Hata Stoke city anataka achukue EPL.

Benitez, amechukua UCL, ni kocha mzuri na anajulikana vyema, saivi yuko Newcastle, ivi unataka kunambia priority alopewa ni kuwa achukue EPL? Priority alopewa Benitez ni kuiondoa Newcastle kwenye relegation Zone tu. Huu ni mfano tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom