Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nilikua naangalia press conference ya Ange baada ya mechi jamaa anaonekana amekasirika vibaya mno. Anaongelea juu ya misingi ndani ya timu kua legelege akaulizwa hilo swala kaona nje ya timu au ndani ya timu akajibu kote.

This means Ange focus yake ni ushindi ila timu haina huo utamaduni, kwao mafanikio ya msimu ni kumaliza juu ya Arsenal au Arsenal asipochukua ubingwa. Makocha wawili waliopita Jose na Conte wote waliongelea hilo swala kwamba "Timu haina winning mentality"

Conte alienda mbali akasema labda hii ni historia ya Tottenham. Lakini hili swala la misingi Jose alilisema akiwa na nyumbu pia, mwingine aliyeongelea misingi ya nyumbu ni Zlatan, Pogba na Cristiano.

Kama Bongo, mafanikio ya Simba ni Yanga asishinde kitu bila kujali kama yeye hatoshinda pia and vice versa. Conte alifukuzwa kwa hili alilofanya Ange, so tusubiri kuona ikiwa Tottenham wataona aibu na kujirudi au watamfungashia virago Ange.

Loser mentality zipo kwa midtable teams mara nyingi, atafurahia kusuluhu au usipomfunga magoli mengi. Wewe upo ulimwengu mwingine kabisa yeye yupo busy kufuatilia unacheza na nani next game. Atatoa ubashiri pale, haitakua anavyotaka. Atakunywa K Vant kutuliza hasira, atajichua kidogo. Kisha anarudi tena kuleta ubashiri mpya au kuandika utumbo mpya.

Lolote litakalomjia kichwani muda huo.
 
Laana Fc, Hii Arsenyau hata ikimchukua Guardiola bado itaendelea kuzisindikiza timu nyingine kuchukua makombe.
Hawa wachezaji wafuatao baada ya kujua Arsenyau ni Gundu Fc wakaamua kuwakimbia na kwenda kubeba makombe ya maana kwenye timu zinazojielewa
 
Hiyo para ya pili toka mwisho daah...
 
Mkorea baada ya kuaminishwa ujinga na boss wake Masingeli nae akaubebelea vilevile kama ulivyo na kuanza kuwalisha Kima wenzie matango pori

Sijui mkorea anajisikiaje sasa hivi baada ya motivational speaker kumkimbia na kumuachia msalaba wake aubebe mwenyewe.
Masingeli msimu uliopita aliwakimbia mkabakia kuchezea spana peke yenu, na msimu huu kala kona tena lakini hamjifunzi kitu

Ngoja tuanze kufukua makaburi.
 

Projects za Timu zetu zisizotumia oil money ni ngumu sana kuwa Complete kwasababu ukiwa katika hatua ya kukarabati upande mmoja basi Mwengine unabomoka, ukienda kukarabati uliobomoka mpaka ukifanikiwa basi utakuta huu uliojenga mwanzo nao unaanza kutoboka.
Cycle inaenda hivyo mpaka unapotomoka kabisa.

Mcheki Klop:
- Alikarabati Forward kwanza (Man + Salah)
Mido na Mabeki akaacha.
- Akakarabati Mido (Kamleta Chamberlain) ikakubali.
Mabeki kaacha.
- Akaanza kukarabati Mabeki (Gomez + VVD + Kipa).
Ghafla Mido ikabomoka kwa kuumia Chamberlain na Henderson kushuka kiwango.

- Akaamua kuirudia Mido kwa kumleta Fabinho/Keita.
Ghafla Beki ikabomoka kwa kuumia Gomez na mpaka leo haijakaa sawa.

- Akiwa anapambana kukarabati Beki iliyobomoka basi ghafla Forward ikabomoka kwa kuondoka (Mane na Firmino kuzeeka).

- Akaachana na Beki akaenda kukarabati Forward (Nunez + Gakpo + Diaz) lakini hakufanikiwa.
Ghafla Mido ikabomoka.

- Akasema wacha akarabati Mido (MacAllister + Wataru + Szobo).
Lakini Mabeki + Forward wameoza.


Hiyo ndiyo Cycle ya Timu zetu ndugu usitegemee kumaliza hizo unazoziita Phase ukiwa kamili kama huna oil money au pesa za kihuni kama za Abramovic.

City alikuwa na Aguero, akaleta Jesus kuziba nafasi ya Aguero, Jesus hakufit akaleta Haaland.
Anarekebisha kila sehemu kwa wakati mmoja.
 
Kwa sasa arsenal tunahitaji wachezaji walio bora, mchezaji ambae anaweza ingia kwenye kikosi chochote duniani..
Saliba,ben white, partey, odeergad.. wanahitajika wengine wenye ubora mkubwa saana.

Mpaka kufikia hapa ubora wa mbinu za mwalimu ndio umetufikisha hapa, tunahitaji wachezaji bora zaidi, kuwa bora zaidi.
 
Kaka nina ombi moja kwako! Naomba uniwekee na Picha za Alex-Oxlade Chamberlain baada ya kuondoka Arsenal.

Natanguliza Shukurani
Broo nisamehe sana sijui nilighafilika nini mpaka nikasahau kumuweka dogo janja Chamberlain kwenye orodha.
Nina imani hata kesho kina Sakatonge na Ordegard wakiamua kuondoka kwenye hio Academy wanaenda kubeba makombe makubwa.
RVP mpaka kesho akihojiwa hua analaani kwelikweli kupoteza miaka 11 ya career yake kwa kuchezea Gundu Fc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…