Uchambuzi
George Ambangile
London is RED
Kwa dakika zote 95 Arsenal walikuwa timu bora uwanjani , hasa kabla ya kadi nyekundu ya Lamela . Arsenal walitawala sana mchezo, walikuwa fresh sana, wapo fast, walipasiana mpira vizuri, walipress kwa umakini sana , wachezaji wengi sana walikuwa kwenye kiwango kizuri uwanjani
Jose Mourinho ni moja ya kocha bora kabisa Duniani katika kipindi cha miaka 20 linapokuja suala la mbinu. Kitu alichonishangaza leo kwa kipindi kirefu cha mechi hakuona tatizo upande wake wa kulia na kushoto wa Arsenal. ESR na Kieran Tierney walimuadhibu sana Doherty , muda mrefu alikuwa anapamba ( 2 Vs 1 ) na mashambulizi mengi yalikuwa upande ule . Hata goli la Martin Odegaard limetokea upande ule kwa kumuacha Doherty hajui aanze kwa ESR au Tierney . Ilikuwa either Bale arudi nyuma kumsaidia au Moura ahamie upande wa kulia kwasababu ni mzuri kwenye kuzuia .
Odegaard, Xhaka na Partey kabla ya kadi nyekundu walimeza sana kiungo . Walitengeza pembe tatu. Martin muda wote yupo nyuma ya HΓΈjbjerg na Ndombele wakati Xhaka na Partey mbele ya viungo wa Spurs . Matokeo yake hakukuwa na mipira mingi kwenda kwa Kane, Lamela, Lucas au Bale . Lakini mbinu bora ilikuwa Arsenal wakianzia nyuma , Xhaka anakuwa kama beki wa kushoto, Tierney anasogea juu na ESR , anachagua kuingia ndani nyuma ya HΓΈjbjerg au kukimbia katikati ya Sanchez na Doherty . BRILLIANT
Nafikiri mchezaji bora wa Spurs alikuwa Lucas Moura aliwapa Arsenal matatizo yote kwa kasi yake, ufundi na mpira mguuni , na hali ya kutokata tamaa , alilazimisha vitu vitokee . Kati ya wachezaji wenye bahati uwanjani leo basi ni Leno. Sielewi kwenye mpira wa adhabu wa Kane alikuwa anaenda wapi . Amepanga ukuta wake kulia kwake , tena kuna mchezaji amelala chini ya ukuta , Kane wakati anaenda kupiga Leno akaanza kuhamia kule alipopanga ukuta, bahati yake mpira uligonga mwamba.