Usajili news:
Wakuu habari za mkesha wa xmas na natumai kila alie mkristo atamkaribisha mtoto Yesu ambae ndo kwanza ana siku moja tangu amezaliwa huko Bethlehemu.
Ilikuwa ni baada ya wazazi wake Bi Mariam na bwana Joseph kutembea umbali mrefu kutoka Nazareti wakitafuta hifadhi ya kumpokea mtoto Yesu.
Sasa tukisherehekea sikukuu hii ya mwisho wa mwaka siku inayofuata wana Gunners tutakuwa tukiiangalia Arsenal ilozaliwa upya baada ya kumkaribisha kocha mkuu mpya bwana Mikael Arteta.
Arteta amekwishatoa mwongozo kwa wachezaji kwamba anataka wachezee vipi timu yetu hii ambayo ni moja ya timu kubwa 9 duniani, na hii ni kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Pia Arsenal ni timu ya tano duniani kwa kuwa na washabiki wengi na Forbes imeiweka Arsenal kuwa klabu ya tatu kwa kuwa na thamani kubwa nchini Uingereza kwa kuwa na thamani ya kiasi cha dola za marekani bilioni 2.24
Arteta ameitaka bodi ya Arsenal isajili mabeki wawili na mchezaji mmoja wa kiungo.
Kwa kawaida inachukuliwa kuwa Januari ni msimu wa usajili ambao ni wa kimbinu au "tactical transfer" na ule wa wakakti wa kiangazi au Summer ni usajiki wa kimkakati yaani "strategic transfer".
Hivyo basi ikiwa kuna timu itamweka mezani dau lolote kwa Xhaka basi Winfried Ndidi wa Lecester atasajiliwa na Arsenal mwezi ujao.
Ndidi ni mlinzi wa kati ambae anaweza kuja kusaidia sehemu ya kiungo lakini Leicester wanaweza kuweka ugumu.
Upamecano atagharimu kiasi cha pauni milioni 70 na Arsenal hawawezi kufanya usajili huo ingawa kwa kuwa kumwita Willima Saliba kutashindikana kutokana na Saliba kuwa majeruhi, basi Dayot Upamecano anaweza kusajiliwa wakati wa kiangazi ambapo Sokratis na Davil Luiz wataondoka.
Hivyo basi, mechi ya Boxing day na Bournemouth tutegemee Arsenal ileile ilocheza na Everton au ilobadilishwa kidogo ambapo Lucas Torreira anaweza kuendelea kushirikiana na Granit Xhaka katikati, huku nyuma wakiwepo kipa Leno, Maitland Niles kulia na Bukayo Saka akicheza kama cover kwa Kolasinac na Tierney.
Mbele pembeni kutakuwa na Nicolas Pepe kulia , Mesut Ozil kati ndani , Aubameyang kushoito na Lacazette katikati.
Kheri ya Christmas.