Mdudu Nzi anachungulia kwa mbali huku akiruka huku na kule kuzengea mzoga. Mdudu hakuna mzoga leo wafikishie ujumbe huu na #Mburukenge wote wa jukwaa hili mwanana.
FT Sunderland 0-2 Arsenal
Point tatu muhimu kibindoni
Dua zako hazinipati kamweeeee wewe kesho yako macho na masikio tu.........
Mie nawaombea mema mtoe draw ya 0-0 ambayo kwenu ni ushindi mkubwa hutaki! πππ haya unaijua speed ya Chelsea kesho wakiwachapa 3-0 kibarua cha Van Girl ndio kitaota rasmi nyasi sijui mtarudi kwa SAF?
Asante kwa dua zako niombee tu nishinde mbona unakuwa mgumu kulisema hili???Yaani kesho mtashangaa sipendi kujinadi sana,maajabu ya tembo kuangushwa na sisimizi,Tchao........
Mshinde halafu muwe juu yetu kwa 2 points? Ni bora tu mtoe draw ili msiwe mbali sana lol!!!! ikifika wakati muafaka tuwaage rasmi na kuwatimulia vumbi. Sare inawatosha kabisa ni sawa na ushindi mkubwa kwenu ππ
Hahaha!!!! Utasubiri sanaaaaaaa!!!!!! Kesho Chelsea akipigwa mjue tu ndoo ni yetu. Niombee heri tu acha wivu bana!!!!!!
Hahahahaha lol!!!! Si vibaya kujipa matumaini ati!!! na uje hapa jukwaani badala ya kujificha na kusepa kimya kimya mkishatundikwa goli za kutosha. Mie nakuombea kila la heri ila nakuomba usininunie. ππ
Hanuni mtu hapa hata tupigwe week(7)!!! Kesho nipo sana ila game sitaona ntakuwa safarini ntakuwepo kugonga like.
Ahsante kwa kuamua kutonuna lol!!! Uende salama na ujue kesho nitawashangalia kiaina aina lol! ili mtoe draw ya 0-0 msituangushe katika kuwapunguzia speed hawa Chelsea.