- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Ni magonjwa ya mfumo was upumuaji yamekatisha uhai wake akiwa na Miaka 41 tu.
Bavarians Msiba huu usiwapite na wale wenzangu wa PES ( pro evolution soceer ).
Winger teleza ameenda.
Pumzika kwa amani mkongwe.
Soka halikudai.
Bavarians Msiba huu usiwapite na wale wenzangu wa PES ( pro evolution soceer ).
Winger teleza ameenda.
Pumzika kwa amani mkongwe.
Soka halikudai.
- Tunachokijua
- Arjen Robben ni mchezaji wa mpira wa miguu Raia wa Uholanzi ambaye amewahi kutumikia vilabu vya Chelsea, Real Madrid, Bayern Munich. Alistaafu kucheza soka mnamo mwezi Julai 15, 2021
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa Robben amefariki, taarifa hiyo ikisema “Aliyekuwa winga wa Uholanzi na Bayern Munich, Arjen Robben, amefariki dunia kufuatia matatizo yaliyochangiwa na maradhi sugu ya mfumo wa upumuaji baada ya miaka ya kupambana na changamoto za kiafya, familia yake imetangaza kupitia ujumbe wa kusikitisha uliouacha ulimwengu wa soka katika mshangao.”
Ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichoripoti taarifa hiyo.
Septemba 13, 2025 wawakilishi wa mchezaji wa mpira wa miguu Arjen Robben walithibitisha rasmi kwamba hajafariki. “Amejiunga na orodha ndefu ya watu maarufu waliowahi kuwa wahanga wa taarifa za uongo. Bado yuko hai na anaendelea vizuri, acheni kuamini kila kitu mnachoona mtandaoni,” walisema.
Baadhi ya mashabiki wameonyesha hasira zao kwa taarifa hiyo ya uongo wakisema ilikuwa ni ya kizembe, ya kusikitisha na yenye kuumiza hisia za mashabiki wa mchezaji huyo anayependwa sana. Wengine wanasema hili linaonyesha umaarufu wake mkubwa duniani kote.