shumbimadelu
Senior Member
- Jan 8, 2013
- 185
- 64
- Thread starter
- #61
Mambo mengine tuweke ushabiki nyuma na tuwe tayari kuongea na kusimamia ukweli. Mimi ni mwana chama hai wa CHADEMA. Mara ya kwanza nilipotoka chuoni, mwezi Juni mwaka jana nilikuta mji umebadirika kabisa. Zile bendera nzuri za CHADEMA ambazo zilikuwa zinaupendezesha mji, hazikuonekana tena. Maeneo mengi ambayo kulikuwa na Bendera za CHADEMA, nafasi yake ilikuwa imechukuliwa na bendera za ccm. Nilishangaa sana, na ikabidi niwaulize wenyeji niliowakuta. Jibu ambalo lilipata kutoka kwa wengi, walisema, bendera siyo issue, issue in mioyo ya watu, watu wako CHADEMA japo mashina yao yamewekwa bendera za ccm! Ilinichukua muda mrefu kidogo kuamini.
Najua wengi tunapenda kusikia mazuri tu kutoka CHADEMA, hata mimi ni mmoja wao, lakini kwenye ukweli lazima tuseme. Kama sijakosea, Said Arf alishinda kwa tofauti ya kura 47 katika uchaguzi uliopita, tofauti sana na uchaguzi wa 2005 ambapo alipata kura nyingi sana. Hili pekee linaonesha kukubalika kwake kumepungua sana. Japo anafanya kazi nzuri, lakini mvuto wake umepungua kwa wananchi na nafikiri ameshindwa kuwa na techniques za kuwavuta watu na kukubali sera za chama. Tusifarijiane, huyu Mzee atakiacha chama cha CHADEMA katika hali mbaya sana. Na anaposema kuwa haogombei tena, siyo kwamba hapendi, lakini ameshaupima upepo na ameona kuwa kukubalika kwake kunashuka kwa nguvu sana hapa Mpanda mjini na hivyo anataka amuachie mwingine aibu ya kushindwa ili yeye ajisifu kuwa ndiye alikuwa anaibeba CHADEMA MPANDA MJINI.
Tusibishane, ukweli daima utasimama, mimi binafsi nilisikitishwa sana na huyu Mzee kutupa kadi ya chama, eti kwa sababu alikasirishwa na vijana. Ina maana siyo mvumilivu kiasi hicho? Kuitupa kadi ya chama ni kukidhalilisha chama. Nilisikitika sana, na hata leo hii siamini kama kweli alifanya kitendo kile.
Hili suala la chama kukosa ofisi ya maana hapa Mpanda Mjini, nilizungumzwa sana, japo kwenye mikutano ya siasa tunafarijiana na kupeana moyo kuwa tuna mkakati wa kujenga ofisi kubwa ya mkoa. Lakini hiyo itachukua muda sana, kwa nini tusiwe na ofisi at least yenye hadhi kwa sasa wakati tunashughulikia hiyo ya mKoa? Huyu Mzee kweli amefanya mengi, lakini nafikiri kuwa atamaliza vibaya sana ubunge wake hapa Mpanda Mjini.
Kuna hii case ya gari la AMBULANCE kukaa nyumbani kwa mbunge. Mimi bado sijajua, ila nilisikia tetesi kuwa hizi gari zilitolewa na CHADEMA MAKAO MAKUU kwa kila jimbo ambalo lilikuwa na mbunge wa CHADEMA, na kwamba kwa mujibu wa maelekezo ya CHADEMA MAKAO MAKUU, ilitakiwa hizi gari zikabidhiwe kwa uongozi wa hospitali za mkoa au wilaya. Nasikia Ndesambulo na wengine walizikabidhi gari hizo kwa serikali kupitia uongozi wa hospitali husika, huku kwetu gari linakaa kwa mbunge. Mimi hofu yangu, jamaa anaweza akafuta yale maandishi "MBUNGE MPANDA MJINI CHADEMA" kama hatogombea tena uchaguzi ujao, na kama atagombea mwingine akashindwa, je itaendelea kuwa ambulance?
Lisemwalo lipo, kama halipo linakuja. Nafikiri tunahitaji kuwa na kikao cha vijana mkoa wa Katavi kwa ajili ya kujadili mustakabali wa chama hapa mkoani, vinginevyo, tutarudi nyuma ambako binafsi sipendi. Ni hayo tu!!!!
Huo ndio ukweli ila hawataki tuseme ukweli eti ukisema unitwa gamba.Hawa wenzetu wanaupofu sijui limbwata la Josephina linatudhuru wote?Wanani criticise bila point hawajibu hoja na kusema kama mi naongea majungu na uongo.Je ukweli upo wapi?bora wewe umeliona hili.