Arfi anaiua CHADEMA wilayani Mpanda

Arfi anaiua CHADEMA wilayani Mpanda

shumbimadelu

Senior Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
185
Reaction score
64
Ndugu wanajamvi,huyu jamaa ambae ni makamu mwenyeketi wa CHADEMA taifa na ni mbunge wa Mpanda kati au mpanda mjini ila huyu hana alilofanya hapa jimboni kwake.Tangu awe mbunge, vijana wengi wamekihama chama,mashina mengi ya CHADEMA hapa mjini yamevunja na kuwekwa bendera za CCM pia jamaa anaendeleza makundi na majungu na hataki kuambiwa ukweli na ndio maana alitupa kadi ya chama alipoulizwa na vijana juu ya maendeleo ya chama.

Mbunge anahusishwa kutumiwa na mheshimiwa PINDA kuiua CHADEMA hapa Mpanda eti sababu yeye hagombei tena ubunge.Cha maana alichofanya mpaka sasa ni kumlipia mzee mmoja aliyempigia kampeni chakula kwa msomali mmoja panaitwa madini cafetaria na anamlipia kwa mwezi.

Sasa ni mwezi wa tatu sasa ofisi ya CHADEMA hapa MPANDA MJINI imefungwa sababu wameshindwa lipa kodi ya pango.Haonekani ofisini kwake na ofisi yake inatia aibu kwa kujaa maji katika kipindi hiki cha mvua mkoani humu. Najitahidi kuapload picha kuonesha ofisi ya mbunge ilivyojaa maji na yaliyokuwa mashina ya CHADEMA ambayo sasa yamewekwa bendera za CCM lakini inashindikana.
 
Vijana ndio wanye matatizo wala siyo Arfi.Wakiwa wanaipenda CHADEMA watafanya mikakati yao kama vijana ili kuiinua CHADEMA na kujiunga CCM kuna nipa wasiwasi kuwa walikuwa wachumia tumbo na wala hawana mapendi na chama chao.Hutakiwi kukimbia vita bali kutafuta suluhisho ili ushinde.Poleni Mpanda
 
Chadema kina sifa ya kufanya maamuzi magumu mfukuzeni haraka.
 
Mwanachama mwenye uadilifu na chama chake matatizo kama haya anayapeleka kunakohusika sio hapa kila mtu aone ndio nini? Ndio umetatua tatizo?

Ndio maana watu kama nyie tunawaona gamba tu...
 
Ndugu wanajamvi,huyu jamaa ambae ni makamu mwenyeketi wa chadema taifa na ni mbunge wa mpanda kati au mpanda mjini ila huyu hana alilofanya hapa jimboni kwake.Tangu awe mbunge, vijana wengi wamekihama chama,mashina mengi ya chadema hapa mjini yamevunja na kuwekwa bendera za ccm pia jamaa anaendeleza makundi na majungu na hataki kuambiwa ukweli na ndio maana alitupa kadi ya chama alipoulizwa na vijana juu ya maendeleo ya chama.Mbunge anahusishwa kutumiwa na mheshimiwa PINDA kuiua chadema hapa mpanda eti sababu yeye hagombei tena ubunge.Cha maana alichofanya mpaka sasa ni kumlipia mzee mmoja aliyempigia kampeni chakula kwa msomali mmoja panaitwa madini cafetaria na anamlipia kwa mwezi.Sasa ni mwezi wa tatu sasa ofisi ya chadema hapa MPANDA MJINI imefungwa sababu wameshindwa lipa kodi ya pango.Haonekani ofisini kwake na ofisi yake inatia aibu kwa kujaa maji katika kipindi hiki cha mvua mkoani humu. Najitahidi kuapload picha kuonesha ofisi ya mbunge ilivyojaa maji na yaliyokuwa mashina ya cdm ambayo sasa yamewekwa bendera za ccm lakini inashindikana.

wewe uliyepost hii thread ndiye unayeiua CHADEMA hapo mpanda hasa kwa majungu yako haya.
 
tangu saa tisa na robo hadi sasa 15:53 bado hujaweza kuweka picha?
 
Vijana ndio wanye matatizo wala siyo Arfi.Wakiwa wanaipenda CHADEMA watafanya mikakati yao kama vijana ili kuiinua CHADEMA na kujiunga CCM kuna nipa wasiwasi kuwa walikuwa wachumia tumbo na wala hawana mapendi na chama chao.Hutakiwi kukimbia vita bali kutafuta suluhisho ili ushinde.Poleni Mpanda
kweli kabisa kama ni kweli anatumika kuua chama vijana mnapohama si mnamrahisishia kazi tu kama anavyoidai mlete mada kwamba ametumwa na Pinda
 
Vijana wapenda mabadiriko hawawezi kukaa na kulalama badala yake watakaa na kujibidisha hata kurejesha nguvu ya chama lakini kama munafanya kumkomoa Arfi basi kubalini kwamba mumejizira
 
Gamba hili linatumika na ccm hana jipya huyu vijana mpanda tuko saafi na mbunge wetu!anza upya tena kudanganya!
 
Gamba hili linatumika na ccm hana jipya huyu vijana mpanda tuko saafi na mbunge wetu!anza upya tena kudanganya!

Hakuna gamba wala anayetumika na ccm hii kitu ndio itatuangusha chadema inabidi tukubali ukweli iki tujipange na si kupinga kila kitu na mtu anayesema ukweli unaitwa gamba.je ukweli ni upi kama mimi nadanganya?
 
wewe uliyepost hii thread ndiye unayeiua CHADEMA hapo mpanda hasa kwa majungu yako haya.

Hakuna majungu hapo bro.je ninachosema ni uongo?kama we upo mpanda,je ofisi ya mpanda ipo wazi?je umepita ofisi yake leo?je wewe mara ya mwisho kumuona arfi hapa mpanda ni lini?je lile shina la cdm pale kwa mafundi baiskeli lipo?
 
kweli kabisa kama ni kweli anatumika kuua chama vijana mnapohama si mnamrahisishia kazi tu kama anavyoidai mlete mada kwamba ametumwa na Pinda

Hili si la kulipuuzia.Kwa fununu nilizonazo CDM ilishinda mpanda kwa Kura za chuki, kwani mtu aliyekuwa anakubalika ndani ya CCM alichakachuliwa ,hivyo watu waliunganisha nguvu na kuipa CDM.Lakini 2015 huyo jamaa yuko kwenye mkakati wa kurudi kugombea na amejipanga vilivyo nikisoma huu uzi ,naamini kwamba hili jimbo 2015,kama CDM hawajipangi linaondoka.
 
Mkuu haya unayoyamwaga hapa hayana tofauti na ya wale waliotimuliwa na jana wakajiunga na chama cha magereza.. Kuleta hapa unadhani kutasaidia vipi ku-solve tatizo kama ni kweli yapo hayo usemayo..?
 
Back
Top Bottom