Sidhani kwamba kitendo cha serikali ya Samia kumfungulia Mbowe mashitaka ya ugaidi na tuhuma nzito za kupanga mauaji ya viongozi, inamaanisha kwamba Samia ni katili zaidi kuliko Magufuli.
Inajulikana kwamba Magufuli binafsi alikuwa mara nyingi akitamani hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wapinzani na wengine waliokatisha mbele yake. Kuna wakati alisikika akisema alitamani awe IGP ili awanyooshe watu fulani. Katika kesi ya mauaji ya Akwilina, ilisikika kwamba aliagiza kina Mbowe wafunguliwe kesi ya mauaji ya Akwilina. Kilichozuia hayo hakifahamiki. Mara nyingine alisikika akiagiza kwamba mtu yeyote anayelalamika vyuma vimebana, afunguliwe mashitaka ya kutoa takwimu zake binafsi, maana takwimu za serikali zinasema uchumi inapaa. Hilo nalo halikutekelezwa.
Kinachoonekana hapa rais Samia ana mfumo wa utawala tofauti kidogo na wa Magufuli. Nadiriki kusema Samia, dove, kazungukwa na more powerful Hawks, wakati Hawk Magufuli alizungukwa na very influential doves.
Samia kaahidi mengi ambayo kashindwa kuyatimiza, the Hawks carried the day. Rejea ahadi ya kukutana na wapinzani. Hata hii bajeti yake inaonesha jinsi anavyoyumba na kuyumbishwa na Hawks.
Pamoja na yote hayo, persecution inafanikiwa pale the persecuted wanaogopa. Lakini Mbowe ambaye during Magufuli tyranny alikuwa mostly Dove, sasa anabadilika na kuelekea kwa Lissu. Hata tone yake imebadilika sana. Hawa ndio mashujaa wa kweli wa Tanzania