Ardhi na Maji kuamua Ubunge Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ardhi na Maji kuamua Ubunge Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Zitto, Mar 11, 2012.

 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Chama chetu kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Uzinduzi ulifana sana kwa maandamano ya wananchi kutoka pande zote za Jimbo na pia Helkopta iliyowaleta Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mheshimiwa Mbowe na Mgombea wetu ndugu Joshua Nassari. Uwanja wa Leganga ulitapika watu na wananchi walipamba barabara Kuu ya Moshi-Arusha.

  Katika mazungumzo yangu na ndugu Nassari na wananchi wa Arumeru, ni dhahiri tatizo la mgawanyo wa Ardhi kati wananchi na matajiri wachache litakuwa ni agenda kubwa. Nimepata muda kidogo kuandika makala hii fupi.

  Ardhi, Maji na Ajira kuamua Ubunge Meru

  "Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi mnavyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu". Haya yalikuwa baadhi ya maneno yangu katika hotuba ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua kampeni za chama chetu katika viwanja vya Leganga katika mji mdogo wa USA River wilayani Arumeru.
  Siku moja kabla ya siku ya uzinduzi nilikuwa najisomea makala mbalimbali kuhusu Wilaya ya Arumeru. Pia nilitumia muda mrefu kuzungumza na wananchi wa Meru ili kujua uchaguzi huu una maana gani kwao. WaMeru wengi niliozungumza nao waliniambia namna wanavyochukizwa na ukosefu wa Ardhi kwa wananchi. Baadhi waliniambia kwamba Kama Serikali haitachukulia suala la Ardhi kwa uzito wake Meru kutatokea vurugu kubwa sana.*
  Vurugu Meru sio Jambo jipya kabisa. Inakumbukwa kwamba miaka ya 1950 kulitokea fujo na wananchi kuchomewa nyumba zao ili kupisha wakulima wakubwa kutoka Afrika Kusini (makaburu) katika eneo la Engarananyuki. Vurugu hizi ndio zilipelekea WaMeru kuchanga fedha kumpeleka ndugu Jafet Kirilo huko Umoja wa Mataifa kutetea Ardhi ya Wameru mwaka 1952 kufuatia vurugu za mwaka 1951. Licha ya juhudi hizo bado Ardhi ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Meru.
  Mashamba makubwa ambayo walipewa walowezi wakati wa Uhuru yaligawiwa kwa familia chache sana Meru. Wanasiasa walijipa mashamba makubwa na mengine mpaka Leo hayakugawiwa. Ujamaa na utaifishaji wa mashamba haukufanyika Meru kwa mshangao mkubwa sana na hata mashamba ambayo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliagiza wapewe wananchi walipewa Wabunge, Madiwani, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri (soma Brian Cooksey kuhusu uwekezaji katika Maua, June 2011).
  Hivi Leo Ardhi kubwa ya Meru imeshikwa na matajiri na kulimwa Maua. Kilimo hiki cha Maua mwaka 2008 kiliingizia Taifa fedha za kigeni takribani tshs 150bn. Hata hivyo kuna malalamiko makubwa sana ya wananchi wanaofanya kazi katika mashamba haya kuhusu malipo duni na nyenzo za kufanyia kazi. Kuna malalamiko kuhusu kemikali na madawa yanayotumika na *afya ya mfanyakazi kutozingatiwa.
  Ifahamike kwamba Benki ya Rasilimali Tanzania inasimamia mikopo ya zaidi ya tshs 50bn ambazo kampuni za Maua zilipewa kwa Dhamana ana ya Serikali. Katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, suala hili liliibuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TIB kukiri kwamba hakuna kampuni umeanza kulipa mikopo hii. Ni dhahiri Serikali itajikuta inalipa madeni haya yaliyokopeshwa kwa kampuni binafsi! Hii pia inaonyesha namna amabvyo serikali inafanya haraka na wepesi kusaidia wawekezaji kuliko wananchi wanaoteseka na kukosa Ardhi ya kulima na kujipatia ruziki.
  Wawekezaji wanapewa Ardhi na mtaji!*
  Haya ndio yanajenga hasira ya wananchi wa Meru. Hasira hii kwa vyovyote itahamishiwa katika sanduku la kura ili kumpata Mbunge kutoka miongoni mwao atakayeweza kusimama kidete kuhakikisha Ardhi inapatikana kwa wananchi wa Meru. Kwa nini huko nyuma, katika chaguzi zilizopita Jambo hili halikuwapa hasira wananchi? Ni dhahiri hapakuwa na Mwanasiasa ambaye ana uwezo mkubwa wa kulieleza na kuwapa imani wananchi. Ndugu Joshua Nassari amedhihirisha kwamba analijua tatizo hili kwa dhati kabisa. Nilivyomsikiliza akiongea katika kampeni, na pia katika mazungumzo yetu binafsi amenithibitishia kuwa ni mwanasiasa kijana mwenye kipaji kikubwa katika kujenga hoja na ku articulate masuala ya msingi.
  Changamoto nyingine kubwa kwa Meru ni haki ya kupata Maji. Meru kuna Maji mengi sana lakini matajiri wenye mashamba wameyazuia Maji hayo na hivyo wananchi wa kawaida hawapati Maji ya kumwagilia mazao Yao na pia kwa matumizi ya nyumbani. Hili nalo linajenga hasira kubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Ardhi na Maji ni masuala yanayokwenda pamoja wilayani Meru.
  Mwisho kabisa nimeona makundi ya vijana wasio na ajira na hivyo kukosa Kipato. Vijana wengi wanashinda kwenye stendi za mabasi na kuita abiria. Ukosefu wa Ajira kwa vijana Kama tusemavyo kila wakati ni changamoto kubwa sana kwetu viongozi na hasa viongozi vijana. Natumai ndugu Joshua Nassari atahusisha suala la Ardhi na Maji katika muktadha mzima wa Ajira na Kipato kwa wananchi wa Arumeru Mashariki. Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari*
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Azimio la Arusha kutogusa Arumeru? Chini ya Sokoine wa huko? Imenistua kidogo pengine sera ilikuwa na mapungufu kuliko tulivyowahi kufikiri!
   
 3. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Zitto, tunashukuru lakini siku nyingine uweke paragraph. Ni Tabu sana kusoma ujumbe mrefu usiokuwa na Paragraph hususani kwa Front size ndogo!
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tunatakiwa kufanya mabadiliko nchi nzima. Meru ni part tu.
   
 5. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  juzi juzi tu halmashauri ya meru iliuza viwanja kwa bei ya ajabu.square meter 1 kwa sh za kitanzani elfu kumi na sita.sikuelewa mlengwa wa viwanja hivi ni nani.
   
 6. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Siku zote mtaji wa ccm ni umaskini na ujinga wa watanzania.
  Ccm wanatumia ujinga wa kutoelewa mambo wa watanzania kwa kuwadanganya watakavyo. Mfano usipo chagua ccm amani itatoweka na mtapambana na rungu la dola kwa yoyote atakaye pigia kura upinzani na kukufukuza kazi. kwa ujinga wetu tunakubali.
  Ccm wanatumia umaskini wetu kama mtaji wao kwa kutugawia kofia, kanga, tshirt, sabuni, sukari na chumvi ili wapewe kura, nasi sababu ya ujinga na umaskini na kutoelewa kwetu tunakubali. Ccm wanaogopa ukweli
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ni idea nzuri, lakini angalieni msije kuwa wapiga propaganda kama magamba. Mkishaiwahadaa wananchi wawape kura kwa kutumia kigezo cha ardhi na maji, halafu mkashinda uchaguzi, mtawanyang'anya matajiri ardhi yao? Mtatumia kigezo gani? Sheria zinasemaje kuhusu umiliki wa ardhi? Au hao wawekezaji/matajiri hiyo ardhi waliipataje? Hakukuwa na taratibu za kisheria za kuwapa hiyo ardhi? Kama zilikuwepo, mtatumia kigezo gani kuwanyang'anya na kuwapa wananchi? Mtaishia kuibua migogoro kama ya Zimbabwe, maana hata baada ya kuinyang'anya kutoka kwa hao matajiri sidhani kama mtaweza kuwagawia wananchi wa kawaida kwa usawa. Kwa vyovyote vile mtaibua migogoro mingine katika ugawaji wa hiyo ardhi kwa wananchi. Angalieni hiyo hoja isije ikageuka kuwa mwiba kwa Nassari hapo baadaye.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Zitto,

  Hiyo mikopo ya 50B uliyoiongelea, ilitolewa na nani kupitia TIB ili wakopeshwe wakulima, au kama ni fedha ya TIB yenyewe Jee, kuna vigezo vipi ambavyo TIB wanavizingatia kuhusu "collateral"? Au benki za Tanzania zinatoa mikopo bila "collateral"?

  Usishangae kuhusu Nyerere kutokutaifisha huko, Nyerere kutaifisha kwake kulilenga kundi fulani tu, lakini si wengi wanaotaka kuliongelea hili na ni wengi ambao hawalijui hili kwa kuwa haliongelewi. Nakupa pongezi kwa kuwa jasiri na kuliweka wazi. Kwani Watanzania wengi wanaaminishwa kuongea mapungufu ya Nyerere ni "taboo".

  A taboo is a strong social prohibition (or ban) relating to any area of human activity or social custom that is sacred and/or forbidden based on moral judgment, religious beliefs and or scientific consensus. Breaking a taboo is usually considered objectionable or abhorrent by society. The term comes from the Tongan word tabu, meaning set apart or forbidden, and appears in many Polynesian cultures. In those cultures, a tabu (or tapu or kapu) often has specific religious associations. American author Herman Melville, in his first novel "Typee" describes both the origin and use of the word in Polynesian culture. "The word itself (taboo) is used in more than one signification. It is sometimes used by a parent to a child, when in the exercise of parental authority forbids the child to perform a particular action. Anything opposed to the ordinary customs of the islands, although not expressly prohibited is said to be 'taboo'."

  When an activity or custom is taboo, it is forbidden and interdictions are implemented concerning it, such as the ground set apart as a sanctuary for criminals. Some taboo activities or customs are prohibited under law and transgressions may lead to severe penalties. On the other hand taboos result in embarrassment, shame, and rudeness. Although critics and/or dissenters may oppose taboos, they are put into place to avoid disrespect to any given authority, be it legal, moral and/or religious.

  Read more: Taboo - Wikipedia, the free encyclopedia
   
 9. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,544
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hizi ndio hoja za kujadili sio mambo ya kutoboa masikio .
   
 10. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Imeandikwa na Zitto Kabwe.
  Chama chetu kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Uzinduzi ulifana sana kwa maandamano ya wananchi kutoka pande zote za Jimbo na pia Helkopta iliyowaleta Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mheshimiwa Mbowe na Mgombea wetu ndugu Joshua Nassari. Uwanja wa Leganga ulitapika watu na wananchi walipamba barabara Kuu ya Moshi-Arusha.

  Katika mazungumzo yangu na ndugu Nassari na wananchi wa Arumeru, ni dhahiri tatizo la mgawanyo wa Ardhi kati wananchi na matajiri wachache litakuwa ni agenda kubwa. Nimepata muda kidogo kuandika makala hii fupi.

  Ardhi, Maji na Ajira kuamua Ubunge Meru

  "Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi mnavyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu". Haya yalikuwa baadhi ya maneno yangu katika hotuba ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua kampeni za chama chetu katika viwanja vya Leganga katika mji mdogo wa USA River wilayani Arumeru.

  Siku moja kabla ya siku ya uzinduzi nilikuwa najisomea makala mbalimbali kuhusu Wilaya ya Arumeru. Pia nilitumia muda mrefu kuzungumza na wananchi wa Meru ili kujua uchaguzi huu una maana gani kwao. WaMeru wengi niliozungumza nao waliniambia namna wanavyochukizwa na ukosefu wa Ardhi kwa wananchi. Baadhi waliniambia kwamba Kama Serikali haitachukulia suala la Ardhi kwa uzito wake Meru kutatokea vurugu kubwa sana.*

  Vurugu Meru sio Jambo jipya kabisa. Inakumbukwa kwamba miaka ya 1950 kulitokea fujo na wananchi kuchomewa nyumba zao ili kupisha wakulima wakubwa kutoka Afrika Kusini (makaburu) katika eneo la Engarananyuki. Vurugu hizi ndio zilipelekea WaMeru kuchanga fedha kumpeleka ndugu Jafet Kirilo huko Umoja wa Mataifa kutetea Ardhi ya Wameru mwaka 1952 kufuatia vurugu za mwaka 1951. Licha ya juhudi hizo bado Ardhi ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Meru.

  Mashamba makubwa ambayo walipewa walowezi wakati wa Uhuru yaligawiwa kwa familia chache sana Meru. Wanasiasa walijipa mashamba makubwa na mengine mpaka Leo hayakugawiwa. Ujamaa na utaifishaji wa mashamba haukufanyika Meru kwa mshangao mkubwa sana na hata mashamba ambayo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliagiza wapewe wananchi walipewa Wabunge, Madiwani, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri (soma Brian Cooksey kuhusu uwekezaji katika Maua, June 2011).

  Hivi Leo Ardhi kubwa ya Meru imeshikwa na matajiri na kulimwa Maua. Kilimo hiki cha Maua mwaka 2008 kiliingizia Taifa fedha za kigeni takribani tshs 150bn. Hata hivyo kuna malalamiko makubwa sana ya wananchi wanaofanya kazi katika mashamba haya kuhusu malipo duni na nyenzo za kufanyia kazi. Kuna malalamiko kuhusu kemikali na madawa yanayotumika na afya ya mfanyakazi kutozingatiwa.

  Ifahamike kwamba Benki ya Rasilimali Tanzania inasimamia mikopo ya zaidi ya tshs 50bn ambazo kampuni za Maua zilipewa kwa Dhamana ya Serikali. Katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, suala hili liliibuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TIB kukiri kwamba hakuna kampuni ambayo imeanza kulipa mikopo hii. Ni dhahiri Serikali itajikuta inalipa madeni haya yaliyokopeshwa kwa kampuni binafsi! Hii pia inaonyesha namna amabvyo serikali inafanya haraka na wepesi kusaidia wawekezaji kuliko wananchi wanaoteseka na kukosa Ardhi ya kulima na kujipatia ruziki.

  Wawekezaji wanapewa Ardhi na mtaji!
  Haya ndio yanajenga hasira ya wananchi wa Meru. Hasira hii kwa vyovyote itahamishiwa katika sanduku la kura ili kumpata Mbunge kutoka miongoni mwao atakayeweza kusimama kidete kuhakikisha Ardhi inapatikana kwa wananchi wa Meru. Kwa nini huko nyuma, katika chaguzi zilizopita Jambo hili halikuwapa hasira wananchi? Ni dhahiri hapakuwa na Mwanasiasa ambaye ana uwezo mkubwa wa kulieleza na kuwapa imani wananchi. Ndugu Joshua Nassari amedhihirisha kwamba analijua tatizo hili kwa dhati kabisa. Nilivyomsikiliza akiongea katika kampeni, na pia katika mazungumzo yetu binafsi amenithibitishia kuwa ni mwanasiasa kijana mwenye kipaji kikubwa katika kujenga hoja na ku articulate masuala ya msingi.

  Changamoto nyingine kubwa kwa Meru ni haki ya kupata Maji. Meru kuna Maji mengi sana lakini matajiri wenye mashamba wameyazuia Maji hayo na hivyo wananchi wa kawaida hawapati Maji ya kumwagilia mazao Yao na pia kwa matumizi ya nyumbani. Hili nalo linajenga hasira kubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Ardhi na Maji ni masuala yanayokwenda pamoja wilayani Meru.

  Mwisho kabisa nimeona makundi ya vijana wasio na ajira na hivyo kukosa Kipato. Vijana wengi wanashinda kwenye stendi za mabasi na kuita abiria. Ukosefu wa Ajira kwa vijana Kama tusemavyo kila wakati ni changamoto kubwa sana kwetu viongozi na hasa viongozi vijana. Natumai ndugu Joshua Nassari atahusisha suala la Ardhi na Maji katika muktadha mzima wa Ajira na Kipato kwa wananchi wa Arumeru Mashariki. Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari.
   
 11. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  namshukuru sana mh zitto.

  Ardhi hiyo iliuzwa kati ya million 5 na 15, hiyo elfu kumi ni changa la macho na kuchukua hela za walalahoi.

  Kuna kabare estate agent wakishirikiana na manispaa ya meru wanauza ardhi mpaka million 50.

  Hiyo ardhi ni ya nani? Wamepata wapi? Wizi mtupu.

  Ardhi ni tatizo kubwa hapa nchini, kuna matatizo ya ardhi pande zote za nchi. Wananchi wanadhulumiwa.

  Kampeni za arumeru ziwe chachu ya kudai haki za ardhi kwa wananchi nchi nzima.

  Niliwahi kuandika kuhusu ardhi mara nyingi hapa nitajaribu kuzirudisha tena hewani muzisome. Pia katika mapendekezo/kero aliyokuwa anakusanya marehemu regia niliandika.

  Natumaini mh zitto utarudi tena arusha - arumeru mashariki na utakazia zaidi ili liwe swala la kitaifa. Sijui kama mnakumbuka marehemu regia mtema aliongea bungeni.

  Pia katika hotuba ya waziri kivuli wa ardhi mh halima mdee. Alitaja vigogo wanaohodhi ardhi huku vijana na wananchi wakitaabika.
   
 12. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siku hizi ni rahisi kujadili mgombea aliyetoga(siyo kutoboa) masikio kuliko kujadili kati ya Nasari na Sumari nani ana uwezo wa kutatua tatizo la ardhi au maji Arumeru. Hata hii siredi ingekuwa ina mashabiki wengi kama zitto angeandika "sumari jinsia yake ina utata". JF ni sehemu tu ya tatizo kubwa sana tulio nalo watanzania la kutokutaka kujadili mambo ya maana na tatizo hili linaletwa na wengi wetu kutokupenda kusoma.

  Hapa Zitto amechokoza tu, sasa ni zamu ya wagombea wenyewe kuchambua kwa kina na kutupa mawazo yao ni kwa jinsi gani wataweza kutatua matizo haya mawili. Na kwa watu wa Arumeru wajikite kwenye kuhudhuria mikutano ya wagombea hawa na kuwahoji maswali kwani ni wao ndiyo watakuwa wabunge na siyo kundi kubwa la wapiga debe ambalo kwa sasa limevamia Arumeru kwani mwisho wa siku watabakia wenyewe na mbunge wao watakayemchagua!!
   
 13. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ninavyofahamu kiwanja cha bei nafuu kilianzia na gharama ya milioni kumi na sita
   
 14. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kweli Uda, elfu kumi ilikuwa changa la macho, just formalities ili wazitafune vizuri hizo hela za viwanja.

  Viwanja wameuziana wenyewe na kujenga nyumba za kupanga
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kipande hicho kinafurahisha sana, kwani hicho ndio kiini cha matatizo, na ni vizuri umeujulisha umma kuwa tatizo limeanzia wakati wa Nyerere (kabla ya Uhuru sitoongelea, ilipaswa Nyerere atatuwe tatizo).

  Inaonesha wazi hapo ingawa Nyerere kaagiza wapewe wanachi, wakapewa hao uliowataja na huku Nyerere alishindwa kufanya chochote kuhusu hilo. Nani aliyewapa kama si Nyerere mwenyewe? Ardhi ya Tanzania haigaiwi na mwingine zaidi ya Rais. Hapo sasa!

  Nna uhakika, tatizo hilo likifika kwa Mzee wa kutatua matatizo, halitochukuwa raundi zaidi ya mbili kwenye ulingo wake na litakuwa historia.
   
 16. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wewe tangu zama zileee ukiitwa vileee ulikuwa ukisikia jina "Nyerere" unaweweseka! Nilifikiri ulipopigwa ile kitu utabadilika!! Rais tangu lini akagawa Ardhi? Miye namiliki ardhi sehemu mbali mbali na hakuna hata moja niliyopewa na Rais.
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Invisible na JF Admins!
  nilishaomba mtubadilishie hii font lakini naona mmekaa kimya kuna wengine tuna matatizo ya macho na Migraine, sasa hiyo thread ya Zitto haina hata paragraph tutaisomaje?
  nimesoma mistari kumi nishaanza sikia kizunguzungu..
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Soma vizuri, Nyerere "aliagiza", sasa hizo zako sijui aliyeagiza nani. Lakini Zitto kasema wazi. Una matatizo ya kusoma?
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Hapa ndio watu wanaposimamia kuwa rushwa imeanzia mbali haya ya sasa yanafumuka sababu ya utandawazi tu! Kwa maelezo haya ya Zitto hata Azimio la Arusha rushwa ilitembea!
   
 20. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Safi sana hii Zito kweli ardhi imekuwa ni tatizo ila wasiwasi wangu ni ardhi ipi sasa mtakayo rudisha kwa wananchi?
  Nikijaribu kuangalia maeneo yale yaliyo kuwa ya wazi wameshagaiwa wenye nguvu ya pesa,
  Na hayo makampuni ya maua ukienda kuangalia dhamani ya uwekezaje walioufanya ni wa pesa nyingi na wamepewa yale mashamba kisheria kabisa wengine wana lease ya miaka 99.
  Najaribu kufikiri,Natamani yatokee uliyoyaandika ila napata wasiwasi wa utekelezwaji wake pindi tutakapokuwa tumempa Nassary ridhaa.
   
Loading...