JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,314
- 5,478
Mwakameta amepunguza uzito kutoka Kilo 151 alizokuwanazo kabla ya Februari 20, 2023 alipowekewa puto hadi kufikia Kilo 92.65 alipotolewa puto hilo Februari 26, 2024.
Akielezea kuhusu safari yake ya kupungua uzito Mwakameta amesema ilianza baada ya kumuona msanii Peter Msechu ambaye aliwekewa puto hospitalini hapa na kuona kwamba huduma hii ni ya kweli na ina matokeo mazuri.
“Kipindi nilipokuja kuwekewa puto nilikuwa na kilo 151 lakini mpaka leo nimekuja kutoa puto baada ya mwaka mmoja nina kilo 92.65, watu walikua wakinicheka kutokana na uzito uliokithiri pia ninataka kuwaasa watanzania wenzangu wenye matatizo ya uzito mkubwa kuweka puto kunasaidia kupunguza uzito na wasiogope," amefafanua Mwakameta.
Kufuatia matokeo hayo mazuri ameishauri kufika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ili kupata huduma ya kuweka puto ambayo imemsaidia na hajapata madhara yoyote zaidi ameweza kubalilisha mfumo wake wa maisha.
Muhimbili Mloganzila ilianzisha huduma ya kupunguza uzito kwa kutumia puto (intragastric balloon) ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2022 takribani wananchi 158 wamenufaika na huduma hiyo.
Chanzo: Hospitali ya Mloganzila