Si kweli, number of downloads hulipwi hata shilingi tano.. Mimi developer so najua, ingekua hivo kila mtu angetengeneza app.
Apps kama hazina matangazo na ni bure basi watakua na njia yao wenyewe ya kupata pesa, mfano wengine wanapata from investors, apps kama QuizUp, haziingizi hata shilingi from users, pesa wanapewa na investors tu, wanatengeneza kwanza base ya watu mwisho wa siku watakuja kupata returns baadaye wakishakua na users wengi.
Kupatana nao kama hawalipwi na mtu anayeuza kitu yaani percentage flani ya kile kitu anachouza basi wapo bado wanajenga user base yao, site ikishakua famous ikapata users wengi sana then itawapa mpenyo rahisi kuchaji wafanyabiashara wanaouza vitu kwenye site yao. Huwezi kuanza tu mwanzo na kuwachaji watu pesa huku huna users hutopata muuzaji.
Kuhusu instagram accounts, zinaingiza pesa kwa njia nyingi,
Njia ya kwanza unatangaza kitu unachouza watu wanakucontact unawauzia.
Njia ya pili, unajenga followers wengi, then unauza account kwa watu wanaohitaji kutangaza biashara zao.
Njia ya tatu, unajenga followers wengi alafu unatafuta watu wanaotaka kutangaza biashara unawachaji kiasi flani kwa kila tangazo.