Appropriate use of honorary doctorate

Appropriate use of honorary doctorate

ebandio

Senior Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
107
Reaction score
32
Wadau,
I was reading through the TCU "Quality Assurance General Guidelines and Minimum Standards for Provision of University Education in Tanzania" second edition, and found some interesting guide regarding the correct use of titles from Honorary Degrees especially the PhDs. Part III provides guide on the minimum guidelines for harmonization of awards offered in Tanzania and 3.5 provides guidelines on Honorary Doctorates so referred to as honoris causa. Items 3.5(g) and (h) provides that:
"(g) The nomencleture for honorary doctorate award should be Honorary Doctorate Award and is abbreviated as PhD (Hon. Causa)

(h) A holder of honorary award will be required to indicate in the title that the award referred to is honorary and not academic as follows, i.e. Mr Mashauri Maneno, PhD (Hon. Causa) and not Dr. Mashauri Maneno"
end of quote.​

Is this in actual practice as the guidelines directs so. Your opinion please.
Alamsiki
 
ebandio, kwani matumizi ya hii shahada ya heshima kwa sasa yakoje. Nasikia JKN alikuwa nazo za kuzidi lakini sikuwahi kusikia wakimwita kwa jina hilo.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli zipo in practice. Ma-Rais wetu wote wamepewa hizo Honorary PhDs. Nyerere, Mwinyi na Mkapa wote wanazo ila walikataa wasiitwe Dr Kama utambulisho wao. But our current President yeye amekomalia kuitwa Dr. Hajataka kufata nyayo za wenzie.
 
Hiyo haina matumizi yoyote zaidi ya heshima tu. Huwezi kufanyia kazi au hata kuajiliwa kwa kutumia hiyo Honorary PhD, ni Non-academic degree.
 
Last edited by a moderator:
wakiweka hako hicho kibatanisho watajitwalia ujiko sa ngapi?
 
Waandishi wetu uchwara ndio tabu ....
 
Nje ya academia kujitutumua kujiita Dr., hata kama si honorary, ni ulimbukeni unaoonyesha jinsi gani sisi ni wageni wa haya mambo.

Robert Gates, Mkurugenzi wa zamani wa CIA ambaye alipata pia kuwa Waziri wa Ulinzi wa US, ana Ph.D. ni Dr. Robert Gates.

Lakini ukitafuta habari zake ni nadra sana kukuta anatumia Dr.

Kina Susan Rice, Condoleezza Rice wote wale ni Ph.Ds. Tena si honorary.

Lakini ni nadra sana kuona wanaitwa au wanasisitiza kuitwa Dr.

Ni huku kwetu tu mashikolo mageni ndiko tuna kasumba hii.
 
Ni kweli zipo in practice. Ma-Rais wetu wote wamepewa hizo Honorary PhDs. Nyerere, Mwinyi na Mkapa wote wanazo ila walikataa wasiitwe Dr Kama utambulisho wao. But our current President yeye amekomalia kuitwa Dr. Hajataka kufata nyayo za wenzie.
JPM PhD ya kwake ameisotea (Chemistry, UDSM) kama wengine as such ana haki ya kuandika Dr. kabla ya jina lake.

Kina Susan Rice, Condoleezza Rice wote wale ni Ph.Ds. Tena si honorary.
Condo ameitwa Dr. Rice wanapokuwa formal. Kitu ambacho nje ya chuo hatumii ni Professor Rice. Though ni kweli hawasisitizi kuitwa Dr au Prof. Huku kwetu u _Prof ni mpaka kufa hata kama umeacha kazi ya chuo.
 
Nje ya academia kujitutumua kujiita Dr., hata kama si honorary, ni ulimbukeni unaoonyesha jinsi gani sisi ni wageni wa haya mambo.

Robert Gates, Mkurugenzi wa zamani wa CIA ambaye alipata pia kuwa Waziri wa Ulinzi wa US, ana Ph.D. ni Dr. Robert Gates.

Lakini ukitafuta habari zake ni nadra sana kukuta anatumia Dr.

Kina Susan Rice, Condoleezza Rice wote wale ni Ph.Ds. Tena si honorary.

Lakini ni nadra sana kuona wanaitwa au wanasisitiza kuitwa Dr.

Ni huku kwetu tu mashikolo mageni ndiko tuna kasumba hii.
Nianze kwa kukuuliza wewe una PhD? Maana kuna tatizo hapa la wivu na kuzungumzia kitu ambacho hatuna.
 
JPM PhD ya kwake ameisotea (Chemistry, UDSM) kama wengine as such ana haki ya kuandika Dr. kabla ya jina lake.

Condo siku zote ameitwa Dr. Rice wanapokuwa formal. Kitu ambacho nje ya chuo hatumii ni Professor Rice.
Siku zote maana yake nini?

Nasoma kitabu chake kipya "Democracy: Stories From The Long Road To Freedom".

Kwenye cover wamemuandika "Condoleezza Rice" si Dr. Condoleezza Rice.
 
Sorry nilikuwa na edit my post na kubakiza wanapotaka kuwa formal ndo humu-address kama Dr.
 
Nianze kwa kukuuliza wewe una PhD? Maana kuna tatizo hapa la wivu na kuzungumzia kitu ambacho hatuna.
Mimi nimefundisha ex girlfriend wangu alipokuwa anatafuta Ph.D. Alikuwa hajui case study ya kutumia kuonyesha kiongozi wa kisiasa aliyewatoa wananchi wake wengi kwenye umasikini, akasema anamjua Yunus Mohammed tu wa Bangladesh, lakini huyo ni social enterpreneur, si kiongozi wa kisiasa. Nikamtajia Fernando Henrique Cardosso wa Brazil. Alivyokwenda ku present darasani kwao darasa zima halikumjua Cardosso ni nani.

That goes to show kwamba sio kila mtu anayejua mambo anaingia huko kutafuta ma Ph.D. Wengine tunajenga biashara zetu.

Sasa hivi ex girlfriend ana Ph.D yake na ananishukuru kila siku kwa msaada niliompa wakati anaitafuta kwa maana nilikuwa kama teaching assistant kwake.

Mimi kwa career yangu na biashara zangu Ph.D ni kupoteza muda na resources.

Kwa watu wanaoielewa Ph.D, kama hutaki kufundisha au kwenda kwenye a very specialized research field, Ph.D ni kutafuta ujiko tu.

Kufikiri kwamba kuichambua Ph.D ni lazima uwe na Ph.D ni ulimbukeni mwingine.

Ni mawazo mgando ya kufikiri aliyevaa suti ni mstaarabu, mwenye hela ana akili, anayejua Kiingereza kasoma, mwenye Ph.D ni msomi.
 
Mimi nimefundisha ex girlfriend wangu alipokuwa anatafuta Ph.D. Alikuwa hajui case study ya kutumia kuonyesha kiongozi wa kisiasa aliyewatoa wananchi wake wengi kwenye umasikini, akasema anamjua Yunus Mohammed tu wa Bangladesh, lakini huyo ni social enterpreneur, si kiongizi wa kisiasa. Nikamtajia Fernando Henrique Cardosso wa Brazil. Alivyokwenda ku present darasani kwao darasa zima halikumjua Cardosso ni nani.

That gies to show kwamba sio kila mtu anayejua mambo anaingia huko kutafuta ma Ph.D. Wengine tunajenga biashara zetu.

Sasa hivi ex girlfruend ana Ph.D yake na ananishukuru kila siku kwa msaada niliompa wakati anaitafuta kwa maana nilikuwa kama teaching assistant kwake.

Mimi kwa career yangu na biashara zangu Ph.D ni kupoteza muda na resources.

Kufikiri kwamba kuichambua Ph.D ni kazima uwe na Ph.D ni ulimbukeni mwingine.

Ni mawazo mgando ya kufikiri aliyevaa suti ni mstaarabu, mwenye hela ana akili, anayejua Kiingereza kasoma, mwenye Ph.D ni msomi.
Acha wivu acha waliopata PhD watambe kwa kuitwa Dr. Ni uswahili kusema kuwa ni kupoteza resources. I can tell you bado kabisa, hata ukiwa mkulima kupata PhD muhimu. Kumbe inaonyesha ni kwa nini unamchukia Dr Magufuli ni kwa sababu yeye ana PhD na wewe huna. Usipende kuzungumzia kitu ambacho ni kikubwa kwako acha wenye PhD wajijadili la sivyo huo ni wivu wa uswazi kwetu
 
Kwanza kabisa unaonekana kukosa maarifa kwa kulinganisha moja kwa moja Ph.D na usomi.

Pili unafanya psychological projection.

Unafikiri kwa sababu wewe una tabia ya wivu, kika mtu ana wivu.

Mimi naishi Marekani.

Mwalimu Ph.Ds ni walimu wa vyuo vikuu.

Walimu wa vyuo vikuu wanaliowa mishahara midogo sana na hawathaminiwi kama huko nchi ambazo elimu ya darasani ni ngeni bado.

Ukiongelea kumuonea wivu mtu kwa sababu ya Ph.D unajionyesha ulimbukeni wako wa kuiweka juu Ph.D.
 
Wadau,
I was reading through the TCU "Quality Assurance General Guidelines and Minimum Standards for Provision of University Education in Tanzania" second edition, and found some interesting guide regarding the correct use of titles from Honorary Degrees especially the PhDs. Part III provides guide on the minimum guidelines for harmonization of awards offered in Tanzania and 3.5 provides guidelines on Honorary Doctorates so referred to as honoris causa. Items 3.5(g) and (h) provides that:
"(g) The nomencleture for honorary doctorate award should be Honorary Doctorate Award and is abbreviated as PhD (Hon. Causa)

(h) A holder of honorary award will be required to indicate in the title that the award referred to is honorary and not academic as follows, i.e. Mr Mashauri Maneno, PhD (Hon. Causa) and not Dr. Mashauri Maneno"
end of quote.​

Is this in actual practice as the guidelines directs so. Your opinion please.
Alamsiki
Tatizo la hili tamko la TCU linasahau kila chuo duniani kina style yake ya kutumia hizi degree. Kama ya kwako umeiotoa China utaitumia kamachuo chako kinavyo eleza. Sasa labda wao wanaelekeza kwa zile zinazotolewa Tanzania zitumikeje. Mr Mashauri Maneno, PhD (Hon. Causa) kwangu hii haimeki sense either utumie Mr Mashauri Maneno or Dr. Mashauri Maneno, full stop, lakini kuchanganya Mr na PhD kwenye jina hilohilo nashikwa na kigugumizi. Alternatively atumie Mashauri Maneno PhD(Hon. causa) iko poa.
 
Mimi nimefundisha ex girlfriend wangu alipokuwa anatafuta Ph.D. Alikuwa hajui case study ya kutumia kuonyesha kiongozi wa kisiasa aliyewatoa wananchi wake wengi kwenye umasikini, akasema anamjua Yunus Mohammed tu wa Bangladesh, lakini huyo ni social enterpreneur, si kiongozi wa kisiasa. Nikamtajia Fernando Henrique Cardosso wa Brazil. Alivyokwenda ku present darasani kwao darasa zima halikumjua Cardosso ni nani.

That goes to show kwamba sio kila mtu anayejua mambo anaingia huko kutafuta ma Ph.D. Wengine tunajenga biashara zetu.

Sasa hivi ex girlfriend ana Ph.D yake na ananishukuru kila siku kwa msaada niliompa wakati anaitafuta kwa maana nilikuwa kama teaching assistant kwake.

Mimi kwa career yangu na biashara zangu Ph.D ni kupoteza muda na resources.

Kwa watu wanaoielewa Ph.D, kama hutaki kufundisha au kwenda kwenye a very specialized research field, Ph.D ni kutafuta ujiko tu.

Kufikiri kwamba kuichambua Ph.D ni kazima uwe na Ph.D ni ulimbukeni mwingine.

Ni mawazo mgando ya kufikiri aliyevaa suti ni mstaarabu, mwenye hela ana akili, anayejua Kiingereza kasoma, mwenye Ph.D ni msomi.
Aisee hata huyo aliekuja kumuoa inabidi na yeye akuacknowledge na kukushukuru mkuu
 
Hajaolewa bado. Alikuwa anataka sana nimuoe lakini nikampotezea.

Hata kesho nikimwambia vaa haraka haraka twende kufunga ndoa anakubali.

Na huyo si pekee. Huyo Mmarekani yuko hapa US. Kuna mwingine Mzanzibari yuko Zanzibar sasa nafikiri. Ilikuwa niende Zenj kuchukua mke. Inakuwa Ph.D huna muda wa kuitafuta unaioa tu kama Joe Biden.

Sasa mtu ambaye anasujudia sana Ph.D akisikia hivyo atashangaa sana.
 
Hajaolewa bado. Alikuwa anataka sana nimuoe lakini nikampotezea.

Hata kesho nikimwambia vaa haraka haraka twende kufunga ndoa anakubali.

Sasa mtu ambaye anasujudia sana Ph.D akisikia hivyo atashangaa sana.
Huku kwetu tuna shida sijui ni ulimbukeni... Waalimu wa nje huwa hawataki hata kidogo kuwa adressed by the titles kama Prof au Dr.. hayo utayaona tu atakapokuwa ameandika academic work au publication.. Kuna kipindi maprof wa Sua pale walienda kuintroduce mradi huko mgeta, wako kama watano kila mmoja anajitambulisha naitwa Profesa fulani.. wakulima wakashangaa na kuuliza inakuwaje watu watano wote majina yenu yanafanana?
 
Back
Top Bottom