Apple yafungua Appstore na iTunes Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Apple yafungua Appstore na iTunes Tanzania

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Millah, Jul 24, 2011.

 1. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [h=3]Apple yafungua AppStore Tanzania[/h]

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Bendera ya Tanzania, chini kulia ikithibitisha kuwa hii ni Appstore ya Tanzania[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Kwa muda mrefu sasa tumepunguza kasi ya kuandika makala mpya kwa matayarisho ya uzinduzi rasmi wa blogi yetu ya kiingereza yaani www.gadget-one.com, lakini hili imekuwa ni vigumu kuruhusu litupite. Kampuni ya Apple watengenezaji maarufu wa simu za iPhone na gajeti nyingine wamefungua maduka yao ya mtandaoni, yaani AppStore la gajeti zinazotumia iOS (iPhone, iPod Touch, iPad na Apple TV) na Mac AppStore la kompyuta za Mac katika nchi 33 zaidi Duniani ikiwemo Tanzania. Read more »
  C
  hanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia
   
 2. Given Edward

  Given Edward Verified User

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yeah, i'm not sure if I should be happy with this. Wakifungua appstore ina maana wataanza kufuatilia bidhaa zao. Na wakifuatilia itabidi tulazimike kununua os zao za Mac na sio kudownload pirated versions ambazo haziruhusiwi. Tukumbuke 2008 Microsoft ilipowakamata watanzania wawili kwa kukutwa na pirated windows, walipekekwa court. So tuwe makini.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ni habari njema sana..
   
 4. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama Apple ni wafuatiliaji wa masuala kama haya, tofauti na Windows, Apple hupigana na masuala haya kwa kutumia teknolojia na mbinu za kibiashara, kwa mfano miaka ya nyuma walikiwa wakitoa update kuzipach pirated software, tangu Mac AppStore imeanza wameacha mtindo huu, isipokuwa wanaendelea nao kwenye iOS firmware na hasa iPhone. Hivi sasa inaelekea wanalenga kufanya Apps na bidhaa nyingine kuwa affordable ili kuwafanya watumiaji wasione haja ya kuchakachua. Kwa mfano Mac OS X Lion wameishisha bei ukilinganisha na Snow Leopard kwa $100, yaani kutoka $129 hadi $29. Pia wameondoa masuala ya keys, yaani ina maana kwamba watu 10 mkishare akaunti na kununua app na wote mkazitumia, technically hamjavunja sheria na wala sio poracy. Mbinu kama hizi zimeboost sana mauzo ua Apple katika software, kwa mfano siku ya juzi tu pekee waliopotoa Lion wameuza nakala milioni moja kwa siku moja. Hii ilikuwa ni rekodi
   
 5. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  yaan kuna apps kibao tu tutakua tunakosa,tena tanzania?huh! Sio kila apps zilizopo appstore zinapatikana nchi zote hata zile za bure,bora ujiunge zako na free acc. ya US upate apps zote,thats wat i've bin doing for a longtime,na idivice yko iwe jailbroken otherwise utaumia!
   
 6. fxb

  fxb Senior Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ha haa haa hivi application zilizokuwamo kwa simu zote zaweza tumika TZ? Unapochakachua zinasaidia kukidhi matumizi ya kifaa ulichonacho?
   
 7. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kwamba si kila App kwenye AppStore inapatikana Dinuani kote, hata hivyo AppStore ya iOS ina apps 425,000. Na si kweli kwamba Apps hizi zote zinapatikana US Store, kwa mfano BBC iPlayer inapatikana bure UK na US ni $10 kwa mwezi. Na zipo Apps nyingi tu ambazo ni maalum kwa nchi fulani kwa hiyo hata duka la US huzipati. Pia jailbreak ni moja kati ya njia ya kupata apps za bure lakini jailbreak ina matatizo mawili makubwa.

  1. Mara nyingi iOS device (iPhone, iPad, iPod Touch au Apple TV) inakuwa very unstable, na hivyo mara nyingine kukubidi kuifuta device yako yote na kuanza upya.

  2. Inabidi iOS yako iwe nyuma, yaani kwa mfano sasa hivi iOS 5 beta 4 imetoka juzi, ambayo anategemea jailbreak hawezi kuitumia iOS hiyo kwa vile hakuna jailbreak yake.

  Kwa hiyo Appstore itasaidia wale ambao wamechoshwa na hizi mbio za paka na panya (Hackers Jailbreaks and Apple Patches) na hasa hasa wale ambao wako tayari kutoa $3 kununua apps kama vile The Economist, ambapo hata ukichakachua huwezi kuipata app hii
   
 8. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  US appstore ina karibia content zte zilizopo appstore....app gan utaitafuta ukose? Na kuhuhusu jailbreak tayar ios 5 beta 4 ishakua j.b tayari..
   
 9. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mkuu apple wanatengeneza apps kulingana na nchi husika kuna apps ya airtel ukiifunga kwenye simu yako inakuwa ni useless kwa sababu inatumika kwa Marekani na Canada tu.
   
 10. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ts true lakin point yangu ni kua store ya marekani ina karibia apps zote.
   
 11. newtonfox

  newtonfox Senior Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 196
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  yeah acha nisubirie hawa nokia waanze 2mia windows Os maana symbian naona wamenichosha.. ...apple za wakubwa
   
 12. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nitakupa mfano wa apps 5 ambazo zinapatikana kwenye appstore ya UK lakini USA hakuna. Sky Go (ambayo ina channel 5 za skysports pamoja na sky news) na ITV Player, BBC iPlayer, Natwest na Three. Na ujue kwamba zipo nyingine nyingi tu. Kwa mfano kuna baadhi ya apps ambazo ni za kichina au kirusi kwa ajili ya mambo yao na kadhalika hizi kwa nini waziweke kwenye US store? Hii inatokana na sababu kama vile biashara ya app husika haipo USA au app inahusika na organisation fulani kama vile hospitali ambayo haipo USA, lugha mbali mbali ambazo hazizungumzwi US na kadhalika.

  Katika masuala ya Jailbreak, hata kama jailbreak ya iOS 5 beta 4 imeshatoka, nilichokuwa ninataka kueleza ni kwamba mara nyingi kunakuwa na muda wa kusibiri baina ya jailbreak na firmware mpya. Nadhani hii naina ubishi.
   
Loading...