Nevergive up
JF-Expert Member
- Dec 24, 2024
- 349
- 503
SETNET
Sisi ni vijana wa Kitanzania tulioamua kuanzisha app ya kisasa kwa nia ya kuwa na jukwaa la kijamii, kibiashara, kielimu na kiburudani linalotoka Tanzania, kwa ajili ya Watanzania na dunia nzima.
SETNET ni app ya kizalendo inayochanganya huduma nyingi maarufu kwenye app moja ili kurahisisha matumizi na kukuza uchumi wa kidigitali wa ndani.
Sifa Kuu za SetNet:
1. Mawasiliano kamili: Kutuma ujumbe wa maandishi, sauti, picha, video, nyaraka, mahali, zawadi n.k (individually & kwenye magroup).
2 .SetBot AI: Kujibu maswali papo kwa papo kwa kutumia akili bandia.
3 .Status & Story: Kushirikiana maisha na marafiki – kwa uma au kwa faragha.
4 .Shorts & Picha (TikTok/Instagram style): Kushiriki video fupi na picha, likes, comments, na followers.
5. S-Tube: Kupakia na kutazama video kama YouTube – kwa elimu, burudani au biashara.
6. Movie & Music Zone: Filamu, nyimbo, na chaneli binafsi za kisanaa.
7. Book & App Store: Vitabu vya kielimu na apps za ndani – kusoma, kupakua, kuchangia.
8. SetNet Market & Wallet: Soko la bidhaa na malipo ya mtandaoni kwa kutumia dola, kwa urahisi kutoka sehemu yoyote duniani.
Changamoto Yetu Kuu – Kibali cha TCRA
Pamoja na jitihada zetu kama vijana wa Kitanzania, changamoto kubwa tunayokumbana nayo ni ukosefu wa kibali rasmi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuruhusiwa kusambaza app hii kisheria na kwa usalama.
Tunaiomba TCRA au wadau wengine:
Kutupatia kibali halali cha kuendesha huduma hii.
Kutusaidia kwa ushauri wa kisheria na kiufundi ili kuhakikisha app hii inakidhi viwango vya sheria, ulinzi wa data, na matumizi salama ya kidigitali.
Lengo letu ni kuonyesha kuwa vijana wa Kitanzania tunaweza kuwa sehemu ya mapinduzi ya TEHAMA duniani, tukitumia suluhisho lililoanzia nyumbani.napokea ushauri

Attachments
-
IMG-20250731-WA0026.jpg25.2 KB · Views: 17 -
IMG-20250731-WA0024.jpg34.8 KB · Views: 18 -
IMG-20250731-WA0015.jpg41.8 KB · Views: 12 -
IMG-20250731-WA0016.jpg32.8 KB · Views: 16 -
IMG-20250731-WA0012.jpg42.9 KB · Views: 14 -
IMG-20250731-WA0011.jpg56.6 KB · Views: 14 -
IMG-20250731-WA0008.jpg60 KB · Views: 19 -
IMG-20250731-WA0008.jpg60 KB · Views: 14 -
IMG-20250731-WA0010.jpg45.5 KB · Views: 17 -
IMG-20250731-WA0015.jpg41.8 KB · Views: 16