ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Google reader kipenzi cha wengi ipo kwenye mashine ya kuokolea maisha (life supporting machine) na Google imetangaza kuwa mwezi wa saba mwaka huu mashine hizo zitazimwa, huo ndio utakuwa mwisho wa huduma hiyo. Tangazo la Google kufunga huduma hiyo limewashikitisha wengi. Wadau mbali mbali ulimwenguni wako kwenye masikitiko kufuatia tangazo la kuondolewa kwa huduma hiyo. Kwa mujibu wa mtandao wa Digital Trends watu laki moja na ishirini na tano elfu wametia sahihi ya malalamiko (petition) kujaribu kuiokoa huduma hiyo isiondolewe.
Kukiwa hakuna uhakika wa kurudi kwa huduma ya Google baada ya mwezi wa saba kufikia, tutazungumzia app mbadala zinazoweza kutumika kwenye nafasi ya Google Reader kama app kwenye tableti na simu, pamoja na baadhi ya mambo muhimu katika apps hizo. App tutakazozizungumzia ni za bure tu, kwa vile hatuoni sababu ya kutumia app za kulipia kwenye eneo hili kutokana na ukweli kwamba app za bure zina ufanisi wa kutosha katika kusaka na kusoma habari za chaguo la msomaji.
Summly (iPhone tu): Samly sio tu haitumiki kwenye Android bali hata kwenye iPad hakuna app hii, isipokuwa tu kama uko tayari kutumia ki-app ‘kiduchu' kwenye skrini kubwa ya iPad ua iPad Mini au ukaikuza na kupoteza uzuri wa app yenyewe. Hata hivyo Samly ni app ya aina yake hasa kwenye suala la matumizi ya ishara katika utendaji wake, na muonekano wake ni wakuvutia kufuatia mchanganyiko wa rangi na , upungufu mkubwa wa app hii ni kwamba haikuruhusu kukusanya habari zako mwenyewe bali inakupa tu nafasi ya kuchagua aina ya habari unazozipendelea, hata hivyo app hii inauwezo mkubwa wa kukusanya habari kwa kutumia vigezo mbali mbali kama vile jina la kampuni, jina la bidhaa au jambo lolote ambalo linavuma ulimwenguni kwa wakati husika. Hivyo hii ni app kwa ajili ya wale wasiojua ni wapi pa kupata habari lakini wanajua aina ya habari wanazozipendelea, au wanaotaka kupata habari kutoka vyanzo vya ziada mbali ya vile wanavyovifahamu wao. App hiii imetolewa kwenye AppStore kufuatia kununuliwa na Yahoo hivyo wale tu ambao tayari wanayo ndio watakaoweza kuendelea kuitumia.
Google Currents (iOS na Android): Hii imetolewa na Google wenyewe, ajabu ni kwamba imeshindwa kupata umaarufu mkubwa. Huenda hii ndio sababu ya Google kuzima Google Reader. Google Current hupangilia habari kwa utaratibu wa kuvutia, inaruhusu kuchagua website ambazo zenye RSS kukuletea habari kwenye app hii, hivyo unaweza kuchagua cha kusoma na mtandao wa kuchukua habari uzipendazo. Upungufu mkubwa wa Google Currents ni kuwa na ugumu wa kuongeza habari ambazo zinatoka kwenye mtandao ambao sio maarufu sana. Hivyo kwa wale wanaosoma habari za mitandao maarufu peke yake basi hii ni app ya chaguo lao.
Taptu (iOS na Android): Taptu ndio app inayowezesha ku-customise habari kuliko app zote huku ikitumia kauli mbiu "DJ your news". Kwanza inaruhusu kuhukua habari za mtandao wowote, lakini zaidi app hii unaweza kufuatilia habari moja kutoka sehemu mbali mbali kwenye hub moja, kwa mfano unaweza kutengeneza hub itakayokueletea habari kutoka vyanzo mbali mbali kuhusu Samsung Galaxy S4 au kuhusu iWatch. Hivyo kwa wanaotaka kuchimba na kufuatilia kwa undani kabisa habari fulani muhimu basi app hii itawafanyia kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kabisa, kwenye Android app hii ina widget kuanzia mstari mmoja mpaka ukurasa kamili, chaguo ni lako. Hii ni app kwa wale wanaotaka kufuatia habari fulani kwa kina na wanajua wapi pa kupata habari, au wanafahamu ni habari gani wanataka kuifuatilia. Kwa watumiaji wa Mac Taptu pia hupatikana kwenye Nook, Blackberry na komyuta za Mac. Unaweza kutumia app hii kufuatilia kuanzia kutangazwa kwa bidhaa fulani hadi tarehe ya kuuzwa, matatizo yanayoikabili na hadi mwisho utakauchagua wewe mwenyewe.
Feedly (iOS na Android): Feedly ndio app inayosemekana kunufuaika zaidi na tangazo la kufungwa kwa huduma ya Google Readers kwa kupata wateja zaidi waliotumia app hiyo. Kwa mujbu wa wa CNet, Feedly imepata watumiaji laki tano zaidi tangu kutangazwa kufungwa kwa Google Reader, watumiaji wa Feedly hutakiwa ku-sign in kwa kutumia akaunti ya Google Reader au kufanya usajili. Uzuri wa Feedly mbali na urahisi wa kupata habari kwa wale ambao tayari ni watumiaji wa Google Reader lakini pia unaweza kubadili muonekano wa habari kwa kuchagua muonekano tofauti wa habari (mosaic, magazine, list na Cards) lakini pia unaweza kupangilia habari kama vile za zamani zikae mwanzo au mwisho, kuleta muonekano halisi wa website husika, kuchagua habari uzipendazo (kwa chanzo) zipewe kupau mbele. Hii ni app kwa wale wanaotaka kuhamisha moja kwa moja mambo ambayo walishayausanya kwenye Google Reader, au hata kwa wale wanaotaka kuanza upya.
Flipboard (iOS na Android): App hii haina tofauti sana na Feedly ingawa ina muonekano wa mtindo wa jarida (magazine view) huku ikitumia maboksi, kigodo ina ugumu wa kupata habari za mitandao ambayo sio maarufu, lakini app hii ni maarufu sana hawa kwa watumiaji wa simu na tableti za Galaxy zinazotolewa na Samsung kwa vile app hii huja "pre loaded" kwenye gajeti hizo. Flipboard pia ina uwezo wa kutumika kuangalia huduma mbali mbali za mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, youtube, linkedIn, Flikr, Instagram na kadhalika. Ikiwa bado hukutosheka pia unaweza kuitumia app hii kusomea vitabu (ebook), na kama bado hujaridhika basi unaweza kuitumia app hii kusikilizia redio za mtandaoni. Katka ubereshwaji (update) ulifanywa hivi karibuni, app hii pia inakuruhusu kuhifadhi (save) habari unazozipendelea na kuzisoma kwa mtindo wa jarida.Hii ni app kwa ajili ya wale wanaotaka kufanya mambo mengi kwenye app moja, au kusoma habari kwa pamoja bila ya kuhamishwa kwenye app nyingine za huduma hiyo kama vile Read it Later (Pocket).
Hivyo uwepo na ufanisi wa app kama hizi ndio hasa uliowapelekea Google kufikia uamuzi wa kufunga huduma hii. Google hutumia analytics kujua kama huduma bado ina wateja wengi au laa, bila ya shaka kupungua kwa watumiaji ndio sababu ya msingi ya kufungwa kwake lakini walichokuwa hawajaangalia Google ni kwamba watumiaji wa Google Reader wako addicted na huduma hiyo na ndio kilichopelekea watumiaji hao kuanzisha "petition"
Chanzo: Gajetek Habari: App Mbadala kufuatia Kufungwa Kwa Google Reader