Apandishiwa kodi kisa ndugu amekuja kutembelea

The Teacher

Senior Member
Feb 2, 2013
176
81
Nina ndugu yangu anasoma Memorial kigamboni, tumempangishia chumba maeneo ya kigamboni kwa urasa kodi ni tsh. 70000/= kwa mwezi per room. Sasa kuna mdgo mtu katoka mkoani kuja kukaa kidogo na Dada ake mama mwenye nyumba kapandisha kodi na kufikia tsh. 90000 / = mdgo angu kaniomba ushauri afanyaje but Ana kodi yake mpka mwezi June na mama nyumba kasema ajazilizie tsh. 20000 /= kwa kila mwezi.
 
Waliandikishana Mkataba kwamba kodi ni TShs. 70,000?..maana waTZ tupo vizuri kwenye kufanya mambo "kienyeji"

Kama ana mkataba, asilipe hiyo 20,000. Hata kama hakuna mkataba, akomae kibishi na amueleze mwenye nyumba kwamba huyo ni mgeni tu na si mpangaji mpya
 
Wanafunzi sina imani nao saaana.
Naimani huyo mama sio mjinga,mchezo huo niliufanya saana mabibo wakati ninachumba,nilibeba jamaa 4 kwenye room moja nikawa nakula nusu ya kodi ya nyumba kutoka kwao,nikajikuta kimahesabu silipi kodi na pesa ya kula juu.Yaani kodi ndani ya kodi aiseeee
Na kwanini asije kumtembelea wakati wa likizo?yaani akae hata mwezi mmoja,
Maana Tatizo la mabinti,unaweza kukuta muda mfupi huyu dada mgeni nae anaingiza wanaume humohumo inakuwa Double Standard.

Mie nakushauri mlipe tu kesi iishe,ukiwa hujakaa nyumba za wanafunzi huwezi jua,ila kuna siri kuuubwaa,mie shahidi
 
Asilipe maza akizingua aende mahakamani...katika Law of contract mkataba ni ule uliokubaliwa mwanzo na pande zote. Utatambulika mpaka ukiexpire Yaan ukiisha ndipo pande husika inaweza kuweka mashart mengine ktk mkataba mpya..Asilipe amshtaki kwa breach of contract!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom