BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 778
- 1,269
Wakuu Habari za Asubuhi
Kuna mambo mengi ambayo huwa yanakwama kwasababu ya kushindwa kuanza leo, watu wengi wamekuwa pale pale, miaka nenda rudi sababu ya kuahirisha kufanya mambo ambayo pengine yangewasogeza mbele kama Wangeanza kufanya jambo kwa wakati.
Watu wanaahirisha kuoa, watu wanaahirisha kusoma, watu wanaahirisha kujenga, watu wanaahirisha mambo mengi ambapo baadae wanakuja kujilaumu kwanini hawakufanya. Huu ni ugonjwa mkubwa.
Umewahi kuwaza ungeanza kutunza Tsh 100,000/= au 200,000/= au 300,000/= kila mwezi kwa miaka 5 iliyopita leo ungekuwa wapi? Vipi ukianza leo, baada ya miaka 5 ijayo utakuwa wapi kiuchumi. Achana na kiasi cha fedha, embu chukulia ungeanza leo kutunza/ku save angalau 15%/20% ya pato lako mwaka 2023 utakuwa na fedha kiasi gani? Anza Leo.
Anza Leo, panda miti leo kwenye shamba lako, ili miaka kadhaa upige hela. Najua ukiwaza mpaka mwaka 2025 ndio uvune miti yako utaona mbali sana. Lakini je, mwaka 2010 ungeambiwa panda miti yako ili uje uvune 2017,si ungeona ni mbali sana. Lakini huu ndio mwaka 2017. Kwa aliyekuwa na spirit kama hii mwaka 2010,leo anakula matunda.
Anza Leo kulima, Anza Leo kufuga, Anza Leo biashara, usiahirishe. Watu wengi wapo pale pale sababu ya kuahirisha.
Tarehe 30/11/2018 utajiuliza kwanini hukufanya leo, utajilaumu kwanini hukuanza leo.