Ansbert Ngurumo: Wabunge wadhalilishWe, DC alindwe??

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,214
22,992
Another objective masterpiece from Ansbert Ngurumo.....READ ON!

===============================================================================
Wabunge wadhalilishwe, DC alindwe?

By Ansbert Ngurumo


TUSEME ukweli. Yaliyompata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, akiwa kwenye “uhalifu wa kisiasa” juzi si mazuri hata kidogo.

Lakini ni vema ukweli wetu uvuke hapo. Tumtazame kama kiongozi wa serikali katika eneo lake, na tumuulize: alijiingizaje katika siasa za vyama vya watu?

Alitarajia akisaidia hujuma za Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wapinzani, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wangemshangilia na kumpaka mafuta?

Mikakati ya ushindi wa CCM ilikuwa inamhusu nini? Hakujua kuwa kwa kitendo cha kujifungia ndani na makada wa CCM, alikuwa anahujumu haki na kuhatarisha amani yake na wengine?

Na kama alitaka kuwahujumu CHADEMA, ilikuwa lazima awafuate katika eneo walikokuwa wamepangiwa mkutano wa hadhara? Haiwezekani ameponzwa na ubabe na jeuri ya cheo na ukada usio mahali pake?

Kama alikuwa katika mkutano halali wa kikazi, kama watetezi wake wanavyodai, yeye kama mwakilishi wa rais katika eneo husika, kwanini hakuwa na ulinzi wowote hadi vijana wa CHADEMA walipomwokota na kumpa kibano?

Kama alivyohoji mtu mmoja jana, kama DC huyo asingewafuata CHADEMA huko walikokuwa, wangemtoa wapi “kumdhalilisha”? Na kama wao wangekuwa wanatendewa haki huko nyuma, na hata katika uchaguzi wenyewe wa Igunga sasa hivi, wangepata wapi hisia na sababu za kuhoji kazi aliyokuwa anafanya kwenye mkutano wa ndani, na hata kumtia mbaroni?

Bila kujadili uhalali au uharamu wa hatua waliyomchukulia vijana hao, nilipoona picha magazetini, DC akiwa ameshikiliwa kama mwizi, huku akiangua kilio hadharani, na baadhi ya wananchi wakishangilia, kumbukumbu zangu zilinipeleka katika tukio la aina hiyo Januari 5, mwaka huu mkoani Arusha.

Na baada ya kusikia viongozi makada, wanachama na mashabiki wa CCM wakilalamika kwamba Fatuma amedhalilishwa; na hasa baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kujiapiza jana kwamba “sasa liwalo na liwe, na kitakachotokea wasilaumiwe,” nikalazimika kukubaliana na usemi wa wahenga kwamba mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Katika tukio la Arusha, polisi – mbali ya kujeruhi kwa risasi na kuua raia watatu – waliwatendea vibaya baadhi ya washiriki wa maandamano, wakiwamo wabunge na wake za watu.

Kwa mfano, polisi wa kiume walimpiga ngwara Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, akadondoka na kudunda kichwa chini kwenye barabara ya lami. Hakuna mwana CCM hata mmoja aliyeguswa na udhalilishaji huo.

Walimtwanga vitako vya bunduki dereva wa mbunge mwingine, Grace Kiwelu, wakavunja vioo vya gari na kumshambulia tumboni na kifuani.

Askari wa kiume walimshika vibaya na kumshusha suruali kwa nyuma, Josephine Mushumbusi, mchumba wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. CCM walishangilia matukio hayo kwa sababu aliyedhalilishwa hakuwa mwenzao!

Leo polisi Igunga wanahaha kusaka waliomshughulikia DC, lakini hawajamtia mbaroni polisi hata mmoja aliyemdhalilisha Lucy na Josephine miezi minane iliyopita.

CHADEMA walipolalamikia unyanyaswaji huo, na mengine ya kukamatwa kwa wabunge wao wengine, CCM wakasema huo ni ulalamishi tu.

Nina hakika, kama DC angekuwa kwenye kazi halali, hata angetaka kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CHADEMA, wasingemdhuru. Hata katika uchaguzi mkuu mwaka jana, wenzake kadhaa walifanya hivyo, wakapewa heshima kama viongozi wa serikali.

DC huyu amepatwa na masaibu haya kwa kuwa alijiingiza katika kampeni za kuibeba CCM; na bahati yake mbaya amenaswa katika mazingira yenye utata, akiwa na makabrasha yanayoonyesha dalili za hujuma za kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM.

Kwa watu walioonewa kwa muda mrefu, hakukuwa na hatua mbadala isipokuwa kumtia mbaroni na kumwondoa katika eneo husika. Yaliyoambatana na hatua hiyo ni mjadala mwingine ambao utatafutiwa nafasi yake.

Hoja hapa ni kwamba vijana wa CHADEMA wamepata ushahidi wa kuonyesha kwamba malalamiko yao ya siku nyingi si kulalama tu. CCM inataharuki kwa sababu aliyechukuliwa hatua ni kada wao.

Jeshi la Polisi linamwaga FFU mjini Igunga, kwa maelezo ya kulinda amani, lakini iwapo vijana watagundua nalo halitendi haki, hiyo amani haitalindika kirahisi – maana lazima wanaolindwa waone haki katika ulinzi huo.

Uhalifi hauchagui cheo cha mtu. Unaweza kufanywa na DC, polisi au wafuasi wa vyama. Na katika kauli hizi za “tusilaumiane kwa yatakayotokea,” ni dhahiri kwamba dalili za amani ya Igunga haziko karibu.

Lakini haya ni matukio yaliyoasisiwa zamani na watu wale wale waliokuwa wanashangilia matukio ya Arusha, huku wakibeza wanaolalamika.

Hawakuona ubaya wabunge “kudhalilishwa” lakini sasa wanaona haifai kwa mkuu wa wilaya kudhalilishwa. Nadhani, kama hawakumtuma, wangepaswa kumhoji kabla ya kumtetea.

Alikuwa anafanya nini katika siasa za wenye vyama vyao, yeye akiwa kiongozi wa serikali inayopaswa kutoa haki kwa vyama vyote?

Na sisi tunajiuliza, kama Nape ana huruma na anajali utu na heshima wanayostahili waheshimiwa hawa, kwa nini hakujitokeza Januari 5, kuwatetea wabunge waliodhalilishwa na polisi?

Na hili jeshi la vijana wa CCM wanalotaka kuliondoa kambini na kulimwaga mitaani dhidi ya CHADEMA, huku FFU wakiwa tayari wanarandaranda mitaani; lina hakika kwamba litalinda amani iwapo CHADEMA nao watatunisha misuli kwa nguvu waliyonayo ambayo hatujui mapana yake? Ndiyo amani na utulivu tunaoimbiwa?
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,214
22,992
moderators, hii thread imejirudia.
tafadhali muiunganishe na ile inayoendelea kule kwenye jukwaa la "hoja something"

originally nilli-post huku kwenye "jukwaa la siasa".... ilipogoma nikaihamishia kule kwenye jukwaa jingine.
 

Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
Watu wanaopenda mabadiliko wanapoona ccm na serikali yake wanatenda udhalimu huu wanafurahia maana ndiyo yatakayo harakisha ukombozi wao!
 

Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
'For every action there is equal and opposite reaction'


Watu wanaopenda mabadiliko wanapoona ccm na serikali yake wanatenda udhalimu huu wanafurahia maana ndiyo yatakayo harakisha ukombozi wao!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,498
64,949
Huyo polisi alikuwa na yeye anahamu ya kuona nini kimemzuzua Slaa ikabidi na yeye ajionee hayo Makalio ya Josephine.
Hoja ya kipumbavu hutolewa na mpumbavu. Asante kwa kujidhihirisha
 

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,561
11,336
Nape Nape Nape!!endeleeni na unafiki wenu nyie ndio binadamu wenye thamani peke yenu hapa Tanzania,wengine si binadamu wanastahili kunyanyaswa hata bila kosa lolote,huku nyie mkiguswa hata kidogo tu tayali mnawaleta vibaraka wenu FFU kupiga na kuua watu,I HATE ALL MEMBER'S OF CCM.
 

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,561
11,336
Nape Nape Nape!!endeleeni na unafiki wenu nyie ndio binadamu wenye thamani peke yenu hapa Tanzania,wengine si binadamu wanastahili kunyanyaswa hata bila kosa lolote,huku nyie mkiguswa hata kidogo tu tayali mnawaleta vibaraka wenu FFU kupiga na kuua watu,I HATE ALL MEMBER'S OF CCM.
 

Bigaraone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
723
351
Tatizo la ccm na vyombo vya serikali wanafiki Watanzania labda wanaishi ktk zama za utumwa na utwana ambapo haki ya mtu inaangalia cheo. Ndipo inaposhiikitisha kuona watu wanataka kutuaminisha kuwa dc amedhalilishwa kiasi cha mwanamke yeyote Tanzania. Polisi wanawakamata wabunge ambao ni chaguo la watu wanamwacha dc aliyekuwa anafanya kitendo cha hujuma. Hivi polisi wetu wataacha lini kufanya kazi zao kwa kufuata taaruma zao kuliko maagizo? Kwa nini wazuilie wabunge ambao ni chaguo la wananchi eti kwa sababu kadhalilishwa mteule wa rais. Mteule wa rais ni zaidi ya wawakilishi wa wananchi?

Kama ni kudhalilishwa ccm na serikali yake ndio inajidhalilsha kila uchao maana wanaacha mambo ya msingi-haki za binandamu, ajira na utu wa mtanzania wao wanasubiri kuwakamata wabunge kwa maagizo toka juu. Juu wapi huko kusikoheshimu nguvu ya umma? Ebu angalia mama ntilie wanavyoburuzwa na mgambo wakati wanatafuta riziki yao baada ya kugandamizwa na mfumo wa kinyonyji wa ccm. Agalia watoto wa kike wanavyotanda barabarani usiku wakiwa nusu uchi wapate riziki yao. Lini polisi na ccm wamekaa chini kuangalia namna ya kuwasaidia hawa. Angali madanguro ya ngono-moja limetaarifiwa na BBC kwa kirefu yanavyodhalilsha utu wa mtu. CD Igunga amekuwa zaidi ya hawa kina mama mpaka jeshi la polisi lipeke FFU watande mitaani kiasi hicho. Mei nafikiri polisi wasijidhalilishe kiasi hicho.Mlishadhalilshwa vya kutosha na nyie ni wakati wenu kuamka mtoke ktk giza nene la fikra mjue mbele ya haki hakuna rais, ccm, dc au igp. Haki ni natural phenomenon haingalii cheo cha mtu. Na mbele ya Mungu sote ni binadamu.Mtaamrishwa kuwa chapa hao wapinzani virungu lakini mjue nyie sio roboti.Mna akili, mna utu, mna ubongo. Tumieni vipaji hivi. La sivyo malipo ni humu duniani.Tutwashitaki kwa Mungu
 

twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,100
2,786
Ninashaka kama akili za A.Ngurumo zinaunguruma.DC ALIINGILIA VIPI MKUTANO WA CDM?.DC ALIKUTWA NDANI YA CHUMBA TENA OFISI AMEKAA AKIWA NA VIONGOZI WENZAKE.SASA NAJIULIZA MUDA ALIUTOA WAPI WA KWENDA KUVURUGA MKUTANO WA CDM.CDM NDIO WALITOKA KWENYE ENEO LA MKUTANO NA KUMFUATA DC NA KUMDHARIRISHA KITU AMBACHO WANANCHI TUSIOTUMIA MAJAN YA JA...CA HATUKIKUBARI.NASEMA NGURUMO ACHA KUTETEA KITUMBUA CHAKO HAPO TANZANIA DAIMA,HAWATAKUPA UBUNGE WA VITIMAALUM MAANA NI KWA WANAWAKE TENA WAKE ZAO KAMA ROSE...WA SILAA
 

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
Ninashaka kama akili za A.Ngurumo zinaunguruma.DC ALIINGILIA VIPI MKUTANO WA CDM?.DC ALIKUTWA NDANI YA CHUMBA TENA OFISI AMEKAA AKIWA NA VIONGOZI WENZAKE.SASA NAJIULIZA MUDA ALIUTOA WAPI WA KWENDA KUVURUGA MKUTANO WA CDM.CDM NDIO WALITOKA KWENYE ENEO LA MKUTANO NA KUMFUATA DC NA KUMDHARIRISHA KITU AMBACHO WANANCHI TUSIOTUMIA MAJAN YA JA...CA HATUKIKUBARI.NASEMA NGURUMO ACHA KUTETEA KITUMBUA CHAKO HAPO TANZANIA DAIMA,HAWATAKUPA UBUNGE WA VITIMAALUM MAANA NI KWA WANAWAKE TENA WAKE ZAO KAMA ROSE...WA SILAA
usije shitakiwan for defamation kwa usilolijua..............huh
 

Bigaraone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
723
351
Nape wewe umekuwa nani ktk tasinia ya siasa na haki za nchi hii. Kupewa cheo uchwara kuwa propangist wa chama cha magamba haikufanyi kuwa na akili sana. Tunaujua ukilaza wako tokea Bangalore ulipokuwa na Mzumbe Sekondari unaposoama kwa kusuasua. Hujawahi kuwa na akili bali mtu wa kujipendendekeza, mlaghai, mnafiki na mzabizabina. Polisi mnaowachochea wabebe virungu na silaha za moto dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia ni zao la mfumo gandamizi. Mnatumia frustrations na ujinga wao kama mtaji wa ccm. Kwa sababu ya malipo duni na kushindwa kuijua kesho wnaishi kutii amri bila kutumia bongo.Mnafikiri wanawaheshimu. La sivyo ni njaa yao. Tunawaona kila tupitapo polisi wanvyoishi ktk uduni wnua maisha na fikra. Daladala wapande bure, kwenye maduka yao vitu bei rahisi na mtaani watuombe lifti na beer. Huu ndio udhalilishaji kuliko wa kukamatwa dc. Lakini yote yana mwisho.Kuna siku watachoka na kutumia silaha zao dhidi yenu. Bi indhira Gandhi aliuawawa na walinzi wake waliokuwa watiifu kwake miaka nenda rudi, siku ilipofika walichoka. Mdogo wake rais wa Karzai wa Afghanistan ameuawawa na mlinzi wake. Fundisho kwa kina Nape. Natumai polisi wetu wanatakiwa kuamka kutoka kwenye vichaka vya fikra
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

7 Reactions
Reply
Top Bottom