Ansbert Ngurumo humtendei haki rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ansbert Ngurumo humtendei haki rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kipepeo, Dec 2, 2009.

 1. Kipepeo

  Kipepeo Senior Member

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 186
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimelazimika kujibu makala ya ANSBERT NGURUMO nikiamini kwamba kama ilivyo kwa binadamu wote akiwemo NGURUMO mwenyewe wana mapungufu ya kibinadamu. Msingi wa mapungufu haya ndiyo hatua muhimu ya binadamu mwenye busara kukubali ukweli kwamba hakuna binadamu aliyekamilika.

  NGURUMO aliandika makala ya kubeza uamuzi wa Rais KIKWETE kuzungumza moja kwa moja na wapigakura wake kama alivyofanya kwa mara ya kwanza tarehe 9 septemba, 2009. Hoja za NGURUMO ni dhaifu na zenye kujaa zengwe la jambo lililojificha nyuma ya mashambulizi ya NGURUMO dhidi ya Rais KIKWETE kama nitakavyofafanua baadaye.

  Kwa wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia maandiko kadhaa ya NGURUMO dhidi ya KIKWETE wanajiuliza kulikoni? Zipo taarifa kuwa NGURUMO ni mmoja wa majeruhi wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, ameamua kuendesha siasa za fitina kwa mlango wa nyuma huku akidai anafanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

  Wanaokujua wanadai kuwa wewe ni mhanga wa siasa za ukimbizi kutoka chama kimoja kwenda kingine kufuata maslahi binafsi kutokana na tabia hiyo umejikuta unajenga chuki dhidi ya marafiki zako wa zamani.

  Wapo wanaodai kuwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005 NGURUMO ulikuwa mmoja wa waandishi wa habari mahiri waliomkubali KIKWETE na hivyo kufanyakazi ya ziada kuueleza umma wa Watanzania kumchagua mgombea huyo. Hata hivyo, watu wa karibu na wewe wanaeleza kuwa mahala na wakati fulani baada ya uchaguzi huo ulitarajia kulipwa fadhila ya kazi hiyo hasa kupewa nafasi ya uongozi katika utawala wa awamu ya nne ingawa hatujui kama wewe ni chaguo la Rais.

  Nalazimika kujiuliza pengine elimu ya NGURUMO imeanza kuyeyuka kwa namna anavyoweza kutumia kalamu yake vibaya pale aliposema Rais KIKWETE anahusudu usanii kwa sababu ya uamuzi wake wa kuongea moja kwa moja na wananchi na wapenzi wake wa kisiasa. Rais ni wa wananchi wote na anapofanya jambo kubwa kitaifa anashauriana na washauri wake na wale wa chama chake cha CCM ili kupata msimamo mmoja. Hata NGURUMO kuwa na mtazamo huu siyo kosa kisiasa unaweza kuwa unasimamia mtazamo wa CHADEMA na gazeti la Tanzania Daima kuwa Rais atakayetoka upinzani hataruhusu kuulizwa maswali na wananchi.

  Kama kweli NGURUMO mzalendo tungependa nasi kupata vielelezo vya ujumbe mfupi wa simu (SMS) unaodai ulitumwa kwa wingi na wapambe wa Rais KIKWETE kuonyesha kwamba ndiye mgombea anayeungwa mkono zaidi katika kura za maoni za mwaka 2005 eti wakati sivyo. Vielelezo hivyo vinaweza kuwa namba za watumiaji ili wananchi waweze kuchambua. Hizi ni propaganda zinazolenga kuonyesha kwamba Rais KIKWETE hakuwa lolote katika mchakato huo.

  NGURUMO kuja na hitimisho la udanganyifu wa kura hizo bila vielelezo kutoka kampuni ya simu iliyoendesha kura hizo za maoni ni propaganda za kisiasa. Ni vyema NGURUMO akajua kuwa kura hizo za maoni zinaratibiwa na kampuni ya simu ili kupata chanzo kimoja cha kura husika, hivyo mtu mmoja akipiga kura ya maoni zaidi ya mara moja hakuna ubishi kwamba kampuni husika haiwezi kukwepa kulaumiwa. Wote tungependa kujua kampuni ya simu iliyoendesha kura za hujuma na kwani inapaswa kushitakiwa kwa vielelezo alivyokusanya NGURUMO.

  NGURUMO anadai alipokea bahasha kutoka kambi ya KIKWETE ili kuandika habari nzuri za kambi yake katika gazeti la Tanzania Daima. Tanzania Daima ni gazeti la CHADEMA na kambi ya KIKWETE ni ya CCM inahitaji ujasiri wa kijinga kuamini kuwa kambi ya CCM ilipeleka bahasha kwa mhariri wa gazeti la CHADEMA, kwa maana ya NGURUMO ili CHADEMA waiandike vizuri CCM. Si hivyo tu wakati huo huo CHADEMA ilikuwa na mgombea wake katika uchaguzi huo, kwa maana ya FREEMAN MBOWE. Kama kweli hiyo ilitokea basi hatuna budi kuamini kuwa bahasha aliyopewa NGURUMO haikuwa na jambo jipya bali kulijaribu gazeti la CHADEMA kama litaweza kuandika habari nzuri za CCM.

  Kusambaza taarifa kwa njia ya bahasha kwa vyombo vya habari kuujulisha umma kwamba KIKWETE kashinda kura za maoni za BBC haliwezi kuwa jambo baya katika uchaguzi au ni kwa sababu KIKWETE hakuwa mgombea wa CHADEMA?

  NGURUMO una propaganda za kufikirika kwamba Rais KIKWETE alitumia vyombo vya habari vibaya kuwamaliza wengine kisiasa. Nina hakika kambi ya CHADEMA na mgombea wao wa Urais pia walitumia vyombo vya habari kumuuza mgombea wao na bado wanaendelea kutumia vyombo hivyo ikiwemo gazeti la Tanzania Daima kujiimarisha na kujitangaza kwa wananchi. Hatua hizi hazikwepeki kisiasa ambapo magazeti ya CCM yanaandika mazuri ya CCM na ya CHADEMA mazuri ya CHADEMA.

  NGURUMO wananchi wa kizazi kipya cha siasa za sasa ni wadadisi na wapenda kujua mambo kwa undani, hivyo hotuba za Rais pekee haziwezi kujenga mahusiano mema na wananchi. Hiki ni kizazi cha teknolojia ambapo binadamu wanapashana habari kwa kasi ya ajabu tofauti na huko nyuma. Mkuu wa nchi asipowapa wananchi taarifa muhimu na kupata maswali kutoka kwao ni sawa na kuruhusu kuaminika kwa taarifa za mitaani ambazo zinaweza kupotoshwa na vyombo vya habari, watu aina ya NGURUMO wakiwemo wapinzani kwa minajiri ya kisiasa.

  Kambi ya akina NGURUMO inataka kuwa na jukwaa lao la kusemea lakini haitaki wenzao wakapata jukwaa kama hilo, ni kama hivi NGURUMO kamsema Rais lakini hataki siku ikafika akaulizwa ukweli wa propaganda za akina NGURUMO. Hali hii inaweza kuwa moja ya sababu za kambi ya akina NGURUMO kuzidiwa kete na kushitushwa na umaarufu atakaopata Rais kupitia kipindi cha Muulize Rais hasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2010.

  Rais si mtu binafsi ni taasisi na kuonyesha kwamba kipindi cha Muulize Rais kilipokewa vizuri ni kujitokeza kwa zaidi ya watanzania 7000 kumuuliza maswali ya papo kwa papo. Mtindo huu pia hutumiwa na nchi zilizoendelea katika kuimarisha haki za binadamu na utawala bora. Wataalamu wa mambo ya siasa wamekuwa na hoja kwamba umbali uliopo kati ya Rais na wapiga kura wake ni mrefu wenye kujaa urasimu unaokinzana na mbio za kampeni za uchaguzi ambapo mgombea anaongea moja kwa moja na wapiga kura wake.

  Hoja hapa ni kwamba, Rais wa nchi anatakiwa kuwa karibu na wananchi kadri inavyowezekana hata baada ya kuukwaa Urais. Dunia ya kisasa imeanza kumuona Rais kuwa ni Kiongozi Mkuu wa nchi anayejishusha na kuwasiliana na wananchi bila kujali hadhi na tabaka lao. Wananchi wanatakiwa kujisikia kuwa Rais ni mtu wao kama ambavyo inakuwa wakati wa kuomba kura. Mtazamo wa NGURUMO haukubaliki kwa viongozi wa kuchaguliwa na wananchi.

  Kitendo cha Rais kuongea na wananchi moja kwa moja kilifuatiliawa na nchi vyingi kama vile za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DR Congo na pia kupitia mabalozi na mashirika ya kimataifa. Taarifa mbalimbali kutoka maeneo hayo zilitolewa na kumpongeza Rais KIKWETE kwa kuthubutu kutenda kile ambacho Marais wengi hususan wa Afrika hawajakifanya.

  NGURUMO huwezi kutia maneno yako mdomoni kwa Rais eti hawaamini wasaidizi wake ndiyo sababu kaanzisha kipindi cha Muulize Rais, hizi ni fikra za kale zilizoambatana na uzamani ulioachwa nyuma na utandawazi. Kipindi cha Muulize Rais siyo kwa ajili ya kujua matatizo ya wananchi kupitia vipindi vya Radio na televisheni kama asemavyo NGURUMO na wala vipindi hivyo si dawa ya matatizo kama unavyodai lakini kinaweza kuwa jukwaa huru lenye nia njema kuelekea kutatua matatizo kwa njia ya uwajibikaji wa pamoja. Hivyo Rais alikwenda pale kupata kujua moja kwa moja wananchi wanafikiri nini kutoka vinywa vyao kisha kuwa na maamuzi sahihi juu yao. Nikiwa Mtanzania nafarijika kuwa kipindi cha Muulize Rais ni njia nyingine nzuri ya kupooza hasira za wananchi wanaoona serikali haina majibu na inashindwa kufanya kazi.

  Hapana shaka, mtindo wa Rais wa kutoa majibu ya nyongeza, kwa mfano jibu la barabara ya Kigoma na kuongeza maelezo zaidi katika barabara za maeneo mengine nchini yanaonyesha Rais ni Kiongozi wa wote. Rais alitaka kuonyesha kuwa kucheleweshwa kwa barabara za Kigoma kusiwe kigezo cha kushutumu kuwa serikali yake haijafanya kitu katika sekta ya barabara bali wakati inajipanga kufanya hivyo Kigoma wakati huo serikali ilikuwa Lindi na kwingineko nchini. Hili siyo kosa katika kujibu maswali kama ambavyo NGURUMO anasema kuwa Rais anakwepa swali. Hapa Rais alisaidia pia kuondoa hali ya kujirudia kwa maswali ya aina moja kutoka mikoa tofauti ambapo wananchi wanauliza katika jambo moja hilo hilo.

  NGURUMO, tuambia ni nchi gani duniani yenye sheria ya kumzuia Rais kuteua rafiki katika uongozi kama anatimiza vigezo vyote na sifa stahiki. Hoja hapa ni kwamba, Rais kumwamini rafiki ambaye baadaye anamwangusha ni jambo lingine na hili pia huweza kutokea kwa mtu asiye rafiki wa Rais hata kama alichaguliwa kwa kufuata ushauri . Ni vyema tukajadili kwa kiasi gani sifa za rafiki (ikiwemo uadilifu) zilikuwa hazitoshi kuliko kujadili ni kwa nini alimpatia nafasi ya uongozi rafiki yake. Hali hiyo ipo na kwingineko duniani ingawa wenzetu katika nchi zilizoendelea wamefanikiwa zaidi kutenganisha kazi na urafiki jambo ambalo tunahitaji kujifunza. Kwa mfano, Mwanasheria Mkuu wa Marekani ni rafiki mkubwa na wa siku nyingi wa Rais BARAKA OBAMA pia Barozi mteule wa Marekani nchini Tanzania ni rafiki na Swahiba mkubwa wa Rais OBAMA.

  NGURUMO wananchi wa kizazi kipya hawadanganyiki unaposema kwamba maswali kwa Rais yalirekodiwa kabla si jambo tunalohitaji bali ukweli na usahihi wa majibu ya Rais kwetu ndiyo hoja ya msingi. Swali linaweza kuwa halijarekodiwa lakini likajibiwa kwa uongo ni nini faida yake kwa wananchi?

  NGURUMO anatuambia kipindi kilimdhalilisha Rais. Si kweli, naamini kipindi cha Muulize Rais kimemjenga Rais kuliko kumbomoa kama ambavyo NGURUMO anataka tuamini. Rais hakuja na jambo jipya alitaka wananchi wake wasikie kauli ya mkuu wa nchi kuhusu matatizo ya nchi na kisha kumwachia kila mmoja kuhakiki kwa viwango vinavyozidiana. Uwezo wa kupima mambo ni wa kila mmoja wetu.

  NGURUMO, kumbuka pia kwamba, uendeshaji wa vipindi hutofautiana kutoka redio moja kwenda nyingine na televisioni moja na nyingine, si vyema kulinganisha kipindi alichokuwa anaendesha TIDO MHANDO akiwa BBC na Kipindi cha Muulize Rais. TBC Rais alikuwa anapokea maswali kwa wananchi na kipindi cha MHANDO cha BBC kilikuwa cha mtangazaji kuwahoji viongozi maarufu ambapo mtangazaji anakuwa msemaji mkuu.

  Naomba kupimwa kwa hoja na siyo hoja hizi katoa nani.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  1.Mkuu weka kwanza hiyo link ya Ngurumo alizungumza nini ili watu wapate mwanga wa uliachokiandika hapa.
  2. Simpendi kabisa Ngurumo baada ya kuwa mmoja wa wabakaji wa demokrasia ndani ya Chadema.
  3.Ila kwa haraka haraka nilipopitia hoja zako inaonyesha Ngurumo yuko sahihi , nitaconfirm tu nikijua kwa kina aliandika nini!

  Hoja zako inabidi uziangalie tena ili kuepusha matusi tena ya nguoni, kumtetea JK inataka moyo ndugu!Ukiweza kutetea uozo wa JK ambao uko wazi kabisa unaweza kutembea sokoni kariakoo uchi mchana kweupe!

  The best way was to verify and seek more information on what Ngurumo said.BBC,REDET na baadhi ya magazeti kuwa vilimbeba JK sio siri iko wazi,kabisa!

  wakati unatuwekea link, naomba pia kukuuliza watanzania milioni 40 wakiwa na simu za mkononi wote wakatuma meseji kwa Rais atazisoma kwa siku ngapi??

  Pia katika aliyoulizwa alijibu mangapi? kwa usahihi na kutatua tatizo??

  marais wenzake huwa wanaweka debate, mihadhara, atafute siku aende UDSM, SOKOINE, public places aseme tunakaa na kuongea wamuulize maswali ana kwa ana, angalia Obama.

  Ishu ile ya simu je ni mkakati mwendelezo au ilitokea bahati mbaya tu?

  Haikuhitaji kusoma nakala ya Ngurumo kujua kuwa ishu ile JK alikuwa msanii! kabla Ngurumo hajaandika wengine tulishajua; kuwa JK msanii

  Alichofanya ni kupata akili ya mtanzania ambaye atafikiri rais kweli anaipenda NCHI HII kwa kutatua matatizo kupitia simu!

  Umeshawahi kukutana na aliyetuma meseji kwa Kikwete??kalaghabaho!
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,356
  Likes Received: 3,121
  Trophy Points: 280
  ngurumo anamtendea haki rais kulingana na hali halisi ya jinsi anavyo endesha nchi..................
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna mtu anayemtendea haki Jakaya zaidi ya Ansbert Ngurumo kwa sababu yeye sio mnafiki bali anamwambia Rais ukweli wa mambo kama yalivyo unlike Salva na genge lake ambao wao wapo kumwambia mwajiri wao uongo [ mfano ni juu ya WEBSITE ya Ikulu] ili mradi waweze kubaki na kupata safari za nje na mkuu zisizo isha; sasa hivi yuko Cuba huku watu wa TRL wanakufa na njaa hawajapata mishahara yao ya Mwezi uliopita!!
   
 5. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Kipepeo
  Jinsi ulivyobwabwaja hapa inaonekana kabisa humjui Ngurumo katika historia yake ya uandishi.

  Rudi nyuma kafanye homework.

  Kalamu ya Ngurumo ni sumu kubwa kwa watawala vibaraka, mafisadi na wababaishaji. Wapambe wao wameshaanza kujipanga kumponda. Na wengi wengine wanakuja.
   
 6. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #6
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona badala ya kumpa kazi kipepeo kuhusu historia ya Ngurumo wakati ameeleza upande wake anavyomjua ni vyema Invincible ueleze unachokijua kuhusu Ngurumo ili wanajf tuweze kutoa michango yetu barabara.
   
 7. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kama umesoma vizuri post ya kipepeo ina mantiki kwani anazungumzia tukio moja tu la Rais kuongea na watanzania moja kwa moja kwamba Ngurumo hajatenda haki anaposema rais alifanya vibaya kuongea na wananchi. hata hivyo, hakuna ambapo kipepeo kamsifia rais bila shaka anajua kama binadamu yapo mazuri na mabaya katika utawala wake jambo ambalo siyo baya. Namna hapa Tanzania ni MBOWE tu ambaye hana mabaya anayofanya. Je katika jamvi hili ni mwiko kumsifu Kikwete hata kama kafanya mazuri?
   
 8. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Na wewe acha kufinyanga, kabla ya kuelewa. Katika maandishi ya mtoa hoja, ameingiza mengi tu, ya hata kabla JK hajaukwaa uraisi. Yote hayo yakionyesha Ngurumo hamtendei haki Kikwete.

  Mtamtetea wee JK, lakini raisi bomu anabaki kuwa raisi bomu tu.
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Acha uvivu. Unataka ku-desa mpaka JF?

  Kuanzia j2 tenga sh 400 ununue gazeti la Tanzania daima. Kuna safu ya Ngurumo humo. Sikushauri sana kuingia website yao, kwa sababu ya update. Ila website ina mazuri yake kwa habari ya archive.
   
 10. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mi naamini uhitaji hata kufika std three ili uweze kupima uwezo wa Mkuu wa Kaya kuongoza nchi hii!!

  Sioni haja ya yeye kuandaa midahalo pale UDSM or else where, kwanza ili iwe nini?? Je tunahitaji midahalo kupima utendaji wa miaka 4 iliyopita?

  Haya ndo yale ya REDET kusema 80% ya wananchi hawaridhishwi na utendaji kazi wa baraza la mawaziri lakini 90% wanaridhishwa na utendaji kazi wa raisi. Huu si usanii wa kutaka kufurahishana? Iweje baraza la mawaziri liwe bovu afu mwenyeketi wake awe mzuri na mahiri?
   
 11. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Yataka moyo kumtetea mkulu wa nchi hasa kwa kuangalia hali halisi ya nchi. Kuongea na wananchi kwa njia ya redio, tv siyo mbaya lakini usanii unaweza kutumika na zikapokelewa simu za watu wasio na hoja makini huku hoja nzito zikitupwa kapuni kwa kisingizio kuwa message zilikuwa nyingi mno na Mkuu hakuweza kuzijibu zote.

  Akitaka kupata issues basi iandaliwe midahalo ambayo itakuwa na maswali na majibu ya moja kwa moja kama mjumbe mmoja alivyoshauri hapo juu.

  Lkn ni ukweli ulio wazi kuwa "Kile Kipindi Kiliindaliwa kama take-off ya kampeni za 2010" na hata mpangalio wa maswali ulilenga kumpa uwanja mheshimiwa wa kujaribu kuelezea mafanikio ambayo hayaonekani kwa macho.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kipepeo upo sahihi,

  Ngurumo ni majeruhi, kila jambo analofanya Rais ni kibaya kwa mtazamo wake. Hakuna ubishi inaeleweka vyema kuwa anatumia kalamu yake kumsakama mkuu wa kaya hata katika mambo mazuri. Ngurumo anasomeshwa na MBOWE Hull University Uingereza unategemea atamsema vizuri Rais? JF ni jukwaa huru acha washiriki wajadili kwa uwazi mazuri na mabaya ya Rais na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli na ukomavu wa fikra.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kipepeo upo sahihi,

  Ngurumo ni majeruhi, kila jambo analofanya Rais ni baya kwa mtazamo wake. Hakuna ubishi inaeleweka vyema kuwa anatumia kalamu yake kumsakama mkuu wa kaya hata katika mambo mazuri. Ngurumo anasomeshwa na MBOWE Hull University Uingereza unategemea atamsema vizuri Rais? JF ni jukwaa huru acha washiriki wajadili kwa uwazi mazuri na mabaya ya Rais na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli na ukomavu wa fikra.
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Dec 3, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kikwete anatendewa haki natena maneno hata anayoambiwa na A.Ngurumo na manno laini tu, mimi naamini huyu rais angekuwa kwenye utawala wa Uingereza ya kina Blair leo angekua kisha pigwa mayai viza na nyanya mbovu kitambo tu.
  unajua waliokulia zama za wanasiasa miungu watu 1960-80s hali hii ya kukosolewa Rais inawasumbua sana, wachache tumeweza kubadilika wengi bado ni waoga wanadhani kumkosoa Raisi ni sawa na kosa la uaini.
   
 15. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Okay tuseme Ngurumo ana bifu na Rais. Je na wakina Mzee Butiku, Warioba, Ask. Kilaini wanamchukia Rais kama vile tulivyoona wanamkosoa Rais JK katika kongamano? Tukubali Ngurumo ni mwiba katika serikali ya JK lakini ni kwa nia njema kabisa.
   
 16. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kwanini mnasumbuka na watu kama Ngurumo?

  tafuta definition ya neno parasite..

  kazi yake kubwa ya pili ilikuwa ni kumfanyia mitihani mwenyekiti,bahati mbaya mwenyekiti Elimu haimpendi!

  suala la kumponda mkuu na utaratibu huu ni suala la kipuuzi!
   
 17. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Vichwa-panzi hujadili watu,vichwa vyenye ubongo hujadili ishu.That summarises your silly arguements.Na huyo rais unayemtetea amewatendea haki gani Watanzania tangu aingie madarakani 2005?Kutulutea Rchmond?Kuilea Kagoda?Kuwalinda Rostam-Lowassa,Chenge,nk?Kusafiri kama Vasco da Gama kila kukicha?

  Hoja zako zimepimwa lakini ni mufilisi kama uwezo wa uongozi wa huyo unayejikomba kwake.
   
 18. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kweli Ngurumo ni Majeruhi ila kuna mengi anayosema yana ukweli.
   
 19. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tatizo la huyu jamaa njaa inamsumbua.kila akielekezwa na bosi wake MBOWE anasikiliza.hivi sasa anabeba mabox Uk.
   
 20. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  baada ya kazi ya kumfanya assignment Mwenyekiti kuisha.sasa kazamia anabeba mabox.
   
Loading...