Ansbert Ngurumo amchana Kikwete live...


TOPICAL - kama alienda shule - aliondoka bila kujua maana ya neno TAFITI (reserach), na aina za utafiti. Vile vile, amekulia na kulelewa katika makundi dhaifu yenye kujaza bongo za watoto sumu ya UDINI. Sijaona popote katika makala ya Ngurumo, alipojadili Uislamu na Ukatoliki wa mtu yeyote. Nyerere alishasema kuwa watu waliofilisika, wanapokosa hoja wanakimbilia DINI na MAKABILA...
 
Kama kawaida yetu wanafiki na waoga, aidha tunabaki kushabikia au tunaogopa usalama wa taifa kusema ukweli. Tatizo haliko kwa mgeni aliye ndani ya nyumba bali lipo kwa mwenyeji aliyemkaribisha ndani ya nyumba. Tu wavivu wa kufikiri mpaka kutenda, vidili vyetu vya lakilaki ndio vinatufanya tubaki kuwa washangiliaji pindi mtu akisema ukweli. Hatuna tofauti na JK, kazi yetu ni kulalamika kila siku wakati mamlaka na uwezo wa kufanya maamuzi tunao.Wanafiki sana sisi
 

Kwani wananchi wa TZ walimchagua Ngurumo aongoze familia yake? Huu ni mfano mbovu, unalinganisha mtu aliyechaguliwa na mamilioni ya waTZ na mambo ya ndoa ya mtu? Familia ya Ngurumo ni personal issue, urais na rais ni public issue na ndio maana rais anapigiwa kura ili atuongoze, mme/ke hapigiwi kura ili aiongoze familia yake.
 

This is very low. Sasa suala la dini linaingiaje hapa? Wewe ndiye unayeonesha kuwa una hisia za kidini ambazo ziko misplaced. Na watu wa aina yako ndio mnaomfanya hata JK aimbe suala la udini ambalo halipo. Ni udhaifu mkubwa sana kujificha kwenye kivuli cha udini kila mnapoambiwa ukweli. Inaonekana dhahiri kwamba baada ya kusoma haya MASWALI MAGUMU ya Ngurumo umeumia sana kwani ni ukweli mtupu. Njoo na hoja inayoonesha dosari kwenye article hii badala ya kukimbilia kwenye huu ujinga wa udini.
 
Ingekuwa vizuri zaidi kama ungetuonyesha ni zipi personal attacks za mwandishi kuhusu Kikwete na kama hoja yake haina mshiko. Ungetusaidia sana hapa nyumbani kwa Great thinkers. Lakini badala yake umejitumbukiza kwenye shimo la udini. Mwandishi katoa points zake, zisute moja baada ya nyingine siyo tu ku-generalize kuwa makala imejaa personal attacks.
 
Ukweli alio usema ni upi? taja walau ukweli moja kwenye hiyo article

Ninachokisema ni kwamba ameeleza hisia, chuki zake binafisi na JK kama vile alinyimwa cheo hivi au sijui!

Ujing wa udini anao yeye ansbert sasa ajitazame mwenyewe kama mwandishi aandike ukweli siyo kuandika huku umesukumwa na wingu la ukatoliki..ila hawatusumbui siku hizi hawa

Uchaguzi uliopita wakatoliki wameumizwa sana baada ya kupiga kampeni kwenye vikao vyao vya kibaguzi mitaani wakashindwa wamekasirika wanaropoka ovyo kama ansbert afanyavyo..
 

Idadi ya watu kama wewe ikiongezeka kidogo, hii nchi itabaki kuwa historia na sehemu kubwa ya ardhi itapanda watu na sio mazao
 

Bah... Suala la familia ya Ngurumo na masuala ya uongozi wa nchi wapi na wapi bana? Hebu tupishe huko...
 


Duh! Kaaazi kweli kweli... Haya bana umeshinda wewe. Lazima utakuwa na uhusiano na gazeti la ANNUR.
 

1. Anaposema wanaomjua udhaifu wake...(bila kusema kina nani) ..hiyo ni hisia, streotype mazungumzo ya watu waliokasirika baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wengi wao wakatoliki hasa maaskofu waliotaka ashinde mtu wao..wananchi wakahukumu tofauti sasa wanavumisha eti rais ni dhaifu..kumbe wameumizwa tu akiwemo ansbert kwenye boti la wakosaji

2. Sehemu zingine zote za makala yake ameongolea management style ya JK, analinganisha na yeye anavyotaka anavyofikiri (hisia, utashi, mtizamo) hajui goverments operation hana evidence yeyote katika makala kwa ujumla ni malalamiko ya wakosaji. JK style yake ni kushtaki viongozi kwa wananchi ili wawe na uhuru wa kuuliza, kujadili na hata kuwaadhibu katika maeneo mbalimbali tofauti na Mkapa ambaye style yake ni kuwatetea, kuwalinda viongozi kwa kuwatukana kuwakashifu wananchi....

3. Mwandishi hatakiwa kuwa mlalamishi bali kuandika analysed opinion..kazi ya kulalama tunamfahamu mtaalamu wa hili (Slaa Phd) kwenye mambo ya kanisa anafahamu sana hiyo
 
Duh! Kaaazi kweli kweli... Haya bana umeshinda wewe. Lazima utakuwa na uhusiano na gazeti la ANNUR.

Kwani ni dhambi kuwa na uhusiano na gazeti hili la Annur?

Je Gazeti Annur si gazeti la Watanzania?

Vipi wewe una uhusiano na gazeti la kiongozi na Nyakati? au Tanzania Daima?
 
Kwani ni dhambi kuwa na uhusiano na gazeti hili la Annur?

Je Gazeti Annur si gazeti la Watanzania?

Vipi wewe una uhusiano na gazeti la kiongozi na Nyakati? au Tanzania Daima?

Si lawatanzania ni la Kidini zaidi lile...
 
Nakumbuka ngumi za utotoni ukiona unashindwa ngumi za kavu kavu unaokota mawe....ndo Chama Cha Magamba hao...wanaishiwa hoja za kujibu wanakimbilia ukatoliki!!!
 
Anaposema wanaomjua udhaifu wake si lazima akutajie majina. Katika taaluma ya uandishi inaruhusiwa kuficha sources zake. Kama amezungumza na watu walio karibu naye je, na hawakutaka watajwe? Mbona mimi nimewahi kuzungumza na waziri mmoja wa Kikwete akimponda ajabu lakini hawezi kusema hayo hadharani? Management style ya Kikwete inafahamika. Angalia alivyosimamia kikao cha NEC cha kuwashughulikia mapacha watatu. Yeye kama CEO alitakiwa atoe maamuzi bila ya kusema tumekubaliana hiki tumekubaliana kile. Halafu siku chache baadaye hata hayo waliyokubaliana wanaanza kuyakana. Badala ya kuwafukuza hao mapacha watatu anawapa nafasi ya kujiamulia wenyewe kama wajifukuze. Ulishasikia wapi CEO wa aina hiyo? Badala ya kuwafukuza mawaziri ambao anaona wanaiharibia serikali yake anawaambia wajiondoe wenyewe. Ulishasikia wapi? Kuna mifano chungu mbovu ya uzembe wa Kikwete katika ku manage masuala ya utawala. JK alipewa mamlaka na wananchi achukue maamuzi magumu. Kazi yake si kushtaki viongozi wenzake kwa wananchi eti wawe na uhuru wa kuuliza. Kuuliza nini? Si afadhali awafukuze kwanza halafu aje awaeleze wananchi sababu zilizompelekea kuwafukuza? That is leadership!
 
Reactions: Bob

Good analysis, pongezi kwakuwa sober nakueleza fikra zako kwa busara umewapita wanachadema wengi akili akiwemo yule mungu wao...

Back to leadership style, JK anachotaka ni capacity building hasa kwa wananchi katika kufahamu, kujadili, na hata ku-question mwenendo wa viongozi wao katika ngazi zote za serikali

Hili linatokana na hulka za wa Tanzania na lina historia yake katika jamii yetu..wewe unaamini katika BAN, SACK and FIRE..hiyo ni style yako ndio maana umetoa mfano wa CEO..serikali siyo kampuni mkuu..operation za serikali ni lazima ubadili culture za wananchi wako

JK alianza kujenga culture ya uwazi "transparance" on government reports and expenditure..report za CAG zikawa Public ndio kina slaa walipopata mdomo mrefu..miaka yote 10 ya mkapa ripot hiyo ni siri ya rais na viongozi wake...ok...kwanini alifanya wakati ana uwezo kuficha na hakuna mtu wa kummuliza kikatiba... alitaka wananchi waelewe, wafuatilia na wahoji viongozi wao..hii nakwamambia imesaidia sana kuwajengea capacity wananchi wetu...mijini na vijijini

Huwezi kukurupuka kuadhibu kufukuza na kushutumu watu kama afanyavyo lowassa bila kuandaa wananchi na wanachi kuwa tayari kuwaaadhibu pia...

Kama ambavyo wewe uko tayari kuona kina Lowassa wanaadhibiwa hayo ni matokeo ya style ya JK..sasa wewe una style yako usifikiri ndio popular style..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…