Akiwa taabani kitandani,mchungaji alimwita lawyer mmoja na banker mmoja ambao ni waumini wake.Lawyer na Banker waliitikia wito haraka.Walipofika,mchungaji alimwambia Lawyer asimame kushoto kwa kitanda na Banker asimame kulia.Baada ya Lawyer na Banker kujipanga,mchungaji hakusema neno tena,akayaelekeza macho yake darini.Lawyer ikabidi amuulize mchungaji;"inakuwaje umetuita halafu huongei,unatazama juu tu?".Mchungaji akajibu;"Yesu alipokufa msalabani,alikufa katikati ya wezi wawili,na mimi nataka nife kama alivyokufa yesu katikati ya wezi wawili!".